Tafuta

Papa awashutukiza vijana elfu 6 wa Ubelgiji wakiwa katika mkesha wa maombi

Hatua nyingine ambayo haikupangwa kwa upande wa Papa mara baada ya kukutana na Wajesuit,alikwenda kwenye jengo la Maonesho ya Bruxessels,lililo karibu na Uwanja wa Mfalme Baudouin ambapo ataadhimisha Misa,kuwasalimia vijana waliokusanyika tangu mchana wakiwa katika Mkesha uitwao:Tumaini la Furaha.”

Na Salvatore Cernuzio – kutoka  Bruxelles

Walipotangaza kutoka jukwaa la Maonesho ya Bruxessels, walikatiza nyimbo na kwaya na kusikia kishindo kikubwa cha furaha, saa moja kabla, kwamba “Papa Francisko atakuja hapa, kati yetu!” Kwa njia hiyo mwishoni mwa mkutano na Wajesuit wapatao mia moja kutoka Ubelgiji na nchi jirani, na mara baada ya kutembelea Chuo Kikuu Katoliki cha Louvain, Baba Mtakatifu Francisko alitaka kwenda tena jioni sana tarehe 28 Septemba kwenye jengo lililo karibu na Uwanja wa Mfalme Baudouin mjini Bruxessels, ambapo Dominika ataadhimisha Misa asubuhi ili awasalimie binafsi takriban vijana elfu 6 waliokusanyika hapo kwa ajili ya mkesha uliopewa jina: “Tumaini linalotokea.” Tukio la kidugu ambalo ni karibu na kusema siku ndogo ya vijana (WYD )ili kusubiri sherehe ya siku ya Papa, Dominika itakayokuwa ndiyo hatua ya mwisho akiwa nchini Ubelgiji, huku wakiimba, wakicheza, wakiomba na kupiga kambi usiku, ndani ya jengo hilo.

Misalaba katika Jukwaa la tamasha ya mkesha wa vijana huko Ubelgiji
Misalaba katika Jukwaa la tamasha ya mkesha wa vijana huko Ubelgiji

Kufika kwa Papa

Washiriki hao kutoka Ubelgiji lakini pia kutoka nchi jirani, sio vijana pekee yake bali hata familia zenye watoto wachanga, mapadre, watawa, makundi ya mahujaji, wakiwa na bendera na mabango, kanga na kofia, walifikiri kwamba wangemuona Papa kesho yake. Badala yake, ilikuwa  saa 2.40 usiku, kwa wimbo wa ”Jesus Christ Superstar” - usioweza kuepukika katika kila tukio la vijana - pazia jeusi kwenye jukwaa lilifunguliwa na Papa akaonekana, katika kiti cha magurudumu, kati ya moshi na taa za rangi ya zambarau zikioneshwa misalaba miwili mikubwa na taa. Simu mahiri zote ziliinuliwa zikiwa zinawaka kusubiri, bendera za rangi tatu za Ubelgiji au manjano nyeupe ya Vatican na vifijo vya kishindo huku Papa Francisko akichukua nafasi yake katika kiti cheupe na kijana mwitaliano aliyekuwa akimwomba kupiga picha: “Selfie! Kisha, kwa upande wa Papa, altazama umati wa watu ambao ulikuwa unakaribia zaidi vizuizi, mikono yake iliyoinuliwa kwa salamu na rahisi: “Habari za jioni!” Na ndiyo ulikuwa mwanzoni wa yale ambayo mara moja yakawa mazungumzo.

Papa katika mkesha wa maombi
Papa katika mkesha wa maombi

Pigeni kelele!

“Nawauliza swali, mnajua vijana wanafanya nini? Nitasema: vijana hupiga kelele! Na ukimpata kijana kama huyu, Papa aliigiza ishara  ya kukaa,  ya uvivu… kijana huyu hana ujana. Ninawapa ushauri: msonge mbele. Mpiga kelele, muwe na kumbukumbu ya Bwana kila wakati na kumbukumbu kwa sala.”

Kamwe usiwatazame wengine kutoka juu kwenda chini

Hotuba hiyo ilionekana kuwa tayari imekwisha, lakini Papa alikatiza makofi ili kutoa ushauri: “Tafadhali wasaidie wengine. Ninawambia jambo moja, swali moja: ni vizuri, kutanzama mtu kuanzia juu hadi chini? Hapana, ni kumwinua kutoka chini. “Lakini kuna hali ambayo unaweza kumtazama mtu kutoka juu kwenda chini.  Je! mnajua hali hiyo ? Ni kumtazama mtu  kutoka juu kwenda chini tu kwa ajili ya kumsaidia kuinuka."

Papa akielekeza mtoto mdogo mikononi mwa mama yake
Papa akielekeza mtoto mdogo mikononi mwa mama yake

Mtoto mchanga ni mkubwa kuliko wote

Kutoka katikati ya jukwaa, Papa Francisko alielekeza kidole kwa mtoto mchanga mikononi mwa mama yake: “Je! Mnaona Yule mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko ninyi nyote, kwa sababu Yesu alituambia kwamba aliye mkuu kuliko wote ni yule aliyejifanya kuwa mtoto.” Wote walipiga makofi tena, safari hii kwa yule mdogo na Papa ambaye wakati huohuo alihitimisha: “Msiache maombi. Sasa ninawapa baraka. Nous nous verrons demain yaani “Tutaonana kesho.”

Papa alimbariki mtoto
Papa alimbariki mtoto

Salamu kwa umati

Mama huyo kijana baadaye alionekana karibu na Papa Francisko akiwa na mtoto mchanga, ambaye wakati huo huo alikuwa mhusika mkuu wa jioni hiyo. Papa Francisko alimbariki huku akiwa tayari ameshaanza kububujikwa na machozi kutokana na kelele na makofi ya mikono yake. Kuanzia hapo, ni kuaga na mwisho wa siku ya wazi ambayo ilihitimishwa na tukio lisilopangwa.

Selfie zilikuwa karibu kila mmoja na simu mkononi
Selfie zilikuwa karibu kila mmoja na simu mkononi
Papa na vijana katika mkesha
Papa na vijana katika mkesha
Mkesha wa vijana na Papa
28 September 2024, 22:30