Papa kwa hija ya wanafamilia huko Pompei na Loreto:muwe vyombo vya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Muda wa sala ya kwaya, ambayo inahusisha wazazi, watoto na babu na bibi na wazee, kuwaunga mkono katika safari yenu kwa nguvu ya imani. Ndiyo maneno ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika Hijia ya 17 ya Kitaifa ya Familia kwa ajili ya Familia, iliyohamasishwa siku ya Jumamosi tarehe 14 Septemba 2024 hadi kufika madhabahu ya Maria wa Pompei na Loreto na Harakati ya Uhushaji wa Roho Mtakatifu (RNS) kwa ushirikiano na Wakuu wa Madhabahu 2 ya Kipapa, Ofisi za Baraza la Maaskofu Italia kwa ajili ya huduma ya kichungaji ya familia na Jukwaa la vyama vya familia nchini Italia. Ni hija inyaooongozwa na mada “Lolote atakalokuambia, fanyeni.”
Kuungana ili kukaribisha zawadi ya Roho Mtakatifu
Katika ujumbe uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatica ukielekezwa kwa Giuseppe Contaldo, Rais wa Harakati ya uhuishaji wa Roho(Rns,) Papa anakaribisha tukio hilo na kutoa salamu zake za dhati na ukaribu wa kiroho kwa washiriki wote. Katika “kukabidhi kwa mtazamo wa upendo ya Mama Bikira familia nyingi katika shida, wale walio katika maeneo ya vita au wanaokabiliwa na umaskini mkubwa,” Papa Francisko “anaungana na mahujaji kukaribisha zawadi ya Roho Mtakatifu ili familia za Kikristo nchini Italia, Ulaya na katika ulimwengu mzima wanaweza kuwa vyombo vya amani kwa kutoa ushuhuda wa uzuri wa maisha ya pamoja.”
Kard.Zuppi: Bwana abariki hatua zenu
Na kwa upande wake Kardinali Mateo Zuppi Rais wa Baraza la Maaskofu Italia CEI) alituma ujumbe wake aliuopatia kichwa: “Bwana abariki hatua zenu! Kardinali anabinisha kuwa "Inapendeza kujua kwamba, kwa mara nyingine tena, wamekubali mwaliko wa kuanza kumfuata Maria ili kukutana na Bwana Yesu, ambaye bado anazungumza na familia yao na ulimwengu leo hii. Safari ambayo ina ladha ya watu: watoto, vijana, watu wazima na wazee. Kila mtu akiwa njiani. Safari ya watu ambayo, kwa mara nyingine tena, inashuhudia jinsi ufuasi wa Bwana Yesu unavyomhusu kila mtu na sio tu baadhi au kategoria fulani. “Lolote atakalokuambia, fanyeni” ni neno la kiinjili linaloashiria mdundo wa hatua zenu."
Maandalizi ya Jubilei 2025
Kardinali Zuppi aidha alibanisha kwamba: “Tuko kwenye miinuko ya mwisho ya mwaka huu kwa maandalizi ya Jubilei na Papa ametualika kuweka maombi katikati ya maandalizi yetu. Na ni mwalimu gani bora kuliko Maria aliyepo ili kujifunza unyenyekevu na matumaini. “Lolote atakalokuambia, fanyeni.” Na Bwana anaiambia nini familia leo hii? Anatuambia tumtumaini, kama watumishi walivyofanya kwenye Arusi ya Kana. Katika siku hiyo ya karamu, Yesu aliwaomba watumishi wajaze mabarasi maji, kazi yenye kuchosha na isiyofaa. Kazi ambayo haikutambuliwa na wageni wa harusi hiyo. Kazi ambayo haikukasirisha mtu yeyote, kwa kuzingatia tu utii na uaminifu. Sisi pia tunaombwa kufanya kazi sawa: rahisi, unyenyekevu,na ujasiri. Tumeitwa kufanya kuwa sehemu yetu katika maisha ya kila siku, kwa njia yetu ndogo, kumruhusu Bwana kubadilisha juhudi zetu zote kuwa divai nzuri.
Wakati wetu wa vita na vurugu tuwe watangazaji na wajenzi wa amani
Kardinali Zuppi amesisitiza kuwa "katika wakati wetu, ambao umeashiriwa sana na vita na vurugu, tufanye kazi ili kuwa watangazaji na wajenzi wa amani, tukijaza uhusiano wetu na ile amani inayotokana na ugunduzi wa Kristo Mfufuka, aliye hai na aliyepo kati yetu. Kwa hivyo njoo! Kwa pamoja tunaweza kuweka katika ulimwengu furaha ya kuwa familia, kwa sababu, kama Papa Francisko anavyotukumbusha: “Mungu ameikabidhi familia mpango wa kuifanya dunia kuwa nyumbani, ili kila mtu aje kuhisi kila mwanadamu ni ndugu” (AL 183). Na hatimaye amewatakia Hija njema na safari ya furaha!