Nia za Baba Mtakatifu kwa Mwezi Oktoba 2024:Kwa ajili ya Utume wa Pamoja!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Nia ya maombi ya kila mwezi ya Papa Francisko kwa mwezi wa Oktoba 2024 ni “kushirikishana utume pamoja,” ambapo Baba Mtakatifu” analialika Kanisa kuombea nia hii katika Video ya Sisi sote kama Wakristo tunawajibika kwa utume wa Kanisa, kwa sababu hiyo kwa pamoja tunapaswa kusafiri njia ya sinodi.” Huu ndio mwaliko ambao Baba Mtakatifu Francisko anatoa katika ujumbe wake kupitia Mtandao wa Maombi ya Ulimwengu wa Papa. Kazi ya Kipapa, ambayo dhamira yake ni kuwahamasisha Wakatoliki kwa njia ya sala na matendo mbele ya changamoto za binadamu na utume wa Kanisa anaohimiza kwa: “Tunaomba kwamba Kanisa liendelee kuunga mkono kwa kila njia mtindo wa maisha ya sinodi, kwa ishara ya uwajibikaji, kukuza ushiriki, ushirika na utume wa pamoja kati ya mapadre, watawa na walei.”
Kuwajibika kwa pamoja katika utume
Papa ameeleza kwamba Wakristo wote, walei, mapadre na watawa wanawajibika pamoja katika utume, kwa sababu tunashiriki na kuishi katika ushirika wa Kanisa. Mapadre si viongozi wa walei, bali ni wachungaji wao na Yesu alituita sisi, mmoja na mwingine kwamba sisi ni jumuiya” na kwa sababu hiyo tunakamilishana kwa pamoja.” Papa alibanisha. “Haijalishi wewe ni dereva wa Basi, wakulima au wavuvi, kwa sababu kila mtu ana utume sawa wa kuwa shuhudia maisha yetu, kila mmoja akichangia kwa kile anachofanya vyema. Walei, waliobatizwa, wako katika Kanisa nyumbani na lazima walitunze na ndivyo ilivyo kwetu sisi makuhani,na waliowekwa wakfu.”
Tunawajika sote katika utume
Papa amesisisitiza kuwa: “Tunawajibika pamoja katika utume, tunashiriki na kuishi katika ushirika wa Kanisa. Picha zinazoambatana na ujumbe wa Fransisko zinaonesha utajiri wa watu wa Mungu: huduma mbalimbali ndani na nje ya parokia, karama mbalimbali, nyakati za maisha ya kawaida. Wanaambiwa na Jimbo la Brooklyn, lenye makanisa 200 ambapo Misa huadhimishwa katika lugha 26 tofauti, kutokana na kuwepo kwa wahamiaji wengi. Kwa kuhusisha kikundi cha wataalamu wa mawasiliano ya kidini, walei wa Jimbo la Amerika ni mfano wa utume wa pamoja.
Jumuiya ya Brooklyn inajitahidi kushiriki
Utayarishaji wa video ulioambatana na maneno ya Papa ulisimamiwa na DeSales Media, hali halisi inayofanya kazi katika mawasiliano na vyombo vya habari katika Kanisa la Brooklyn, kwa msaada wa Mfuko wa Kimataifa wa Sala ya Papa na na ushirikiano na Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu. “Kupitia ushirikiano wetu na 'DeSales Media', tumeakisi michango ya walei katika Jimbo letu na kutoa changamoto kwa waamini kuunda jumuiya ya imani na huduma shupavu, yenye furaha na ukaribishaji,” alisema hayo Askofu Robert J. Brennan, wa Jimbo la Brooklyn, akiongeza kwamba timu “inajitahidi kila siku kufanya sehemu yao katika kushiriki utume.” “Kama wataalamu wa mawasiliano, tumeitwa kuweka talanta na uzoefu wetu katika huduma ya Kanisa, alisema hayo Dominic Ambrosio, mkurugenzi wa programu na uzalishaji katika Vyomvo vya habari vya ‘DeSales Media’, akitumaini kazi hii itawatia moyo wengine kushiriki talanta na imani zao hata zaidi.
Mwaliko wa pamoja
Mwezi Oktoba ambapo mkutano wa sinodi unaadhimishwa jijini Roma, hitimisho la safari iliyoanza miaka mitatu iliyopita na iliyojaa matarajio, shauku na matumaini ni wakati muhimu,” aliakisi Padre Frédéric Fornos, mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Sala ya Kimataifa ya Papa, kuwa ni wakati wa kusikiliza, katikati ya mapambano ya kiroho ambayo bila shaka yatakuwepo, kwa kile ambacho Roho wa Bwana anaambia Kanisa.” Padre Mjesuit aliakisi kwamba katika video “Papa Francisko aliweka mkazo juu ya kile ambacho ni muhimu: “Tunawajibika kwa ushirikiano katika utume.” Njia, kama Papa anavyoonesha, ambayo inapaswa kuwa ya asili, kwa kuwa sisi sote tumebatizwa katika Kristo. Hata hivyo, ukweli kwamba inachukua miaka mitatu kufahamu umuhimu wake unathibitisha ukubwa wa changamoto ambayo Kanisa linajikuta likikabiliana nayo katika njia yake kuelekea kwenye sinodi ya kweli”, aliendelea Padre Fornos, ambaye anakumbuka maneno yaliyorudiwa mara kadhaa na Papa Francisko: “ Bila maombi hakutakuwa na Sinodi.” Sala pekee ndiyo inayoweza kubadilisha mioyo iliyoambatanishwa na mapokeo ya kibinadamu na maslahi binafsi na kulifanya Kanisa kuwa aminifu zaidi katika Injili,” anahitimisha Mkurugenzi wa Mtandao wa Kimataifa wa Nia za sala za Papa, kwamba "katika nia ya Papa kwa mwezi wa Oktoba anaona kutiwa moyo “kuungana katika sala kwa ajili ya Sinodi, ili iwe ni wakati wa kweli wa kukutana, kusikilizana na kupambanua jumuiya, kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu”.