2024.09.19 Wawakilishi wa Kikundi cha Pasaka Pamoja 2025 -(Easter Together 2025) 2024.09.19 Wawakilishi wa Kikundi cha Pasaka Pamoja 2025 -(Easter Together 2025)  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa na kundi la Pasaka Pamoja 2025:Pasaka ni mali ya Kristo na vizuri tuombe neema ya kuwa wanafunzi wake zaidi

Maadhimisho ya Ufufuko wa Bwana kwa mwaka 2025 yatafanyika pamoja na Wakatoliki na Waorthodox wanaofuata kalenda ya Gregorian na Julian.Pia tutakumbuka miaka 1700 ya Baraza la Kiekumene la Nikea,kama ishara ya imani iliyotangazwa na mada ya tarehe ya Pasaka ilishughulikiwa.Sherehe ya pamoja isiwe tena ubaguzi bali iwe ya kawaida.Ni wito wa Papa kwa kundi la Mpango wa'Pasaka Pamoja 2025.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hotuba yake Baba Mtakatifu aliyowakabidhi Kikundi cha Mpango wa Pasaka Pamoja 2025 (Pasqua Together aliokutana nao Alhamisi tarehe 19 Septemba 2024, mjini Vatican, anawakaribisha kwa maneno ya Mtakatifu Paulo: “Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo” (Rm 1:7). Alimsalimu Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, na amemshukuru kwa maneno yake. Kundi hilo linawakilisha mashirika na jumuiya mbalimbali: kwanza kabisa madhehebu ya Kikristo waliyomo, kisha Mashirika ya Walei na Harakati, na hatimaye nyanja mbalimbali za utendaji zinazowaunganisha, kama vile siasa na maandalizi ya Milenia ya Pili ya Ukombozi inayokuja mwaka wa 2033 na mipango mingine kama hiyo.

Papa na wawakilishi wa Kundi la Pasaka Pamoja 2025
Papa na wawakilishi wa Kundi la Pasaka Pamoja 2025

Mpango wa Pasaka Pamoja unatekeleza mipango  ya pamoja katika nyanja hizi zote.  Papa anawapongeza na kuwahimiza waendelee. Kiukweli, kujitolea kwao katika maeneo haya kutasaidia kuepuka kuruhusu tukio muhimu la 2025 lipite bure. Mwaka ujao, ambao ni mwaka wa kawaida wa Jubilei kwa Kanisa Katoliki, sherehe ya Pasaka itaambatana na kalenda za Wakristo wote. Pamoja na ishara hii muhimu, pia tutaadhimisha kumbukumbu ya miaka 1700 ya maadhimisho ya Baraza la kwanza la Kiekumene la Nikea. Mbali na kutangaza Alama ya Imani, baraza hili pia lilishughulikia suala la tarehe ya Pasaka kwa sababu mapokeo tofauti yalikuwa yametokea wakati huo. Kwa zaidi ya tukio moja, “nimeombwa kutafuta suluhisho la suala hili, ili sherehe ya pamoja ya Siku ya Ufufuko isiwe tena ubaguzi, bali iwe ya kawaida.”  Kwa hiyo Papa anawatia moyo wale waliojitolea katika safari hii kuvumilia, na kufanya kila jitihada katika kutafuta mapatano ya pamoja, kuepuka jambo lolote ambalo badala yake linaweza kusababisha migawanyiko zaidi kati ya kaka na dada zetu.”

Zaidi ya yote, hata hivyo Papa amependa kushiriki na kila mtu wazo, ambalo huturudisha nyuma kwenye kiini cha suala: Pasaka haifanyiki kwa hiari yetu wenyewe au kwa kalenda moja au nyingine. Pasaka ilitokea kwa sababu Mungu “aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yh 3:16). Tusisahau ukuu wa Mungu, mtangulizi wake, baada ya kuchukua hatua ya kwanza. Hebu tusijifunge ndani ya mawazo yetu wenyewe, mipango, kalenda, au Pasaka yetu. Pasaka ni mali ya Kristo! Zaidi ya hayo, ni vizuri tuombe neema ya kuwa wanafunzi wake zaidi, tukimruhusu awe mtu wa kutuonesha njia tunayopaswa kufuata. Ni lazima tukubali kwa unyenyekevu mwaliko alioutoa siku moja kwa Petro kufuata nyayo zake, na sio kufikiri kama wanadamu wanavyofikiri, bali kama Mungu (rej. Mk 8:33).

Wawakilishi wa Mpango wa Pasaka Pamoja 2025
Wawakilishi wa Mpango wa Pasaka Pamoja 2025

Kwa hiyo Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa "na tujitahidi kutafakari, kushiriki na kupanga pamoja, tukimweka Yesu mbele yetu, tukiwa na shukrani kwa wito wake na shauku, katika umoja, kuwa mashahidi wake, ili ulimwengu upate kuamini (taz. Yh 17:21). Tunahitaji kutembea pamoja. Kufanya hivyo, itatusaidia ikiwa tutaanza kutoka Yerusalemu kama Mitume, ambao walitangaza ujumbe wa Ufufuko kwa ulimwengu wote kuanzia mji huo mtakatifu. “Kwa njia hiyo ​​pia tumgeukie Mfalme wa Amani ili tuombe kwamba atupatie amani yake. Wapendwa kaka na dada, Bwana awabariki na kukirimia kwa yale mnayofanya. Niwakushukuru kwa mkutano huu. Ninawaombea na tafadhali msisahau kuniombea.”

Papa na Kundi la Mpango wa Pasaka Pamoja 2025
19 September 2024, 11:19