Papa akielekea Papua Ne Guinea. Papa akielekea Papua Ne Guinea. 

Papa Francisko anaelekea Papua New Guinea

Ndege ya A-330 ya kampuni ya Garuda Indonesia ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta Soekarno-Hatta saa 4.37 asubuhi kwa saa za ndani (saa 11.37 alfajiri nchini Italia).Kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jacksons huko Port Moresby kunatarajiwa baada ya kivuko cha saa sita ambacho kitamchukua Papa,pamoja na wasaidizi wake na waandishi wa habari,kutoka Asia hadi Oceania.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 6 Septemba 2024  aliondoka katika mji mkuu wa Indonesia kwa kuendelea na  hatua ya pili ya Ziara yake ya 45 ya Kitume ambayo sasa inampeleka nchini Papua New Guinea, ambako atakaa kwa siku mbili, hadi Dominika tarehe 8 Septemba 2024.

Papa ameagwa uwanja wa Ndege wa Jacarta
Papa ameagwa uwanja wa Ndege wa Jacarta

Ndege ya A-330 ya kampuni ya Garuda Indonesia, ikiwa na wasaidizi wa Papa na waandishi wa habari, ilipaa - karibu saa moja baadaye kuliko ilivyopangwa - kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jakarta Soekarno-Hatta,  saa 4.37 asubuhi kwa saa za ndani  wakati ilikuwa ni saa (11.37 alfajiri nchini Italia).

Watu wengi walitaka kumgusa Papa
Watu wengi walitaka kumgusa Papa

Kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jacksons huko Port Moresby kumepangwa, kulingana na ratiba, saa 12.50 jioni (saa za ndani). Masaa sita ya kuvuka kwa kuhama kutoka bara la Asia hadi Oceania. Baba Mtakatifu baada ya Ibada ya Misa Takatifu ya faragha, aliondoka kwenye Makao Makuu ya Ubalozi wa Vatican huko  Jakarta, akiwaaga kwa upole wafanyakazi na wafadhili. Alifika uwanja wa ndege akiwa na gari jeupe aina ya Toyota alilotumia kusafiri siku hizi tangu akifike huko; njiani vijana kadhaa walishuhudia upendo wao, ikiwa ni pamoja na mama wenye watoto. Karibu na mlinzi wa heshima, katika ujumbe wa serikali, Waziri wa Masuala ya Kidini, Yaqut Cholil Qoumas alimsalimia na kumshukuru Papa Francisko kwa muda mrefu kwa ziara yake nchini humo.

Papa akiwa anaondoka kuelekea Uwanja wa Ndege
Papa akiwa anaondoka kuelekea Uwanja wa Ndege

Papa  Francisko pia alisalimiana na Kardinali Ignatius Suharyo Hardjoatmodjo. Ameonesha urafiki na heshima kama ilivyooneshwa wakati wa kuagwa katika nchi hiyo. Akisindikizwa katika  kiti cha magurudumu, Papa Francisko aliwabariki wale wote waliomkaribia, wakiinama kama tamaduni yao. Uzuri  na hai ni kumbukumbu ya watu wa kukaribisha walioishi siku za umoja wa sherehe, katika kujitolea kuishi kwa udugu dhidi ya kila aina ya itikadi kali na unyonyaji wa imani kwa migogoro.

Kutua huko Port Moresby-Papua New Guinea

Kituo cha Port Moresby pia inajulikana kama Pom Town, ambao ni mji mkubwa na bandari kuu katika Papua New Guinea. Iko katika Ghuba ya Fairfax, kwenye pwani ya kusini ya nchi, inayotazama Ghuba ya Papua. Baada ya sherehe rasimi ya kuwakaribisha itakayofanyika hapo uwanja wa ndege, itakuwa jioni, Papa atahamia Ubalozi wa Vatican ulioko kwenye kilima kulikozaliwa kijiji cha kwanza cha watu wa Asili.

Papa akiwa anaelekea Papua New Guinea
Papa akiwa anaelekea Papua New Guinea

Atakuwa na chakula cha jioni kwa faragha na kisha kujiruhusu kupumzika,ili kujiandalia  siku inayofuata, tarehe 7 Septemba 2024 na mkutano na mamlaka na mashirika ya kiraia katika APEC Haus, kituo kikuu cha mikutano mjini huko, kisha kutembelea shule ya wasichana iliyoanzishwa na Masista wa Upendo wa Yesu,na hatimaye mkutano na viongozi wa kichungaji wa Papua na Visiwa vya Solomon.

Telegramu

Akiruka juu ya visiwa vya Kusini-Mashariki mwa Asia, katika telegramu kwa Rais Joko Widodo, Papa Francisko alitoa shukrani zake za kina kwa mamlaka mahalia na kwa wakazi wote kwa msaada na ishara nyingi za udugu katika siku alizokuwa  katika nchi hiyo. Kila wakati akia katika anga la Indonesia kwa kuvuka kufikia hatua nyingine za safari ya kitume, baada ya Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore - Papa alihakikishia kwamba atakumbuka kwa upendo nchi yao ambayo pia ameomba baraka nyingi kutoka kwa Mungu.

Bango la Makaribisho
Bango la Makaribisho
06 September 2024, 07:54