Tafuta

Papa kwa watoto huko Papua Guinea:Mwanga wa upendo uendelee kuwaka

Papa Francisko alikutana na watoto wa mitaani na watoto walemavu nchini Papua New Guinea na kuwakumbusha kwamba kila mtu ni tofauti kwa sababu Mungu ndiye aliyewaumba hivyo.Katika Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Caritas huko Port Moresby alisalimiana na watoto 800 wanaohudumiwa na Huduma za Mitaani na Huduma za Callan.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 7 Septemba 2024, mara baada ya Mkutano na Mamlaka, Baba Mtakatifu Francisko ametembelea vituo viwili vya Huduma ya Mtaani, inayoendeshwa na Masista wa Shirika la Moyo wa Yesu, ambayo inawajali watoto maskini wenye umri wa miaka 7 hadi 14, ikiwapa mahitaji na elimu muhimu. Na Callan Services ndio mtoaji mkubwa zaidi wa huduma kwa watoto na watu wazima wenye ulemavu nchini Papua New Guinea. Inatumika kama mtetezi mkuu wa haki za ulemavu na uwakilishi, ikizingatia elimu-jumuishi na mafunzo kwa watu wote wenye ulemavu nchini.

Watoto wa Papua
Watoto wa Papua

Katika hotuba yake bila kusoma Baba Mtakatifu Francisko kwanza amewapongeza “wale wote  ambao walioimba na kucheza – kwamba wanafanya vizuri! Baadaye amewasalimia wote na kumshukuru kwa maneno aliyoambiwa na Mkuu wa Jumuiya, na mkurugenzi, pia wote waliohudhuria, watawa na walei  hasa watoto, ambao ni wa ajabu! “Nimefurahiya sana kukutana nanyi na kushiriki wakati huu wa sherehe nanyi. Nawashukuru pia wenzenu, walioniuliza maswali mawili yenye changamoto.

Papa amekutana na watoto
Papa amekutana na watoto

Kuhusiana na maswali hayo hawa walikuwa ni watoto wawili waliuliza maswali: Wa kwanza kutoka Callan Services, akizungumza kwa lugha ya ishara, aliuliza Papa "kwa nini siwezi kama wengine?" Wa pili, kutoka katika Huduma ya Mtaa, aliuliza "Tunawezaje kujifanyaje mema ili kuufanya ulimwengu wetu kuwa mahali pazuri?"

Papa amekutana na watoto na walemavu
Papa amekutana na watoto na walemavu

Kwa njia hiyo Papa alisema: Mmoja wao aliniuliza: ‘Kwa nini mimi si kama wengine?’ na hivyo kwa kujibu alisema kuwa: “Jibu moja tu kwa swali hilo linalonijia ni : “Kwa sababu hakuna hata mmoja wetu aliye kama wengine: kwa sababu sisi sote ni wa kipekee mbele ya Mungu! Kwa hivyo, sio tu kwamba ninathibitisha kuwa “kuna tumaini kwa kila mtu kama ilivyosemwa,  lakini pia ninaongeza kwamba kila mmoja wetu, katika ulimwengu, ana jukumu na utume ambao hakuna mtu mwingine anayeweza kuutimiza na kwamba hii, hata ikiwa inahusisha magumu, wakati huo huo huleta furaha kubwa, katika tofauti na  njia kwa kila mtu. Amani na furaha ni kwa kila mtu.”

Mkutano wa watoto Papua New Guinea
Mkutano wa watoto Papua New Guinea

Papa aidha ameongeza kusema: “Na kwa kujaribu kujifunza - shuleni pia - kila kitu tunachoweza, kukifanya kwa njia bora zaidi, kwa kusoma na kuweka juhudi zetu zote katika kila fursa tunayopewa kuikuza, kuboresha karama na ujuzi wetu. Je mmewahi kuona jinsi gani paka hujitayarisha wakati anapaswa kuchukua hatua kubwa? Kwanza, yeye huzingatia na kuelekeza nguvu zake zote na misuli katika mwelekeo sahihi. Labda anafanya hivyo kwa muda mfupi na hata hatuoni, lakini anafanya hivyo. Na ni vivyo hivyo kwetu sisi: lazima tuelekeze nguvu zetu zote kwenye lengo, ambalo ni upendo kwa Yesu na ndani yake kwa ndugu wote tunaokutana nao njiani, na kisha kwa msukumo kujaza kila kitu na kila mtu kwa upendo wetu!

Fuara ya kukutana na Watoto huko Papua New Guinea
Fuara ya kukutana na Watoto huko Papua New Guinea

Papa Francisko akifafanua swali hilo amekazia kusema kuwa "Kwa maana hiyo, hakuna hata mmoja wetu ambaye ni ‘mzigo’ - kama ulivyosema -sisi sote ni zawadi nzuri kutoka kwa Mungu, hazina kwa kila mmoja wetu! Papa Francisko kwa njia hiyo ametoa Asante, watoto, asante sana, kwa mkutano huu, na asante wote wanaofanya kazi pamoja, hapa, kwa upendo. Ameaomba “ watunze mwanga huu kuwaka kila wakati, ambao ni ishara ya tumaini, na sio kwao tu, bali kwa wale wote unaokutana nao, na pia kwa ulimwengu wetu, wakati mwingine ubinafsi na kujishughulisha na mambo ambayo hayajalishi. Watunze "mwanga wa upendo kuwaka! Na tafadhali, wamuombee yeye pia!”

Papa na watoto
Papa na watoto
Papa na watoto huko Papua New Guinea
07 September 2024, 10:35