Mgogoro kati ya Palestina na Israeli Mgogoro kati ya Palestina na Israeli  (AFP or licensors)

Papa kuwe na amani katika Nchi Takatifu na Yerusalemu!

Papa,katika salamu zake baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,alirejea kuomba amani kwa ajili ya Mashariki ya Kati na Ukraine.Ombi lake ili mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yasitishwe na Yerusalem iwe mahali pa kukutana kati ya dini.Papa kizungumzia idadi ya watu wa Kiukraine wanaoteswa, alikumbusha kuwa:"Mungu anajali mateso yao."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe Mosi Septemba 2024 kati ya maombi mengine mawazo yake kwa mara nyingine tena amkumbuka nchi ya Ukraine na kuwa kuwageukia watu wanaoteseka katika Nchi Takatifu na mzozo wa Israel na Palestina, ambao umemwaga damu katika Mashariki ya Kati kwa takriban karibu mwaka mzima sasa.

Papa alisema: “Niko karibu na watu wa Kiukreni wanaoteswa, wanaopigwa sana na mashambulizi ya miundombinu ya nishati. Mbali na kusababisha vifo na majeruhi, wameacha zaidi ya watu milioni moja bila umeme na maji. Tukumbuke kwamba sauti ya wasio na hatia inasikika daima na Mungu, ambaye habaki kutojali mateso yao!” Papa aliongeza “Kwa mara nyingine tena ninageuza mawazo yangu kwa wasiwasi kwa mzozo wa Palestina na Israeli, ambao unahatarisha kuenea kwa miji mingine ya Palestina. Ninatoa wito wa kusitisha mazungumzo na kuacha mara moja kurusha risasi, kuwaachilia mateka, kusaidia idadi ya watu huko Gaza, ambapo magonjwa mengi pia yanaenea, pamoja na polio.” Hebu kuwa na amani Nchi Takatifu, kuwana amani katika Yerusalemu! Jiji Takatifu na kuwe mahali pa kukutania ambapo Wakristo, Wayahudi na Waislamu wanahisi kuheshimiwa na kukaribishwa, na hakuna anayehoji Hali Iliyopo katika Maeneo Matakatifu yao.”

Madhabahu ya Brazili

Papa Francisko vile vile amekumbuka tukio jingine kwamba “Pia ninasali kwa ajili ya waathirika wa ajali iliyotokea katika Madhabahu ya Mama Yetu Patakatifu wa Conceicão, katika jiji la Recife, nchini Brazili. Bwana mfufuka awafariji majeruhi na familia zao.”

Siku ya kazi ya uumbaji 

Katika siku ya kimataifa Papa Francisko amesema: “Leo tunaadhimisha Siku ya Dunia ya Kuombea Utunzaji wa Uumbaji. Ninatumaini kutoka kwa kila mtu, taasisi, vyama, familia na kila mtu, kujitolea madhubuti kwa ajili ya nyumba yetu ya pamoja. Kilio cha Dunia iliyojeruhiwa kinazidi kutisha na kinahitaji hatua madhubuti na za haraka.”

 

Ziara ya Kitume

Hatimaye Papa amekumbuka ziara yake anayoanza katika Bara la Asia na Oceania: Indonesia, Papua New Guinea, Timor ya Mashariki, Singapore: “Kesho nitaanza ziara ya kitume katika baadhi ya nchi za Asia. Tafadhali mniombe kwa ajili ya  matunda ya safari hii."

Bada ya Angelus
01 September 2024, 16:05