Papa amefika nchini Papua New Guinea

Hatua ya pili ya Ziara ya 45 ya kitume ya Papa imeanza,kati ya Port Moresby na Vanimo kuanzia Ijumaa tarehe 6 hadi tarehe 9 Septemba 2024.Ratiba yake huko Oceania itakuwa kukutana mamlaka,mashirika ya kiraia na kidiplomasia,vituo viwili watoto walemavu na wasiojiweza na hatimaye maaskofu wa Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon,mapadre,mashemasi na waliowekwa wakfu.

Vatican News

Ziara ya Papa huko Papua New Guinea na ndege ya papa ilitua saa 1.06, jioni  kwa saa za huko Port Moresby, ambapo ilikuwa ni saa 5.06 , asubuhi kwa saa za Roma. Ndege hiyo, A330 ya Garuda Indonesia, mbebaji wa kitaifa, ilimsindikiza Papa Francisko, wasaidizi wake na waandishi wa habari wapatao zaidi ya 70 kwenye bodi mwanzoni mwa hatua ya pili ya Ziara ya 45 ya kitume, ambayo itamwona Papa katika sehemu hii ya Oceania hadi Septemba 9 na safari ya  mji wa Vanimo pia.

Mapokezi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jacksons

Wakimkaribisha Papa Francisko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jacksons ambapo ni Papa wa pili nchini Papua New Guinea  katika historia, baada ya Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo  mwaka 1984 - baada ya kurusha mizinga 20 alikuwa Naibu Waziri Mkuu na watoto wawili waliovalia mavazi ya kiutamaduni wakiwa na maua kama zawadi walimpatia. Mara tu baada ya hafla ya kukaribisha, Papa Francisko alilekea makao makuu ya Ubalozi wa Vatican ambao  ratiba  rasmi itaanza  asubuhi, tarehe 7 Septemba 2024 , saa 3.45 asubuhi.

Ratiba ya 7 Septemba

Siku ya Papa itafunguliwa kwa ziara ya heshima kwa mkuu wa nchi ya  Papua New Guinea katika Ikulu ya Serikali, ikifuatiwa na mkutano na mamlaka, mashirika ya kiraia na wanadiplomasia katika Apec Haus. Siku hiyo pia itamwomba Papa, katika Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Caritas,  Huduma watoto wa Barabarani, katika shirika linalowatunza pia  wasiojiweza, na watoto wa Huduma ya  Callan ambao ni mtandao unaotunza watu wazima na watoto wenye ulemavu. Kufunga siku ni kwenda kwenye madhabahu ya Maria Msaada wa Wakristo, pamoja na kukutana  Maaskofu wa Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na makatekista.

Papa amefika Papua New Guinea
06 September 2024, 13:36