Tafuta

Papa Francisko na Scholas Occurrentes:kataeni vita kwa mazungumzo,kujenga&kukua kirafiki

Kwa kuhitimisha siku ya II mjini Jakarta,Papa alitembelea na kuzindua makao makuu mapya ya Harakati ya Scholas Occurrentes katika Jumba la Vijana la ‘Grha Pemuda,’huko Kusini-Mashariki mwa Asia.Alizungumza na vijana watatu:maelewano na amani na kukamilisha kazi ya Umbo la Moyo la vijana zaidi ya 1500 wa Indonesia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hatua yake ya Mwisho wa Siku ya pili akiwa mjini Jacarta nchini Indonesia kwenye ziara yake ya 45 ya Kitume, Baba Mtakatifu amejikita kutembelea Nyumba ya Vijana ‘Grha Pemuda, ambayo ni makao makuu mapya na ya kwanza ya harakati ya “Scholas Occurrentes” Kusini-Mashariki mwa Asia. Kwa njia hiyo akikutana na vijana hao, na moyo wa hotuba yake ilikuwa ni lwamba “kupigana vita kati yetu daima ni kushindwa, lakini majadiliano yanatufanya kukua.” Ziara yake ilikuwa ni sherehe ya elimu-jumuishi, ambayo inafunza kwamba, kuwa tofauti si uovu, bali ni uzuri wa kipekee kama Christine, msichana ambaye tayari amekuwa mhathirika  wa uonevu, anavyomwambia Baba Mtakatifu katika ushuhuda wake. Siku kuu ya Papa  Francisko ambaye alijadili maelewano na mazungumzo na vijana ni katika muktadha wa Elimu ya kiufundi ya Harakati  iliyozinduliwa mnamo mwaka 2013 na Papa Francisko, kwa mbinu bunifu zinazojumuisha teknolojia, michezo na sanaa.

Umbo la Polyhedron la Moyo limekamilishwa na Papa

Picha ya mhemko iliyooneshwa vizuri na Umbo la lenye pembe nyingi la Moyo ambalo ni kazi mpya ya pamoja ya sanaa ya harakati, muundo uliotengenezwa na vifaa vya asili, vya vitambaa na vilivyosindikwa, na kujazwa na vitu vya kibinafsi, na zaidi ya vijana 1500 na ambapo Papa Francesko alikamilisha na ujumbe wake kabla ya kuondoka hapo. Papa aliwasili wakati jua tayari limeshatua, muda mfupi baada ya saa kumi na mbili jioni huko Indonesia (ilikuwa saa 7mchana  nchini Italia) kwenye Jumba la Vijana, akisafiri mita 600 zinazoitenganisha na Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa kwa kiti cha magurudumu. Njiani aliambatana na rais wa “Scholas Occurrentes” Jose Maria del Corral na baadhi ya wanachama wa harakati hiyo na watoto mia moja kutoka jimbo kuu la Jakarta wakimpokea kwa furaha.

Ziara ya Nyumba ya Vijana

Uani anakaribishwa na watoto wawili ambao wanampatia zawadi, huku wengine wakiimba wimbo, wakisindikizwa na orchestra ya vijana wadogo sana, walianekana,  na vyombo vya muziki vya Indonesia vinavyotumika katika (gamelan ya Java na inayoundwa na seti ya gongs ndogo, sawa na sufuria, vilivychomekwa kwenye mbao). Papa Francisko alifika kwenye Ukumbi wa Mtakatifu Mathias na Mtakatifu Tadeus kwenye ghorofa ya tatu, ambapo alikutana na washiriki wa mpango wa Scholas Aldeas, filamu kuhusu kazi nyingine kubwa ya mfano ya Schola, ya ukuta mrefu sana uliokamilishwa na Papa Francisko huko Cascais, wakati wa Siku ya Vijana Duniani (WYD) huko Lisbon ya 2023. Baadaye, aliendelea katika ukumbi wa Mtakatifu Yakobo kwa mkutano wa faragha na bodi ya wakurugenzi ya Scholas Occurrentes.

Mazungumzo na vijana wa Scholas Occurentes

Hatimaye, Papa Francisko, alifika kwenye ghorofa ya nne ya jengo hilo, na kukaribishwa na vijana 200 kutoka Scholas ya Indonesia, wakiwa wameketi sakafuni, na wageni kutoka nchi nyingine za Asia. Kila mtu alimsalimia kwa kupiga kifua chake kwa mkono, kwa kiwango cha moyo, na Papa alifanya vivyo hivyo. Mara moja aliifikia kazi  ya  umbo hilo  (‘Polyedron of the Heart’,) la pamoja lililohusisha watu 1,500, na  watoto kutoka katika mpango wa elimu huko Jakarta, wakishiriki katika warsha huko Bali, Lombok na Labuan Bajo, na wafungwa wa vituo vitatu vya magereza, ikiwa ni pamoja na wale wafungwa vijana, wanawake na wanaume. Uchongaji unajumuisha vitu vya kibinafsi vya wachangiaji wake, ni nafasi takatifu inayohifadhi kumbukumbu, inaashiria jumuiya ya pamoja; inasimulia, kwa kila njia, historia za washiriki wake, ikichanganya elimu, sanaa na teknolojia na inataka kuwakilisha kauli mbiu ya kitaifa ya Indonesia, “Bhinneka Tunggal Ika” (Umoja katika Utofauti). Papa Francisko alikamilisha kwa ujumbe wake, na kumpatia msichana aliyesindikizana naye nakala ya mhusika wa kitabu cha katuni Mafalda, kilichoundwa na Mtu kutoka Argentina Joaquín Lavado, almaarufu Quino.

Ushuhuda wa Anna, mwalimu wa Kiislamu

Katika chumba kikubwa, nyuma ya kiti chake, ukuta ulijaa mimea ya mikoko, ishara ya ulinzi wa mazingira. Papa alisikiliza kwa makini ushuhuda wa kwanza wa Anna, mtu wa kujitolea wa Scholas, mwalimu na mama, akiwa hijabu kichwani mwake. Mwalimu wa chuo kikuu lakini pia ni mzungumzaji wa radio, alisema alijvyo jiunga  Scholas, akiwa Muislamu kwa sababu anapenda elimu. Aliguswa moyo kwa sababu leo hii, kutoka Kanisa kuu, aliona msikiti, na ambapo alijifunza uvumilivu ambao aliupata baadaye katika harakati hiyo. Aliongeza kusema: “Leo hii Scholas kwangu ni nyumba inayoendelea kila wakati, shamba ambalo vijana hukua kama maua.”

Mazungumzo na Bryan mdogo sana

Bryan mdogo sana, akiwa amevalia fulana nyeupe ya Scholas, alisisitiza kuwa katika harakati hizo “tunastarehe kwa kila mmoja wetu, sote tuna marafiki na dini au imani zingine.” Na alieleza kuwa wengi wamesimulia matukio yao mabaya, ubaguzi, uonevu mtandaoni na kupendeza watu ambao wanajifanya bila kuangalia tofauti, bila kubaini nani yuko sahihi na nani asiyefaa.” Papa Francisko alishukuru na kuinua kidole gumba kuonesha sawa yake. Kisha alichukua kipaza sauti na kusema kwamba alizungumza vizuri juu ya ukweli, kwa sababu wakati mwingine ukamilifu wa kufanya hukosa. Kuna mambo matatu: kile tunachofikiri, kile tunachosema na ukweli tunaopitia. Na kuna hatari ya kuwa na mgando, mtu anayefikiria jambo moja lakini anafanya jingine, hana umoja, badala yake ukomavu wa mtu ni kufikiri, kuzungumza na kuishi kwa maelewano.

Maelewano ni jumuiya inayotembea, katika utofauti

Papa alisisitiza kuwa “ Kwangu mimi maelewano, ni pale ambapo jumuiya inatembea pamoja, pia kuona utofauti lakini kutembea pamoja, kwa njia ya haki, bila kuona tofauti za kijamii. Amani ni maelewano,na ili kuifanikisha lazima ufuate kanuni hizi: Ukweli ni bora kuliko wazo, umoja ni bora kuliko migogoro, na yote ni bora kuliko sehemu,”Alisisitiza Papa

Christine: Jinsi ya kufundisha amani katika ulimwengu wenye migogoro?

Hatimaye Christine, ambaye pia alivalia fulana nyeupe ya Scholas, anamwambia Papa Francisko kwamba aliteseka kutokana na uonevu, na kwamba mara nyingi tofauti huleta migawanyiko, husababisha migogoro na mara nyingi husababisha uharibifu, hata katika familia. Lakini katika harakati  hiyo tumejifunza kwamba tofauti hizi si uovu, bali ni uzuri wa kipekee. Tumejifunza kuunganisha tofauti zetu, kujenga vifungo vya umoja na kuelewa kwamba tofauti sio njia ya uharibifu, lakini ni hatua kuelekea umoja. Na aliuliza Papa: “Tunawezaje kufundisha amani katikati ya migogoro inayotokea leo?

Chaguo kati ya vita na matusi na kuunga mkono

Maisha lazima tuyaishi kwa tofauti, ikiwa sote tungekuwa sawa, ingekuwa ya kuchosha Papa  Francisko alimjibu, akisifu ujasiri wake. Katika tofauti, kunaweza kuwa na migogoro au mazungumzo. Ikiwa nchi mbili ni tofauti, nifanye nini? Mazungumzo au vita? Tamaa ya kuwa na kila kitu mkononi huleta vita. Neno sahihi ni kutembea pamoja.” Papa alikumbuka kwamba “Chaguo, ni kati ya kupigana vita na kutukanana, au siasa za mkono ulionyooshwa, wa kukumbatia, wa upendo wa kidugu, na daima kusonga mbele katika mazungumzo, kwa kujadili lakini kwa pamoja. Wakati mwingine, alifafanua, “lazima tujadiliane kati yetu, lakini tujadili kama ndugu, ili kuendeleza njia ya amani. Kufanya vita na mabishano ni jambo baya, lakini si vibaya kubishana kama marafiki na kubadilisha mawazo.” Kwa kuhimiza alisema “msisahau: vita kati yetu daima ni kushindwa, na badala yake kujadiliana na marafiki hutufanya kukua.”

Zawadi na Mama  Huruma

Wakati wa zawadi Papa alipokea baadhi ya jamvi lililpshonwa na kupambwa na wafungwa vijana wa vituo vitatu vya magereza, walioshiriki katika mpango wa umbo wa polyhedron la moyo. Na aliwaachia kama zawadi kwa Scholas Occurrentes Picha ya Mama Mple wa Korsun', inayoitwa Korsunskaya, ambayo hadi Mapinduzi ya Oktoba yalihifadhiwa katika Kanisa la Kulala huko Kremlin.

Mikoko na baraka kwa wote

Mwishoni, Baba Mtakatifu alipanda mikoko kwa ishara ya kumbukumbu ya mkutano huu wa kihistoria, pamoja na Waziri wa Mazingira Luhut na kama mwanzo wa mradi wa mazingira na maendeleo endelevu. Wakati wa Baraka, aliwaeleza kwamba baraka “inamaanisha kusema mema kwa kila mtu mwingine, ni kuwatakia mema. Hapa nyinyi ni wa dini mbalimbali, lakini Mungu ni mmoja tu.”Aliwaalika kila mtu kusali kwa ukimya na kisha kutoa “baraka kwa wote”: “Mungu awabariki kila mmoja wenu, abariki matamanio yenu, abariki familia zenu, abariki sasa yenu na abariki maisha yenu ya baadaye.” Papa Francisko anaondoka katika Jumba la Vijana saa 7.45 jioni kwa saa za huko, ikiwa ni saa 8:45pm nchini Italia, sio kabla ya kubariki picha na vitu ambavyo vimeandaliwa kwa ajili yake kwenye meza kubwa.

Papa na Scholas Occurrente huko Indonesia

 

04 September 2024, 16:22