2024.09.29 Kardinali Alexandre do Nascimento,Askofu Mkuu Mstaafu wa Luanda nchini Angora alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 99. 2024.09.29 Kardinali Alexandre do Nascimento,Askofu Mkuu Mstaafu wa Luanda nchini Angora alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 99. 

Papa amekumbuka Kardinali do Nascimento:mtu jasiri na huru!

Alielekeza hatua zake kwa manufaa ya wote,hadi kufikia hatua ya kushirikiana na Vatican kwa bidii kwa ajili ya maskini na wahitaji zaidi,akiongoza mwelekeo wa Caritas Internationalis.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko ametoa rambirambi zake kwa kifo cha Kardinali Alexander do Nascimento, Askofu mkuu mstaafu wa Luanda, nchini Angola aliyefariki Jumamosi tarehe 28 Septemba 2024 akiwa na umri wa miaka 99. Papa anamfafanua kama “mchungaji mashuhuri” katika telegramu ya lugha ya Kireno iliyoelekezwa kwa Askofu Mkuu wa sasa Filomeno do Nascimento Vieiria Dias, lakini pia kwa maaskofu wasaidizi, mapadre, jumuiya za watawa na waamini wa Jimbo kuu, pamoja na wanafamilia na wale ambao "amehuzunishwa"nchini Angola kwa kifo chake. “Imani katika Kristo na tumaini la uzima wa milele vilimfanya kuwa mtu jasiri na mtu huru, awezaye kuongoza hatua zake kwa ajili ya manufaa ya wote, hadi kufikia hatua ya kushirikiana na Baraza la Kipapa katika bidii yake ya kuwapendelea walio maskini zaidi na wahitaji zaidi; kuongoza mwelekeo wa Caritas Internationalis”.

Udhihirisho wa uso wa Yesu

Kardinali Do Nascimento alikuwa mmoja wa viongozi wa kikanisa walioleta Kanisa la Angola na Afrika katika milenia mpya. Alipokea Kofia ya Ukardinali kutoka kwa Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo 1983, mwaka mmoja baada ya kutekwa nyara wakati wa ziara ya kichungaji na kikundi cha watu wenye silaha ambao wakamwachilia huru mwezi mmoja baadaye. Kwa hakika, Papa Fransisko amekumbuka "utunzaji uliotolewa na mpendwa Dom Alexandre kwa kundi lake katika nyakati za taabu na ngumu, umekuwa kwa kila mtu kielelezo cha uso wa huruma wa Yesu, Msamaria mwema wa wanadamu". Kisha Papa alitoa shukrani kwa Mungu kwa kazi ya Kardinali na kumsihi Bwana "kumfunika mtumishi wake mwaminifu kwa mwanga wa rehema na kufungua milango ya uzima kwa utimilifu.” Hivyo ametoa  baraka kwa wale wote watakaoshiriki katika mazishi hayo.

Papa atoa rambi rambi kufuatia na kifo cha Askofu Mkuu Mstaafu wa Luanda Angola
30 September 2024, 16:55