2024.09.04 Papa alitembelea "Handaki ya Urafiki" 2024.09.04 Papa alitembelea "Handaki ya Urafiki"  (Vatican Media)

Jakarta,Papa atembelea Handanki la Urafiki:kutembea pamoja katika nuru kamili

Ningependa kuwaambia kwamba ninyi ndiyo nuru inayoangaza,pamoja na urafiki wenu,maelewano mnayokuza,msaada wenu wa pande zote na kwa kutembea pamoja kunawaongoza,mwisho wa barabara,kuelekea nuru kamili.”Ndiyo maneno ya hotuba fupi ya Papa akiwa katika 'Handaki la Urafiki' linalotengenisha Kanisa la Mpalizwa na Msikiti wa Istqlal.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akitembelea Handaki la Urafiki (Tunnel of Friendship) linalotengenisa Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa na Msikiti Mkuu huko Jacarta nchini Indonesia tarehe 5 Septemba 2024  alitoa hotuba fupi ambapo aliwashukuru wote kwa sababu ya "Harandaki ya Urafiki inayotaka kuwa mahali pa mazungumzo na kukutana. Ikiwa tunafikiria juu ya handaki, tunafikiria kwa urahisi njia ya giza ambayo, hasa ikiwa tuko peke yetu, inaweza kututisha. Hapa, hata hivyo ni tofauti, kwa sababu kila kitu kinaangazwa," amesema Papa na kuongeza kuwa: “Ningependa kuwaambia, hata hivyo, kwamba  ninyi ndiyo  nuru inayoangazia, pamoja na urafiki wenu, maelewano ambayo mnakuza, msaada wenu wa pande zote, na kwa kutembea kwenu pamoja kunawaongoza, mwisho wa barabara, kuelekea mwanga kamili.”

Papa wakati wa mkutano wa kidini
Papa wakati wa mkutano wa kidini

Papa Francisko akiendelea amesisisitiza kwamba, “Sisi waamini, ambao ni wa mtamaduni  tofauti za kidini, tuna jukumu la kutekeleza: kusaidia kila mtu kupitia handaki na wakati macho yetu yakielekezwa  kwenye nuru. Hivyo, mwishoni mwa safari, tunaweza kutambua, katika wale waliotembea pamoja nasi, kaka, dada, ambao tunaweza kushiriki maisha na kusaidiana. Kwa ishara nyingi za tishio, kwa nyakati za giza, tunalinganisha ishara ya udugu ambayo, kwa kuwakaribisha wengine na kuheshimu utambulisho wao, inawahimiza kuchukua njia ya pamoja, iliyofanywa katika urafiki, na ambayo inaongoza kwenye nuru.”

walioshiriki Mkutano wa Kidini
walioshiriki Mkutano wa Kidini

Papa ametoa shukurani “kwa wale wote wanaofanya kazi wakiwa na hakika kwamba tunaweza kuishi kwa upatanisho na amani, tukifahamu hitaji la ulimwengu wa kidugu zaidi. “Ni matumaini ya Baba Mtakatifu “kuwa jumuiya zetu zinaweza kufunguliwa zaidi kwa mazungumzo ya kidini na kuwa ishara ya kuishi pamoja kwa amani ambayo ni sifa ya Indonesia.” Na hatimaye Papa Francisko ameinua sala yake kwa Mungu, Muumba wa wote, ili awabariki wote ambao watakatisha hadhini hiyo katika roho ya urafiki,maelewano na udugu.

Hutuba ya Papa katika Handaki ya Urafiki
05 September 2024, 11:26