Safari ya Papa kuelekea Asia ndiyo safari ndefu zaidi ya upapa wake
Vatican News
Kilomita thelathini na tatu elfu juu ya anga ya Mashariki ya Mbali, kati ya Nchi nne za mabara mawili na kanda tofauti za wakati. Ziara ya kitume ya 45 ya Upapa ilianza, wakati ndege ya Papa ilipoondoka ardhini kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Fiumicino, Roma na kupinda kuelekea Indonesia kwa mruko wa kwanza wa kilomita elfu 11 kwa wastani wa masaa 13 ya kwenda.
Ni masaa hayo ambayo yatamchukua Papa Francisko, kwenye msafara wake akiwa na waandishi wa habari zaidi ya 70 walio kwenye ndege hiyo na kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Jakarta ambapo anatarajia kufika tarehe 3 Agosti 2024 majira ya saa 5.30 asubuhi, ikiwa ni saa 12.30 alfajiri ya masaa nchini Italia.
Salamu na baadhi ya watu wasio na makazi
Kama kawaida, Papa Francisko kabla kuondoka kuelekea Uwanja wa ndege alitangulia kwa salamu za mshikamano katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, mjini Vatican ambapo alibadilishana muda mfupi baada ya saa 10.00 jioni na wanaume na wanawake wapatao kumi na watano wasio na makazi, wakifuatana na Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican katika Chapisho la Baraza la Huduma ya Upendo ya Kipapa.