Mafuriko makali huko Vietnam. Mafuriko makali huko Vietnam. 

Papa akumbusha waathirika wa kimbunga huko Vietnam na Myanmar

Mara baada ya sala,Papa alikumbuka waathrika wa Vietnam na Myanmar waliokumbwa na mafuriki yaliyosababishwa na kimbunga kikali.Amekumbuka aliyetangazwa mwenyeheri nchini Mexico,Padre Lira wa Shirika la Wamisionari wa Upendo wa Maria Immaculate,aliyefariki 1950.Amekumbusha kuombea Ukraine inayaoteswana nchi Takatifu na Siku ya kitaifa nchini Italia ya Magonjwa nadra.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ninaelezea ukaribu wangu kwa watu wa Vietnam na Myanmar, ambao wanakabiliwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga kikali. Ninawaombea marehemu, waliojeruhiwa na waliohamishwa. Mungu awasaidie waliopoteza wapendwa wao na nyumba zao, na awabariki wale wanaosaidia. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko ameanza mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 15 Septemba 2024 kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katima Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Mwenyeheri mpya 

Papa Francisko aidha alisema kuwa “Jumamosi huko mji wa Mexico Padre Moises Lira wa Shirika la Wamisionari wa Upendo wa Maria Immaculate, aliyefariki mwaka 1950, baada ya maisha yake yote kuwasaidia watu kuendelea katika imani na upendo wa Bwana alitangazwa kuwa Mwenyeheri. Ari yake ya kitume inawahimiza mapadre kujitoa bila kujibakiza kwa ajili ya wema wa kiroho wa watu watakatifu wa Mungu. Aliomba waamini wampingie makofi… na akaona katika uwanja bendera na kusema “Ninaona bendera za Mexico huko ...

Mwenyeheri Moises Lira
Mwenyeheri Moises Lira

“Leo nchini Italia tunaadhimisha Siku ya wagonjwa wa Amyotrophic lateral Sclerosis (ALS). Nawahakikishieni kuwakumbuka  katika maombi wao na jamaa zao; Ninahimiza kazi ya utafiti juu ya ugonjwa huu na vyama vya hiari.”Papa Francisko alisema.

Vita:Ukraine, Myanmar na  Nchi Takatifu 

Na tusisahau vita vilivyoua ulimwengu. Nafikiria Ukraine inayoteswa, ya Myanmar, pia ya  Mashariki ya Kati. Ni waathiriwa wangapi wasio na hatia! Nanawafikiria akina mama waliopoteza watoto vitani. Ni vijana wangapi waliokatisha maisha yao! Ninamfikiria Hersh Goldberg-Polin, aliyepatikana amekufa mnamo Septemba, pamoja na mateka wengine watano, huko Gaza. Mnamo Novemba mwaka jana, nilikutana na mama, Rachel, ambaye alinivutia kwa ubinadamu wake. Ninamsindikiza katika wakati huu. Nawaombea wahanga na kuendelea kuwa karibu na familia zote za mateka. Maliza mzozo wa Palestina na Israeli! Vurugu zikome, chuki zikome! Waachiliwe mateka, mazungumzo yaendelee na suluhu za amani zipatikane.

Salamu kwa mahujaji

Nawasalimu ninyi nyote, Warumi na mahujaji kutoka Italia na nchi nyingi. Hasa, waamini wa parokia ya Mtakatifu  Edwige Regina huko Radom (Poland); kundi la Mapadre Wajesuiti waliokuja Roma kwa masomo; wanafunzi wa Stade (Ujerumani); na washiriki katika relay ya kutembea kutoka Roma hadi Assisi. Na ninawasalimu watoto wa Maria Mkingiwa dhambi ya Asili na amewapongeza. Hatimaye amewatakia Dominika Njema.Wasisahau kumuombea. Amewatakia mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana

Kuhusiana na mafuriko

Tarehe 12 Septemba 2024 ikiwa karinbi ni siku yake ya mwisho huko Singapore, Papa Francisko alielezea ukaribu wake kwa wahasiriwa wa kimbunga mbaya ambacho kimesababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko huko Vietnam. Katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican Papa alisema alihuzunishwa sanakujua juu ya uharibifu uliosababishwa na kimbunga Yagi. Alitoa mshikamano wake wa kiroho kwa waliojeruhiwa na wale wote wanaoteseka na athari zinazoendelea za janga hili. Baba Mtakatifu pia allizikabidhi  roho za marehemu kwa huruma ya upendo ya Mwenyezi Mungu,huku akiomba baraka za Mungu kwa mamlaka za kiraia na wafanyakazi wa dharura wanaotoa msaada.”

Baada ya Angelus
15 September 2024, 15:02