Tafuta

Papa Francisko:tusiwe ndumila kuwili kwa matendo ya nje na ndani!

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 1 Septemba,Papa ametoa tafakari kuhusu Injili ya Siku ambapo ametualika tusipunguze uhusiano na Mungu kwa ishara za nje,ikiwa ndani tunawadharau maskini au tunafanya kazi ya kukosa uaminifu.Hakuna haja ya kujitolea kidogo kisha kusengenya bila huruma kwa kila kitu na kila mtu.Wakristo walioshikamana hufanya maombi thabiti kwa upendo na wengine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume ametoa tafakari yake kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican Dominika tarehe 1 Septemba 2024. Akiaka tafakari hiyo Papa amesema “Leo hii katika Injili ya Liturujia (7,1-8.14-15.21-23),Yesu anatuzungumzia juu ya utakaso na dhambi, mada ambayo ni pendwa kwa watu wa wakati wake ambao walikuwa wakihusisha kimsingi na utazamaji wa ibada na kanuni za mwenendo ili kuzuia kila aina ya mawasiliano na mambo au watu waliokuwa wanafikiria ni najisi na katika muktadha huo kufuta madoa. Baadhi ya waandishi na wafarisayo, wakandamizaji waliokuwa wameshikamana sana na sheria hizo, walimmshutumu Yesu kuruhusu wafuasi wake kuchukua chakula  bila kunawa mikono.

Na Yesu anachukua karipio la mafarisayo kwa wafuasi wake ili kuzungumza nasi(Mk 7,2) na Yeye anatumia fursa hiyo kuwaalika kutafakari juu ya maana ya “utakaso.” Kuhusu usafi, Yesu aliwambia haujaunganishwa na ibada za nje, lakini kwanza kabisa zinamwilishwa na tabia za ndani. Ili kuwa na utakaso, kwa hiyo haitajiki kunawa mikono mara nyingi, ikiwa baadaye utajimwilisha na hisia mbaya kama zile za uchoyo, wivu na kiburi, au mapendekezo mabaya kama vile udanganyifu, wivu, usaliti na kashfa(rej. Mk 7,21-22). Yesu anavutia umakini wa kuwa waangalifu na ibada ambazo hazifanyi kukua wema, badala yake zinaweza kupelekea kuacha na zaidi kuhalalisha, binafsi na wengine, chaguzi na tabia kinyume na upendo, ambazo zinajeruhi roho na kufunga moyo.

Uwanja wa Mtakatifu Petro ulijaa waamini na mahujaji kusali sala ya Malaika wa Bwana
Uwanja wa Mtakatifu Petro ulijaa waamini na mahujaji kusali sala ya Malaika wa Bwana

Papa Francisko amesema kuwa “Na kile ambacho ni muhimu hata kwetu ni kwamba huwezi kutoka katika Misa Takatifu na ukiwa tayari katika uwanja wa Kanisa tu unasimama na kuanza kusimanga vibaya na kukosa huduma kwa kila kitu na kwa wote. “Yale masengenyo ambayo uharibu moyo na roho. Na huwezi kufanya hivyo! Wewe inakwenda Misa na baadaye unafanya mambo mengine ni jambo baya sana!” Au kujiionesha mwema katika sala, lakini baadaye nyumbani unakuwa baridi na kuwa mbali na familia yako,au kuacha wazazi wazee ambao wanahitaji msaada na wa kuwasindikiza (Mk 7,10-13).

Hii ni ndumila kuwili ya maisha na huwezi kufanya. Hayo ndiyo walikuwa wakifanya mafarisayo. Usafi wa nje, bila tabia njema, tabia za huruma kwa wengine. Au huwezi kuwa wa ujuu juu unaonekana kuwa mwadilifu sana kwa kila mtu, labda kufanya hata ile ya kujitolea kidogo na ishara za kujitolea, lakini ndani mwako unakuza chuki kwa wengine, kudharau maskini na walio wa mwisho au kuwa na mwenendo usio mzuri wa kazi yako. Kwa kufanya hivyo unapunguza uhusiano na Mungu kwa ishara za kijuu juu na ndani zinabaki zisizopitia matendo ya kutakaswa na neema yake, kwa kuwa na shaka ya mawazo, ujumbe na mienendo isiyo na upendo.

Papa Francisko ametafakari Injili ya Dominika 1 Septemba 2024
Papa Francisko ametafakari Injili ya Dominika 1 Septemba 2024

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa “Hapa sisi hatukufanywa hivyo kwa ajili ya kitu kingine, sisi tumefanywa kwa ajili ya usafi wa maisha, huruma na kwa ajili ya upendo: ule ambao Mungu anatupatia, ikiwa tunaruhusu kuondoa ndani mwetu kivuli cha ubinafsi, majivuno na hukumu ili kujiunda na sura ya Mwanae Yesu(rej Rm 8,29) ambaye alitoa maisha kwa ajili yetu(Rej 1Gv 3,16). Baba Mtakatifu kwa kuhitimisha amesema: “Hebu tujiulize, basi: je, ninaishi imani yangu kwa njia iliyoshikamana, yaani, kile ninachofanya Kanisani, je, ninajaribu kukifanya nje kwa roho hiyo hiyo? Kwa hisia, maneno na matendo, je, ninaweka ukaribu na heshima kwa ndugu kile ninachosema katika sala? Hebu tufikirie juu yake. Na Maria, Mama aliye safi kabisa, atusaidie kufanya maisha yetu, kwa upendo kuhisiwa na kutekelezwa, ibada inayompendeza Mungu (rej Rum 12:1).”

Tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika 1 Septemba 2024
01 September 2024, 15:30