Tafuta

2024.09.21 kikosi cha Ulinzi wa Fedha na Mapato katika hafla ya kuadhimisha miaka 250 ya kuanzishwa kwa mfuko,nchini Italia. 2024.09.21 kikosi cha Ulinzi wa Fedha na Mapato katika hafla ya kuadhimisha miaka 250 ya kuanzishwa kwa mfuko,nchini Italia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Mamlaka ya Mapato Italia:Tunahitaji mshikamano kama njia ya amani&tumaini lijalo!

Kwa hakika,utajiri wa taifa haupo katika Pato la Taifa tu,upo katika urithi wake wa asili,kisanii,kiutamaduni,kidini na katika tabasamu za wakazi wake na watoto wake.Ni katika hotuba ya Papa kwa Waziri wa Uchumi na Fedha na wahusika wa Mamlaka ya Mapato nchini Italia aliokutana nao Septemba 21 mjini Vatican."Ufisadi ni kashfa ya kukosekana kwa usawa katika jamii."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 21 Septemba 2024, amekutana na Mamlaka ya Mapato ya Taifa na Wanajeshi 300 mjini Vatican wa Mamlaka hiyo katika fursa ya maadhimisho ya miaka 250 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa 'Moto wa Njano' na kuwahimiza kuwa karibu na watu, kwa sababu haki ni muhimu lakini ni upendo pekee ambao unaweza kuponesha. Wao wanapata uzoefu wa kukaribishwa na kuokolewa kwa wahamiaji walio hatarini katika Bahari ya Mediterania, katika uingiliaji kati wa ujasiri wa majanga ya asili, au katika vita dhidi ya 'wafanyabiashara wa vifo' ambao hudhibiti biashara ya dawa za kulevya na mengine mengi. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu akianza hotuba yake amemsalimia Waziri wa Uchumi na Fedha, Jenerali wa Kikosi na maafisa wote na kumshukuru Askofu Mkuu wa Kijeshi na Mapadre wa vikanisa vya kijeshi.

“Katika mila na tamaduni kuna siku zijazo," ndiyo kauli mbiu ya maadhimisho yao ya miaka 250, ambapo Papa amesema inahusu mizizi iliyosababisha msingi wa Ulinzi wa  Mapato na kuipatia mwelekeo wa ukuaji. Ilizaliwa kama chombo maalum cha uchunguzi wa kifedha na huduma ya ulinzi wa mpaka, ilichukua majukumu ya polisi wa ushuru na kiuchumi na kifedha, polisi wa baharini, na tume muhimu katika uwanja wa uokoaji, baharini na milimani. Kikumbusho cha kihistoria cha ahadi hii ni msaada unaotolewa kwa wakimbizi wa Kiyahudi na wale wanaoteswa wakati wa migogoro miwili mikubwa ya dunia. Sehemu kubwa ya uingiliaji kati, kwa hivyo, ambayo inakusudia kujibu shida na ukweli wa uwepo na hatua ya wakati, na wakati huo huo kuwasilisha njia mbadala ya kiutamaduni kwa maovu kadhaa ambayo yanahatarisha kuchafua jamii.

Papa amekutana na Mamlaka ya Ulinzi wa Mapato na Fedha Italia
Papa amekutana na Mamlaka ya Ulinzi wa Mapato na Fedha Italia

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema Msimamizi wao ni Mtakatifu Mathayo ambaye ilikuwa ni sikukuu yake tarehe 21 Septemba ya  mtume na mwinjili. Yeye, kwa hakika, alikuwa ‘mtoza ushuru’, kwa kazi iliyodharauliwa maradufu katika wakati wa Yesu, kwa sababu ilikuwa chini ya mamlaka ya kifalme na kwa sababu ilikuwa ya ufisadi. Papa aliongeza “Ninapenda kwenda kwenye Kanisa la Ufaransa (la Mtakatifu Aloizi) kuona picha ya  Caravaggio, ya “Uongofu wa Mathayo”, ambayo inaashiria kwa kina sana. Mathayo aliwakilisha mawazo ya utumishi na yasiyofaa, yaliyotolewa tu kwa “mungu wa pesa.” Hata leo hii, mantiki kama hiyo ina athari kwa maisha ya kijamii na kusababisha kukosekana kwa usawa na kutengwa: kuanzia katika upotezaji wa chakula, ambayo ni  kashfa, ni kashfa kutengwa kwa raia  na kufaidika na baadhi ya haki zao,” Papa alisisitiza.

Hata Serikali inaweza kuishia kuwa mhanga wa mfumo huu; hata zile za Mataifa ambayo, licha ya kuwa na rasilimali nyingi, bado yametengwa katika kiwango cha fedha au soko la kimataifa. “Je inaelezwaje njaa duniani leo hii, wakati kuna ubadhirifu mwingi katika jamii zilizoendelea? Hii ni mbaya. Na jambo lingine: ikiwa wangeacha kutengeneza silaha kwa mwaka mzima, njaa ya ulimwengu ingeisha kwa sababu wanaona  silaha ni bora kuliko kutatua njaa ...”. Katika mtazamo huo, wao wameitwa kuchangia haki ya mahusiano ya kiuchumi, kuthibitisha utiifu wa sheria zinazosimamia shughuli za watu binafsi na makampuni,” Papa amewahimiza. Kwa hiyo, kufuatilia wajibu wa kila raia kuchangia kulingana na vigezo vya haki kwa mahitaji ya Serikali, bila kupendelea wenye nguvu zaidi, na kupambana na matumizi yasiyofaa ya mtandao na mitandao ya kijamii.

Papa amekutana Mamlaka ya Ulinzi wa Mapato na Fedha Italia
Papa amekutana Mamlaka ya Ulinzi wa Mapato na Fedha Italia

Iwe kuhusu ukusanyaji wa kodi au katika vita dhidi ya kazi ambayo haijatangazwa na inayolipwa kidogo, hii ni kashfa nyingine - au kwa vyovyote vile inadhuru utu wa binadamu, na kwa hiyo hatua yao ni ya muhimu sana. Na yote haya ni njia yao madhubuti na ya kila siku ya kuhudumia manufaa ya wote, kuwa karibu na wananchi, kupambana na ufisadi na kukuza uhalali. Ufisadi huo unaotokea chini ya meza. Neno “rushwa” – “cor-rotto” - "hukumbusha moyo uliovunjika, uliochafuliwa na kitu, umeharibiwa […] Kwa hiyo ufisadi unafichua tabia inayopingana na jamii yenye nguvu sana kiasi cha kufuta uhalali wa mahusiano na mihimili ambayo kwayo jamii imeanzishwa. Kwa hivyo jibu, mbadala sio tu katika sheria, lakini katika “ubinadamu mpya”. Yaani kuanzisha upya ubinadamu,” Papa amekazia kusema.

Mtazamo wa Yesu, uliowekwa kwa Mathayo kijana, unasema kwamba utu na maisha ya mwanadamu ndio moyo wa maisha ya watu. Unaweza pia kuchangia kuongezeka kwa ubinadamu huu mpya kupitia kazi wanayotoa katika huduma ya vijana wanaomba kujiunga na Polisi wa Mapato ya  Fedha na kuhudhuria shule zao. Labda mwanzoni wanatafuta kazi tu, lakini kisha wanapata mafunzo maalum, ambayo, pamoja na kuwapa ujuzi muhimu na uzoefu, pia inakuwa elimu kwa maisha na manufaa ya wote. Mathayo, kwa maana fulani, alihama kutoka katika mantiki ya faida hadi ile ya usawa. Lakini, katika shule ya Yesu, pia alikwenda zaidi ya usawa na haki na akaja kujua ile ya kutoa bure, zawadi binafsi inayozalisha mshikamano, kushiriki na kujumuika." “Uhuru sio tu mwelekeo wa kifedha, lakini mwelekeo wa kibinadamu. Na kuweni watu katika huduma ya wengine, bila malipo, bila kutafuta faida ya mtu mwenyewe. Kwa sababu, ikiwa haki ni muhimu, haitoshi kujaza mapengo hayo ambayo ni ukarimu tu, bali hisani na upendo vinaweza kuponya.

Picha ya Pamoja ya Papa na Kikosi cha Ulinzi wa Mamlaka ya Mapato na Fdha nchini  Italia
Picha ya Pamoja ya Papa na Kikosi cha Ulinzi wa Mamlaka ya Mapato na Fdha nchini Italia

Papa Francisko amesema kwamba wao wanapata uzoefu, kwa mfano, wanapoandaa mapokezi na uokoaji wa wahamiaji katika hatari kwenye bahari ya  Mediterania. Kwa njia hiyo amewashukuru sana kwa hilo. kwa uingiliaji wa ujasiri katika majanga ya asili, nchini Italia na mahali pengine. “Lakini hebu tufikirie juu ya mapambano dhidi ya janga la biashara ya madawa ya kulevya, wafanyabiashara wa kifo.” Kwa hiyo huduma yao haina mwisho na ulinzi wa waathirika, lakini inajumuisha jaribio la kusaidia kuzaliwa upya kwa wale wanaofanya makosa: kiukweli, kwa kutenda kwa heshima na uadilifu wa maadili wanaweza kugusa dhamiri, kuonesha uwezekano wa maisha tofauti.

Pia kwa njia hiyo Papa amesema “tunaweza na lazima tujenge njia mbadala ya utandawazi wa kutojali, ambao unaharibu kwa vurugu na vita, lakini pia unapuuza utunzaji wa jamii na mazingira.” Kwa hakika, utajiri wa taifa haupo tu katika Pato la Taifa, upo katika urithi wake wa asili, wa kisanii, wa kiutamaduni, wa kidini, na katika tabasamu za wakazi wake, za watoto wake. " Papa ametoa mfano kwamba "Wakati mmoja, mkuu wa nchi aliniambia: “Nina kipimo maalum kile cha  tabasamu la watoto na wazee.” Wakati wote wanatabasamu, mambo si mabaya sana katika jamii." Papa ameongeza: "Inapendeza.” Papa amesisitiza. Na hii inakuza ubunifu, uwazi kwa ulimwengu. Ninyi wenyewe ni raia ambao mnalinda ‘utajiri’ huu wa Italia, lakini mko tayari kwenda nje kwa misheni ya kimataifa. Tunahitaji mshikamano huu kwa wengine kama njia ya amani na tumaini la maisha bora ya baadaye!

Wakati wa kusalimiana na Papa washiriki hawa wa Mamlaka ya Mapato na Fedha Italia
Wakati wa kusalimiana na Papa washiriki hawa wa Mamlaka ya Mapato na Fedha Italia

Baba Mtakatifu Francisko amewapongeza, kwa sababu wanashirikiana katika kuchochea imani na matumaini ya watu.“Hawa watu ambao ni sisi sote. Na kuongeza uaminifu, tumaini na tabasamu. “Nitarudi kwa hilo Papa ameongeza. "Kipimajoto chake: je! watoto hutabasamu? Je, wazee hutabasamu? Msisahau.” Papa aidha amesema: "Na katika maadhimisho haya muhimu yanaendana vyema na kaulimbiu ya Jubilei ambayo Kanisa linajiandaa kuiadhimisha, ambayo ni “Mahujaji wa matumaini.” kwa kuhitimisha Papa amewabariki kwa moyo wote na amebariki kazi na familia zao. Tafadhali wasipoteze hisia zao za ucheshi, kwani  hiyo ni afya! Na namewaomba wamuombee tafadhali.

Papa/Mamlaka ya Mapato Italia
21 September 2024, 12:21