Tafuta

Mwenyeheri mpya Ján Havlík aliyekuwa mseminari wa shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo huko Slovakia. Mwenyeheri mpya Ján Havlík aliyekuwa mseminari wa shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo huko Slovakia. 

Papa akumbuka mwenyeheri mpya Ján Havlík,Mseminari huko,Šaštín

Papa amesema:Kijana huyu aliuawa mwaka 1965,wakati wa mateso ya utawala dhidi ya Kanisa katika nchi iliyokuwa inaitwa Czechoslovakia.Ustahimilivu wake katika kushuhudia imani katika Kristo uwe faraja kwa wale ambao bado wanapatwa na majaribu kama hayo leo hii.Alitangazwa kuwa Mwenyeheri tarehe 31 Agosti 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 1 Septemba 2024 mara baada ya tafakari ya Neno la Mungu, kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka tuko la kutangazwa Mwenyeheri mpya huko Šaštín, nchini Slovakia, tarehe 31 Septemba 2024 kwa Mtumishi wa Mungu Ján Havlík, mseminari wa Shirika la Utume  lililoanzishwa na  Mtakatifu Vincent wa Paulo. Papa alisema: “Kijana huyu aliuawa mwaka 1965, wakati wa mateso ya utawala dhidi ya Kanisa katika  nchi iliyokuwa inaitwa Czechoslovakia. Ustahimilivu wake katika kushuhudia imani katika Kristo uwe faraja kwa wale ambao bado wanapatwa na majaribu kama hayo leo hii. Kwa njia hiyo ameomba wampigie makofu Mwenyeheri mpya…

Kuhusu Mwenyeheri Ján Havlík wa Slovakia

Kuhusiana na Mwenyekeri mpya alikuwa Mtu mwenye usawaziko, mwenye furaha, mwenye moyo mkunjufu na anayejali mahitaji ya wengine ambaye, baada ya kukamatwa, aliona kuzorota kwa afya yake. Hayo yalisemwa na Kardinali Marcelo Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, wakati wa mahubiri yake na kueleza mfano wa mwanaseminari wa Kislovakia, tarehe 31 Agosti 2024  huko Šaštín, wakati wa  kuadhimisha Misa kwa ibada ya kutangazwa mwenye heri mtumishi wa Mungu mbele ya Basilika ya Mateso Saba ya Bikira Maria.

Alizaliwa 1928 na kifo 1965

Ján Havlík alizaliwa tarehe 12  Februari 1928, alikufa ghafla tarehe 27 Desemba,1965, miaka mitatu tu baada ya kuachiliwa huru baada ya kuteswa kimwili na kisaikolojia kwa miaka 14, kuhojiwa kwa ukali, kutengwa kwa muda mrefu na kuhukumiwa kazi nzito, lakini kkubaki na imani nguvu za kustahimili kila jambo. Kabla ya kufa aliwasamehe watesi wake. Upendo wa Kristo ni nguvu inayotufanya tushinde udhaifu, nguvu inayotufanya tushinde woga, nuru inayotufanya tushinde giza, alisema Kardinali, ambaye alimfafanua Ján kuwa mtu wa tumaini . Ilikuwa fadhila ya matumaini ambayo ilimfanya kukua na kuunga mkono wito wake.  Ishara ya matumaini, kiukweli, tayari ni chaguo la kuwa mfuasi wa Mtakatifu Vincent wa Paulo, mtakatifu aliyetoa tumaini kwa maskini na wanaoteseka ambao walikutana nao.

Kuhusu yeye alibainisha kwamba: “Alidhihirisha kina chake cha kiroho kwa njia kali zaidi iwezekanavyo katika kushiriki mateso, katika kuwahamasisha wengine kuwa na matumaini licha ya kupitia matatizo mengi.” Wakati wa kifungo chake, Ján Havlík alikutana na Padre mmoja wa Kisalesiani Titus Zeman, aliyetangazwa mwenyeheri mnamo mwaka wa 2017. Kwa mujibu wa Kardinali Semeraro alisema:“Alikuwa mwathirika wa utawala uliotaka kuharibu hali ya kidini na hasa Kanisa Katoliki na wahudumu wake, na alikumbusha kwamba  kulingana na ushuhuda uliokusanywa, gerezani Ján alinakili usiku, akiandika kwa penseli na pia kuwatengenezea wengine nakala, kulinga na kitbu cha  ‘Jacques Maritain's integral Humanism’, takriban kurasa 350. 

Wakati wa misa ya Kutangwazwa mwenyeheri Havlik
Wakati wa misa ya Kutangwazwa mwenyeheri Havlik

Kardinali Semeraro alisema kwamba katika kurasa hizo kulikuwa na maelezo ya yale ambayo Ján alikuwa akipitia: “Ukweli ni kwamba ni mateso ya kujificha; kiukweli ni mapambano dhidi ya Mungu, ya kukomesha dini, kazi ya uharibifu wa kiroho. Kwa hamu ya kushikilia neno la Mungu mfungwa, alisema Semeraro,   mpya uaminifu uliopingana na Mungu, uaminifu kwa wito wake mwenyewe, kwa chaguo lake mwenyewe la upendo kwa wengine.” Kwa hiyo, kielelezo cha uaminifu, Ján Havlík, ambacho leo kinapendekezwa si kwa Kanisa la Kislovakia bali kwa Wakristo wote, kwa hakika, kwa wale wote wanaofanya kazi kwa kupendelea utu wa kibinadamu na kwa ajili ya uhuru wa dhamiri. Hapa kuna hali ya sasa ya kutangazwa kuwa mwenye heri -kwa kuwa katika hali nyingi na hata katika mazingira tofauti ni vigumu, wakati mwingine kishujaa, kubaki mwaminifu kwa Kristo.”

Kardinali huyo alikumbuka ahadi ya Yesu: “yeyote atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiokoa” jambo ambalo linatimia kwa Ján. Umaarufu wa kifo chake cha imani kiukweli ulienea haraka sana, ukienea nje ya mipaka ya taifa na leo, Kanisa linatambua na kulithibitisha hata kwa maneno aliyosema Papa kwamba: Ján Havlík 'alikuwa mfuasi mwaminifu wa Bwana Yesu, ambaye kwake alitoa uhai wake kwa ukarimu, akiwasamehe watesi wake'.”

Wakati wa kufungwa huko Prague
Wakati wa kufungwa huko Prague
01 September 2024, 16:23