Papa kwa waandishi wa habari:ni ziara yangu ndefu zaidi asante kunisindikiza
Salvatore Cernuzio – akiwa kwenye ndege kutoka Roma-Jakarta
Akishangiliwa kwa makofi, Papa Francisko, tarehe 2 Septemba 2024 muda mfupi baada ya kuruka kwa Ndege ya Italia iliyokuwa ikimpeleka Indonesia kwa Ziara yake ya 45 ya Kitume, alitaka kutekeleza mzunguko wake wa kawaida ya salamu kati ya waandishi wa habari karibu 80 kutoka vyombo vya habari vya duniani kote wanaoandamana naye kwenye ndege. Miongoni mwao pia kuna baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi ambazo Papa atatembelea katika safari ndefu ya Septemba 2-13 ambao ni pamoja na Indonesia, Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore.
Papa amesalimiana na waandishi mmoja mmoja
Baada ya kusalimiana na wafanyakazi na wajumbe wa msafara, Papa alielekea sehemu ya mwisho ya ndege na kuchukua kipaza sauti. “Asante kuja nami katika safari hii. Asante kwa usindikizaji wenu, nadhani ni safari ndefu zaidi niliyowahi kufanya.” Haya nidyo yalikuwa ni maneno yake mbele ya waandishi wa habari na wapiga picha ambao wakati huo Papa Francisko akiwa anatembea alikwenda kuwasalimia mmoja baada ya mwingine kwenye viti vyao, walimshukuru yeye binafsi na kumpatia barua na zawadi zao walizoziandaa. Miongoni mwa zawadi hizo, zawadi iliyoletwa kutoka China na mwandishi wa habari Stefania Falasca ambaye alitoa nakala ya mnara wa Xian ulioanzia mwaka wa 635, kichwa cha kale cha kutangazwa kwa Injili katika nchi kubwa ya Asia na mmisionari. Aluoben jina lake, kama tunavyosoma katika maandishi, lilikuja kutoka Uajemi ili kueneza habari njema katika ardhi ya China. “Kutoka Qin”, kifungu kingine cha maandishi kwenye jiwe hilo kinasomeka: usemi wa Kichina unaoonesha jumuiya ya Kanisa la Kisiria ambalo liliweka makazi ya kudumu nchini China katika karne hiyo. Papa alichukua zawadi na kuishikilia kwa karibu, ishara ya upendo huo kwa China ambayo imekuwa ikithibitishwa tena.
Ishara za ukaribu wa Papa na zawadi
Ishara za hisia kutoka kwa Papa Francisko pia kwa zawadi nyingine mbili kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu mkasa wa wahamiaji. Moja ilitolewa na Clément Melki, mwandishi wa shirika la Ufaransa la AFP, alitumwa kwa siku kumi na tano kufuata kazi ya NGO ya Mediterranea Saving Humans kwenye meli ya Mar Jonio. Alimpatia Papa tochi, moja ya zile ambazo wakimbizi wengi kwenye bahari ya wazi hutumia kutafuta njia ya kurudi nyumbani au kuzuiliwa wakati wa ajali ya meli. “Hii ni karibu na moyo wangu", alisema Papa Francisko, ambaye amekuwa makini na mchezo wa janga la uhamiaji.
Mwandishi wa habari wa kituo cha utangazaji cha Radio Cope cha Hispania, Eva Fernandez, anayejulikana kwa zawadi zake za asili kila wakati kwa Papa wakati wa safari za ndege, alikua mjumbe wa familia ya Mateo, mvulana wa miaka 11 kutoka kijiji kidogo karibu na Toledo, Mocejón. Mateo aliuawa Agosti 18 iliyopita wakati wa mechi ya soka na marafiki zake. Muuaji alikuwa kijana kutoka mji mmoja na matatizo ya akili. Hata hivyo, historia hiyo ilizua mtafaruku mkubwa nchini humo, baada ya baadhi ya wawakilishi wa kisiasa kuwashutumu baadhi ya wahamiaji waliokaribishwa katika hoteli iliyo karibu na Mocejón kwa mauaji hayo baada ya saa chache. Familia ya mwathiriwa daima imekuwa ikikataa toleo hili lakini hii imeshindwa kukomesha utata kuhusu sera za upokeaji. Eva Fernandez alimpatia Papa, sare nyekundu ya mpira wa miguu na nambari 11. Papa Francisko alisikiliza historia hiyo, akabariki shati na kuchukua, akaiweka kifuani mwake, barua ambayo mama Mateo alimtumia. Kutoka hapo, makofi na shukrani nyingine kwa waandishi wa habari ambao watafuatana katika hatua za msingi za hija hii ndefu kati ya Asia na Oceania kwa takriban kilomita elfu 33.