Tafuta

2024.09.19 Papa akutana na Washiriki wa Mikutano Mikuu:Ndugu na masisita wa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria na wWtawa wa Mungu Mwokozi (SDS) 2024.09.19 Papa akutana na Washiriki wa Mikutano Mikuu:Ndugu na masisita wa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria na wWtawa wa Mungu Mwokozi (SDS)  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria & SDS:Chukua hatua madhubuti kumfuata Kristo

Ili kuwa kama mitume,mnahitaji kuwa na usikivu wa sauti ya Mungu,kufanya tafakari,uwezo wa kuishi na kutangaza upendo wa Mungu aliyefanyika mwili kwa namna ya pekee katika huduma kwa wahitaji zaidi hata sala ya ekaristi na fidia.Ni katika hotuba ya Papa alipokutana na mashirika ya Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria na Shirika la Mungu Mwokozi(SDS)mjini Vatican Septemba 19.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 19 Septemba 2024, amekutana na mashirika ya Ndugu na Masisitia wa Mioyo Mitakatiu ya Yesu na Maria na Shirika la Maisita wa Mungu Mwokozi(SDS), wakiwa katika fursa ya Mikutano yao Mikuu ya Mashirika yao. Papa akianza hotuba yake amewakaribisha watawa hao wapendwa na kuwakumbusha kuwa "maadhimisho ya Mkutano Mkuu, haijibu mantiki ya kibinadamu au hitaji la kitaasisi, lakini kwa mahitaji ya sequela Christi yaani  kumfuasa Kristo. Hii inahitaji daima umakini wa kusikiliza kile ambacho Roho Mtakatifu anapendekeza ili kuishi kwa uaminifu utambulisho na utume wa kweli wa mashirika yenu.”

Papa akutana na washiriki wa mikutano mikuu
Papa akutana na washiriki wa mikutano mikuu

Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha kuwa kama mitume, wao wanahitaji kuwa na usikivu wa sauti ya Mungu, kufanya tafakari ya kina  na kuwa na uwezo wa kuishi na kutangaza upendo wa Mungu aliyefanyika mwili ndani mwao kwa namna ya pekee kwa njia ya huduma kuelekeza kwa wenye shida zaidi na hata kwa njia ya sala ya Ekaristi na fidia. Papa aidha amesema kwamba kwa kufuata Yesu tu kwa uamanifu na upole, nyumba zao, kama vile kuenea kwa urithi wa kiroho na kihistoria wa Mashirika, unaweza kufurahia upyaishwaji wa uchanuzi ambao utafanya kuangaza karama zao katika wakati wa sasa wa historia ya ubinadamu.

Papa akutana na watawa wakiwa katika Mikutano Mikuu ya shirika lao
Papa akutana na watawa wakiwa katika Mikutano Mikuu ya shirika lao

Papa amesisitiza: "Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria, iweze kuwasukuma kupata daima mtindo mpya wa ushuhuda mbele ya ndugu na wahudumu ambao wanafanya kazi ya Mungu ambayo inatekelezwa katika Kanisa." Baba Mtakatifu  kwa njia hiyo amewaalika "kuchukua hatua madhubuti katika kumfuata Kristo, lakini ambayo haijumuishi kujifunza mafundisho tu, bali pia kufuata mtindo wa maisha. Na hatimaye anawahakikishia ukaribu na maombi yake ili wapate kujipyaisha kwa utambuzi unaovuviwa na kuungwa mkono na tunu za Injili na ili hamu ya kuishi kwa kuungana na Yesu na kubaki waaminifu kwa karama iliyoanzishwa iongezeke mioyoni mwao.

Akiwageukia Shirika la Mungu Mwokozi,(SDS), Papa Francisko alisema: "Pia ninatoa salamu zangu kwenu, Masista wa Mungu Mwokozi mnaoadhimisha Mkutano Mkuu kwa mada yenye changamoto: “Kuenenda pamoja, tukiamsha upya kipaji cha Roho kati yetu kutangaza Injili na kuwatia moyo watu wote”. Papa aliongeza kusema: “Mambo manne: kutembea pamoja - si kupinga, kuwasha upya karama ya Roho kati yetu, kutangaza Injili na kuwawasha watu wote.” Hii inarejea msingi wa karama yenu: sala ya kutoka moyoni ambayo Yesu alielekeza kwa Baba wakati wa Karamu ya Mwisho, kwa ajili ya wokovu wa watu wote: “Uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo” (Yh 17:3). Na ni pale pale, katika Karamu Kuu ambapo, ninawaalika msimame kwa muda mrefu katika maombi, hasa katika siku hizi Mkutano Mkuu,” Papa alikazia kusema.

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mikutano Mkuu ya Shirika
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mikutano Mkuu ya Shirika

Kiukweli ni pale ambapo moto wa Roho unalishwa,na kutoka hapo tunaanza tena kuwaka katika upendo wake ulimwengu mzima, tukitoa huduma kwa wahitaji na kurejesha tumaini kwa waliokata tamaa (taz. Spes non confundit, 3). Huu ndio urithi ambao Mwenyeheri Francesco Maria wa Msalaba na Mwenyeheri Maria wa Malaika waliwaachia, ambao walitaka ninyi kama shirika la kimisionari la ulimwengu wote.” Maria, “nyota ya kaskazini” ya utume, anatufundisha jambo hili, ambaye katika Injili anazungumza kidogo, lakini anasikiliza sana na kuyaweka moyoni mwake. Hii ni mitazamo halali kwetu pia: kuzungumza kidogo - kujadili, kujifungua, lakini kutopotea kwenye mazungumzo yasiyo na maana kwani gumzo na ugonjwa mbaya!, Papa amesisitiza.

Sikilizeni sana, ukimya na kuwa waangalifu kwa wengine

Ushauri wa Papa ni kwamba: “Sikilizeni sana, katika sala, kwa ukimya, kuwa waangalifu kwa wengine. Wakati mwingine hatujui jinsi ya kusikiliza: mwingine anaongea na nusu ya mazungumzo tunajibu. Hapana, tusikiliza kila kitu, hadi mwisho. Msikilize Bwana pia! Sikilizeni na weka mioyoni mwenu, kuwa mitume wa matumaini, katika ulimwengu unaohitaji sana leo. Na katika suala hili ningependa kuhitimisha kwa kukumbuka tabia ya Mama Maria: hajionyeshi kamwe , yeye anavutia  kila wakati kwa  Yesu (taz. Katekesi, 4 Januari 2023). Fanyeni chochote atakachowaambia:” huyu ndiye Mama, alionesha Yesu, siku zote, kamwe hajielekezi yeye mwenyewe kwamba: “Nitazame, mimi ni safi ...” Mama yetu huwa hasemi hivyo. Daima huelekeza kwa Yesu.” Ni lazima tujifunze hilo: kuwaonesha wengine Yesu, sio sisi wenyewe, kwa sababu kwa kila mtu, leo hii na siku zote, tumaini letu liko kwa Bwana, liko kwake (taz Eb 10:23). Kwa kuhitimisha Papa ameshukuru kwa ziara yao na anaomba nuru na nguvu za Roho Mtakatifu kwa kazi yao katika siku hizi za Mkutano Mkuu na kwa ajili ya safari ya baadaye ya jumuiya zenu. Amewabariki kubariki kutoka ndani ya moyo wake na ameomba wamuombee lakini kuomba si dhidi yake.

19 September 2024, 10:38