Tafuta

2024.09.04 Papa amekutana na Maaskofu nchini Indonesia 2024.09.04 Papa amekutana na Maaskofu nchini Indonesia  (Vatican Media)

Papa na Maaskofu:Imani,udugu na huruma,Kanisa linapelekwa mbele na Makatekista

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa amekutana na maaskofu,mapadre, mashemasi,wanaume na wanawake waliowekwa wakfu amesisitiza mambo matatu yaliyomo yaliyomo kwenye kauli ya ziara ya kipapa kuhusu imani udugu na huruma.Na imani hupishwa nyumbani!

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kuanza hotuba yake akiwa katika Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa, Jumatano tarehe 4 Septemba 2024 amesema “Nikiwa na nanyi mbele yangu, ningependa kuwaambia kitu, simameni hapa... Kanisa - lazima tufikiri hivi - Kanisa linapelekwa mbele na makatekista. Makatekista ni wale wanaosongeha mbele, wanaosonga mbele, halafu wanakuja watawa, mara baada ya makatekista wakuja mapadre, askofu; lakini makatekista wako mbele, na ndiyo nguvu ya Kanisa. Wakati fulani, katika moja ya safari hizo za Afrika, Rais wa Jamhuri moja aliniambia kwamba alikuwa amebatizwa na baba yake katekista. Imani hupitishwa nyumbani. Imani hupitishwa kwa kilugha. Na makatekista, pamoja na mama na bibi, wanaendeleza imani hiyo. Ninawashukuru sana makatekista wote: ni wazuri, watu walei, kuna watoto, lakini sisi sote ni ndugu. Sio muhimu tena Papa, kardinali, askofu ... (sisi ni) ndugu, kila mmoja ana kazi yake ya kusaidia watu wa Mungu kukua.”

Mkutano wa Papa na Maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume huko Indonesia

Baba Mtakatifu Baadaye aliendelea na salamu zake kwanaza akikutana na Maaskofu, mapadre, mashemsi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na maketekista waliokuwapo. Papa alimshukuru Rais wa Baraza la Maaskofu Indonesia, Askofu Antonius Subianto Bunjamin, kwa meneno yake, hata kaka na dada walioshirikisha shuhuda zao. Kama ilivyokumbushwa Kauli mbiu iliyochaguliwa ya Ziara ya Kitume, “Imani, Udugu na huruma,” Papa Francisko amefikiria kuwa ziwe fadhila tatu ambazo zinajieleza vizuri katika mchakato wao wa Kanisa, na kuwa tabia yao kama watu, kikabila na kiutamaduni na kuishi kwa amani kama ushuhuda, misingi wa tamaduni ya Pancasila.

Kwa njia hiyo Papa amependa kutumia maneno hayo matatu katika tafakari yake. Kwanza kabisa imani, kwamba Indonesia ni Nchi kubwa, yenye utajiri mkubwa sana wa mali ya katika kiwango cha mimea, wanyama, rasilimali za nishati na malighafi. Utajiri mkubwa hivyo ambao unaweza hata hivyo kwa haraka kubadilika, kuwa wa kijujuu juu, kwa sababu za kiburi na majivuno, lakini ikiwa utafikiri kwa  kiakili na katika moyo uliowazi, unaweza kuwa kinyume chake cha kukukumbuka Mungu, kwa uwezo wake katika sayari na katika maisha, kama tundishwavyo na Maandiko matakatifu (Mw 1; Sir 42,15-43,33). Papa alisema, “ni Bwana anayetoa hayo yote. Hakika hata semtiminta moja ya ajabu katika eneo la Indonesia, na hata maisha mafupi ya kila mmoja wa wakazi wake ambaye siyo zawadi yake, ishara ya upendo wake wa bure na unaotoka kwa Bwana. Na kwa kutazama hayo yote kwa unyenyekevu wa macho ya kitoto unatusaidia kuamini, kujijua kuwa sisi watoto na wa kupendwa (Zab 8) na kukuza hisia za shukrani na uwajibikaji.

Papa amekutana na maaskofu, mapadre na waliowekwa wakfu
Papa amekutana na maaskofu, mapadre na waliowekwa wakfu

Baba Mtakatifu Francisko akidadavua neno la pili la kauli mbiu ni ‘udugu’ alisema alisema, kuhusiana hilo Agnes alitaja juu ya  uhusiano na uumbaji na ndugu hasa walio na mahitaji zaidi, ya kuishi mtindo mmoja kibinafsi, na kijumuiya wenye alama ya heshima, ustaarabu na ubinadamu kwa kwa moyo wa kiasi na upendo wa Kifransiskani. Papa ameongeza Mshairi mmoja wa karne ya 19 alitumia kielelezo kizuri sana kwa kuelezea tabia hiyo kwamba “kuwa ndugu kunamaanisha kupendana kwa kutambuana “tofauti kama matone mawili ya maji.” Na hivyo ndivyo ilivyo. Hakuna matone mawili ya maji yanayofanana, wala ndugu wawili, hata mapacha, hawafanani kabisa. Kuishi udugu, basi, kunamaanisha kukaribishana, tukijitambua kuwa sawa katika utofauti.”

Kwaya iliyoimba katika Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa
Kwaya iliyoimba katika Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa

Hata hiyo ni thamani pendwa ya utamaduni wa Kanisa la Indonesia ambayo inajionesha katika ufunguzi ambao unahusiana na hali halisi zinazojumuisha na kulizunguka kwa ngazi ya kiutamaduni, kikabila, kijamii na kidini kwa kuthamanisha uhusiano na wote na kutoa kwa ukarimu kwa kila mantiki. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa “Hii ni muhimu kwa sababu kutangaza Injili hakuna maana ya kupinga imani binafsi na wala ya wengine, bali kwa kutoa na kushirikishana furaha ya kukutana na Kristo (Taz. 1 Pt 3,15-17), daima kwa heshima kubwa na upendo kidugu kwa kila mtu. Huo ndio mwaliko wa Baba Mtakatifu wa kukaa hivi wawazi na marafiki na wote wakipeshikana, mkono kwa mkono kama alivyosema Padre Maxi, nabii wa umoja katika ulimwengu ambao utafikiri unaendelea kukua daima  na tabia za kugawanyika , kulazimisha na kuchocheana (Evangelii gaudium, 67).

Mkutano wa Papa na maaskofu, mapadre, watawa.waseminari na makatekista
Mkutano wa Papa na maaskofu, mapadre, watawa.waseminari na makatekista

Ni muhimu kujaribu kufikia kila mtu, kama Sr. Rina alivyotukumbusha, tukiwa na matumaini ya kuweza kutafsiri sio tu maandiko ya Neno la Mungu, bali pia mafundisho ya Kanisa katika lugha ya Bahasa Indonesia, ili yaweze kufikiwa watu wengi iwezekanavyo. Na Nicholas pia alisisitiza hili, akielezea utume wa katekista na picha ya ‘daraja’ linalounganisha. Hilo lilinigusa, na kunifanya nifikirie mwonekano wa ajabu, katika visiwa vikuu vya Indonesia, maelfu ya “madaraja ya moyo” yakiunganisha visiwa vyote, na hata zaidi ya mamilioni ya “madaraja” hayo yakiunganisha watu wote wanaoishi huko! Hapa kuna taswira nyingine nzuri ya udugu: mpambano mkubwa wa nyuzi za upendo zinazovuka bahari, kushinda vizuizi na kukumbatia kila aina mbalimbali, na kufanya kila mtu kuwa “moyo mmoja na nafsi moja” (Mdo 4:32).

Baba Mtakatifu Francisko akijikita katika neno la Tatu kuhusu ‘Huruma’ alisema hiyo inaunganisha sana udugu. Kama tujuavyo kiukweli huruma siyo suala la kutoa sadaka kwa kaka na dada wenye kuhitaji, kwa kuwatazama kutoka juu hadi chini, kutoka juu ya uhakika binafsi na fursa binafsi, lakini kinyume cha kujifanya kuwa karibu na wengine, kujivua  kile kinachotuzuia kuinama ili kuingia kweli na mawasiliano na yule ambaye yuko chini hivyo kumwinua na kumpatia matumaini (Fratelli tutti, 70). Na si hiyo tu, inatakiwa hata kukumbatia ndoto na shauku za kukomboa na haki, kumtumza, kuwa mhamasishaji na mhudumu, kwa kuhusisha hata wengine, ili kupanua mtandao  na mipaka katika nguvu kubwa ya kutanua  hisani(Fratell tutti 203). Kuna wale ambao wanaogopa huruma, kwa sababu wanaona kuwa ni udhaifu, na badala yake wanajiinua, kana kwamba ni wema, ujanja wa wale wanaoangalia maslahi yao wenyewe huku wakijiweka mbali na kila mtu, wasijiruhusu kuguswa kwa chochote au mtu yeyote, hivyo kufikiria kuwa mwangalifu zaidi na huru katika kufikia malengo ya mtu. Lakini hii ni njia ya uwongo ya kuangalia ukweli. Kinachofanya ulimwengu uendelee si hesabu za maslahi - ambazo kwa ujumla huishia kuharibu uumbaji na kugawanya jumuiya - lakini upendo unaotolewa. Huruma haifichi maono halisi ya maisha, kinyume chake, inatufanya tuone mambo vizuri zaidi, kwa nuru ya upendo.

Katekesta alitoa ushuhuda
Katekesta alitoa ushuhuda

Baba Mtakatifu amegusia Jengi walilokuwamo kuwa  katika suala hili, “jengo la Kanisa Kuu hili, katika usanifu wake, linaonekana kwangu kufupisha vizuri sana kile tulichosema, katika ufunguo wa Maria. Kiukweli, linaungwa mkono, katikati paa  iliyoelekezwa, na safu ambayo sanamu ya Bikira Maria imewekwa. Hivyo anatuonesha Mama wa Mungu kwanza kabisa kama kielelezo cha imani, huku akiunga mkono kiishara, kwa “ndiyo” yake ndogo(Lk 1:38), jengo zima la Kanisa. Mwili wake dhaifu, unaoegemea nguzo, juu ya mwamba ambao ni Kristo, unaonekana kiukweli kubeba uzito wa ujenzi mzima, kana kusema kwamba, kazi ya mwanadamu na ustadi, haiwezi kujitegemeza peke yake. Kisha Maria anaonekana kama picha ya udugu, katika ishara ya kuwakaribisha, katikati ya lango kuu, wale wote wanaotaka kuingia. Na hatimaye yeye pia ni Picha  ya huruma, katika ulinzi wake juu na kulinda watu wa Mungu ambao, kwa furaha na huzuni, shida na matumaini, hukusanyika katika nyumba ya Baba.

Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amependa kunukuu kila ambacho Mtakatifu Yohane Paulo II alisema wakati wa ziara yake akiwahutubia maaskofu, mapadre na watawa. Yeye alitumia aya za Zaburi isemayo: ‘Laetentur insulae multae,’ yaani ‘Visiwa vyote vifurahi’ (Zan 96,1) na alikuwa amewaalika wasikilizaji wake kuitumia kwa kuwa mashuhuda wa furaha ya ufukuko na kutoa maisha ili hata visiwa vya mbali viweze kufurahi kwa kusikiliza Injili ambayowao wanakuwa wahubiri wa kweli, walimu na mashuhuda.  Kwa hivyo Papa amepyaisha ushauri huo na kuwatia moyo waendelea katika utume wa nguvu katika imani, wawe wazi kwa wote, katika udugu na karibu na kila mtu katika huruma. Amewaomba tafadhali wamwombee.

Hotuba ya Papa kwa maaskofu wa Indonesia
04 September 2024, 12:50