2024.09.04 Papa akutana na Wajesuti huko Indonesia 2024.09.04 Papa akutana na Wajesuti huko Indonesia  (Vatican Media)

Papa Francisko na Wajesuit Indonesia,Spadaro:Ashangazwa na vijana wengi

Mwishoni mwa asubuhi huko Jakarta,baada ya kukutana na rais na mamlaka ya kisiasa na kiraia,Papa alikutana wanashirika 200 wa Shirika la Yesu kutoka visiwani kwa saa moja katika Ubalozi.Mkutano uliozoeleka,mtulivu,alisema katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.Mada nyingi ni pamoja na mazungumzo ya kidini na umuhimu wa kuinjilisha.

Na Salvatore Cernuzio –kutoka Jakarta

Baada ya mamlaka ya kisiasa na kiraia ya nchi, kisha Wanashirika wa Jumuiya ya Yesu iliyomo nchini humo ilikuwa ni miongoni mwa mikutano ya kwanza ya  Papa Francisko huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, katika kituo cha kwanza cha ziara yake ndefu ya Kusini-Mashariki mwa Asia na Oceania (2-13 Septemba). Tendo la kukutana ni utamaduni sasa wa Papa Francisko kwa kila nchi aitembeleayo kukutana na wanashirika wenzake (Wajesuit.) Papa kwa njia hiyo alikutana na Wajesuit 200 kati ya 320 waliopo katika visiwa vyote, tarehe 4 Septemba 2024, asubuhi  5.30  hivi katika ukumbi wa Ubalozi wa Vatican  nchini humo, mahali ambapo Jumanne 3 Septemba mara baada ya kufika alikuwa amewakumbatia maskini, yatima, wakimbizi na wazee.

Papa amekutana na wajesuit wa Indonesia
Papa amekutana na wajesuit wa Indonesia

Maswali na majibu, siri na vichekesho

Mkutano huo ulichukua saa moja na, kama kawaida, ulitiwa alama na mazungumzo ya moja kwa moja yenye maswali na majibu, siri za kibinafsi na vichekesho kadhaa. “Ulikuwa ni mkutano uliotulia, wa kina na mkali na wakati wa familia, kama kwa ujumla  wa Papa Francisko ambaye huwa ametulia sana, na kuhisi yuko nyumbani, kwa hivyo aliweza kutoa maoni ya kwanza juu ya ziara hiyo.” Hayo yametolewa muhtasari na Padre Antonio Spadaro, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na mjumbe wa msafara wa upapa, aliyekuwepo wakati mkutano akiwa ni mwandishi wa habari na Mtaalimungu, akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican vinavyoambatana kwenye ziara hiyo ya kitume. Akiwa na ndugu wa Kiindonesia, hasa, alionesha mshangao na furaha yake kwa kuona vijana wengi na pengine ni jambo ambalo lilinigusa zaidi, Baba Mtakatifu aliona jinsi Wajesuit waliopo katika malezi nchini Indonesia walivyo vijana,” alisisitiza Padre Spadaro.

Mada za mazungumzo, kiutamaduni, utambuzi na sala

Mada nyingi zilishughulikiwa katika mazungumzo ambapo: “Papa alizungumza kuhusu Jumuiya, umuhimu wa utambuzi na sala." Kijana aliye mdogo zaidi alimuuliza  kuwa  "anapata wapi muda wa kusali na akawasimulia baadhi ya matukio,” alieleza Padre Spadaro. Mada zote ambazo zilifungamana na zingine muhimu katika ardhi hii kama vile mazungumzo ya kidini au kiutamaduni, ambayo alisisitiza sana. Hakukuwa na upungufu vikeshesho kwa uzoefu wao binafsi na utani; kama lile lililotamkwa na Papa mwishoni mwa mkutano kwamba: “Tazama, polisi wamefika kunichukua.”

Papa akiwa na Wajesuit wa Indonesia
Papa akiwa na Wajesuit wa Indonesia

Ratiba nzito

"Papa anapenda kuzungumza na ndugu zake, kwa utulivu na kwa njia ya bure na ya hiari, lakini ana ratiba sahihi.” Baada ya mkutano wa asubuhi katika Ikulu ya Rais iliyoko  Istana Negara, alasiri Papa Francisko atakuwa na mikutano mingine miwili iliyopangwa kwenye ratiba saa 10.30 jioni ile ya maaskofu, mapadre, mashemasi, watu waliowekwa wakfu, waseminari na makatekista katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Dhana; saa 11.35 jioni  utawaona vijana wa mtandao wa Kimataifa wa  Scholas Occurrentes katika Jumba la Vijana la ‘Grha Pemuda.’

Mtazamo wa ukweli na utaftaji wa siku zijazo

Kati ya mkutano wote - wa kwanza kati ya mitatu na Jumuiya ya Yesu iliyopangwa wakati wa safari (nyingine mbili zitafanyika Dili na Singapore) - kilichoacha hisia kubwa zaidi kwa Padre Antonio Spadaro ni ‘mwonekano’ wa Papa Francisko. “Katika mkutano huu asubuhi ya leo lakini pia katika mingine ambayo tumekuwa nayo hadi sasa. Papa Francisko anaonaekana  uwezekano katika ardhi hii, uwezekano wa maelewano ndani ya mazingira ya wingi. Hata rais leo hii alizungumzia maelewano na vyama vingi. Ninaamini kuna matumaini hapa kwa mustakabali ulio hatarini kama huu, wakati ulimwengu umegawanyika na kuvunjika. Kwa hiyo, mtazamo wa  Papa huko wazi sana kwa ukweli na utafutaji wa siku zijazo.

Papa alikutana na wajesuit wa Indonesia
04 September 2024, 10:16