Papa Francisko amekutana na viongozi wa kiraia wa Indonesia

Katika tukio la kwanza la umma la ziara yake ya Kitume katika taifa la Asia,akihutubia Mamlaka za kiraia na Mashirika ya Kidiplomasia,Baba Mtakatifu Francisko amekazia juu ya kauli mbiu ya Taifa kuhusu Umoja katika Utofauti na kuahidi uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki kwa mazungumzo ya kidini na maelewano ya kiraia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika tukio la kwanza umma, akiwa katika Ziara ya 45 ya Kitume ambayo inaongozwa na kauli mbiu: “Imani, udugu, huruma” tarehe 4 Septemba 2024 akihutubia mamlaka za kiraia na mashirika ya kidiplomasia, Baba Mtakatifu Francisko amekazia juu ya kauli mbiu ya taifa hilo  kuhusu umoja katika utofauti na kuahidi uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki kwa mazungumzo ya kidini na maelewano ya kiraia.  Amekazia juu ya uzuri mkubwa wa ardhi  hiyo, usawa na heshima kwa haki, lakini vile vile  imani potofu, ardhi ya familia na watoto, uwiano wa busara na laini kati ya tamaduni na itikadi tofauti; upatanisho,  kuwa ziwe miongoni mwa malengo.

Papa akizungumza na mamlaka ya kiraia na wanadiplomasia
Papa akizungumza na mamlaka ya kiraia na wanadiplomasia

Papa amekuwa na rejeo maradufu kwa Mungu na hitaji la baraka zake, zilizoandikwa katika Dibaji ya Katiba. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba hiyo amehimiza dhamira ya kupambana na itikadi kali na kutovumiliana, dhamira ya kiraia inayochochewa na imani wazi ambayo inalenga mazungumzo, na sio sura inayoongoza akili ya kuchochea migawanyiko na kuongeza chuki. Ni katika  siku ya kwanza ya ratiba  za Papa katika ardhi ya Indonesia, ambapo baada ya kuwasili tarehe 3 Septemba 2024 na hivyo siku hii ilianza kwa Misa ya faragha iliyoadhimishwa katika Ubalozi wa Vatican na uhamisho uliofuata kwenye ikulu ya rais iliyoko Istana Merdeka kwa sherehe rasimi  ya kumkaribisha na kumtembelea rais wa Indonesia Bwana Joko Widodo.

Baada ya onesho la guaride na nyimbo huku mlinzi wa heshima akiwa amejipanga nje ya ikulu katika mazingira ya sherehe za wanawake, wanaume na watoto waliovalia mavazi ya kiutamaduni, Baba Mtakatifu Fransisko akiwa ameambatana na mkuu wa nchi walifika kwenye Ukumbi wa Hati miliki kwa ajili ya kutia saini Kitabu cha  Heshima ambayo aliacha ujumbe uliofupisha kile  ambacho angesema dakika chache baadaye mbele ya wawakilishi wa taasisi 300 hivi, mashirika ya kiraia na mabalozi kwamba: “Nikiwa nimezama katika uzuri wa Dunia hii, mahali pa kukutana na mazungumzo kati ya tamaduni na dini mbalimbali, ninawatakia watu wa Indonesia wakue katika imani, udugu na huruma. Mungu ibariki Indonesia!”

Papa akikutana na mamlaka ya kiraia
Papa akikutana na mamlaka ya kiraia

Kawa njia hiyo baadaye, Baba Mtakatifu katika hotuba yake  alisisitiza mambo kadhaa shukrani zake kwa Indonesia, inayoonekana kama picha nzuri ya  sehemu tofauti zilizosawazishwa kati ya kila moja na nyingine zinazofanya kazi kwa utengamano wa kijamii uliosawazishwa, pamoja na mchango wa mara kwa mara wa Kanisa mahalia. Hii ni kazi ya ufundi iliyokabidhiwa kwa kila mtu, lakini kwa namna ya pekee kwa hatua inayofanywa na siasa, inapoweka lengo lake la maelewano, usawa, kuheshimu haki za msingi za binadamu, maendeleo endelevu, mshikamano na kutafuta amani, ndani ya jamii na kwa watu na mataifa mengine. Juhudi, hii ya Indonesia, ambayo Papa ameweka ni kama mfano kwa heshima na mwenendo ambao leo hii  ulimwenguni, huzuia maendeleo ya udugu wa ulimwengu wote, ikiwa ni pamoja na tabia ya kuendesha imani kwa Mungu, ambayo haikutumiwa  kujenga amani, ushirika, mazungumzo, heshima, ushirikiano, udugu, lakini kuchochea migawanyiko na kuongeza chuki.

“Kaka na dada, katika uso wa vivuli hivi, inaburudisha kuona jinsi falsafa inayohamasisha serikali ya Indonesia inadhihirisha hekima na usawa. Kuhusiana na hili, ninayafanya maneno yangu mwenyewe yaliyotamkwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, katika Ikulu hii hii, wakati wa ziara yake mwaka wa 1989. Miongoni mwa mambo mengine, alisema: “Katika kutambua uwepo wa tofauti halali, katika kuheshimu haki za binadamu na haki za kisiasa za raia wote na katika kukuza ukuaji wa umoja wa kitaifa unaozingatia uvumilivu na heshima kwa wengine, ninyi Waindonesia mnaweka misingi ya hilo jamii yenye haki na amani ambayo Waindonesia wote wanajitakia wenyewe na wanayotaka kuwarithisha watoto wao” (Hotuba kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia na kwa Mamlaka, Jakarta, 9 Oktoba 1989). Hata kama nyakati fulani, katika mwendo wa matukio ya kihistoria, kanuni zenye kutia moyo zilizotajwa hapo juu hazijapata nguvu ya kujilazimisha katika kila hali sikuzote, zinabaki kuwa halali na zenye kutegemeka, kama taa inayoonyesha mwelekeo wa kwenda na kuonya juu ya jambo kuu makosa hatari kuepukwa.”

Katika kanda mbalimbali Papa amebainisha tunaona kuibuka kwa migogoro mikali, ambayo mara nyingi ni matokeo ya ukosefu wa kuheshimiana, tamaa isiyo na uvumilivu ya kufanya maslahi yako mwenyewe, nafasi yake mwenyewe, au maelezo ya sehemu ya kihistoria ya mtu mwenyewe yanashinda kwa gharama yoyote, hata wakati hii inasababisha mateso yasiyoisha kwa jamii nzima na kusababisha vita vya kweli vya umwagaji damu. Mfano mwingine ambao Indonesia inatoa ulimwengu kwa Papa Francisko ni kiwango chake cha juu cha kuzaliwa, na familia ambao wana watoto watatu, wanne, watano na wanaosonga mbele, wakati katika maeneo mengine ya dunia suluhisho la kukosekana kwa usawa, kunatokana na kuzuia uzazi, kupunguza utajiri mkubwa zaidi ambao nchi inayo.

Papa akutana na mamlaka ya kiraia
Papa akutana na mamlaka ya kiraia

Aina ya uchaguzi wa kisiasa unaoendana na kutokuwepo katika baadhi ya matukio ya dhamira ya ufanisi na ya kuona mbali katika kujenga haki ya kijamii. Matokeo yake, sehemu kubwa ya ubinadamu imesalia pembezoni, bila njia ya kuishi kwa heshima na bila utetezi kukabili hali mbaya na inayokua ya usawa wa kijamii, ambayo huzua migogoro mikali. Hitimisho la  Papa Francisko ni kwamba kazi ya wale wanaosimamia masuala ya umma inapaswa kuhamasishwa na imani kwamba amani ni tunda la haki, kwa sababu maelewano, hupatikana wakati kila mtu anajitolea sio tu kwa maslahi yake mwenyewe na maono yao wenyewe, bali kwa nia ya kuwanufaisha wote, kujenga madaraja, kuhimiza makubaliano na mashirikiano, kuunganisha nguvu kwa lengo la kushinda kila aina ya ubaya wa kimaadili, kiuchumi, kijamii, na kukuza amani na maelewano.

“Ninatumaini kwamba kila mtu, katika matendo yake ya kila siku, ataweza kupata msukumo kutoka kwa kanuni hizi na kuzifanya ziwe na ufanisi katika utimilifu wa kawaida wa majukumu yao husika, kwa sababu opus justitiae pax, amani ni tunda la haki. Kiukweli, maelewano hupatikana wakati kila mtu anajitolea sio tu kwa masilahi na maono yake, lakini kwa nia ya mema ya wote, kujenga madaraja, na kukuza makubaliano na mashirikiano, kuunganisha nguvu kwa lengo la kushinda aina yoyote ya ubaya wa kimaadili, kiuchumi au kijamii, na kukuza amani na maelewano. Wapendwa kaka na dada, endeleeni kwenye njia yenu ambayo ni nzuri sana na sahihi. Na kwa hivyo nnawapa baraka kwa watu wote. Mungu ibariki Indonesia kwa amani, kwa mustakabali uliojaa matumaini. Mungu awabariki nyote!”

Papa Francisko na mwenyeji wake
Papa Francisko na mwenyeji wake

Baada ya kuhitimisha hotuba hiyo kwa makofi ya muda mrefu, Papa Francisko aliondoka ofisi ya rais akisindikizwa kwa mara nyingine tena na bendera na shangwe za umati uliovalia mavazi ya kiutamaduni.

Hotuba ya Papa kwa Mamlaka ya Kiraia na wanadiplomasia
04 September 2024, 08:39