Siku ya II ya Papa huko Papua New Guinea imeongozwa na ukaribu,huruma na upole!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Francisko ikiwa ni siku yake ya kwanza akiwa katika Nchi ya Papua Guinea, Jumamosi tarehe 7 Septemba 2024 akiwa ni katika Ziara yake ya 45 ya Kitume, ilianza kwa kutembelea Gavana Mkuu wa Papua New Guinea, Bob Dada huko Port Moresby ambapo alimkaribisha Papa Francisko, na kutoa hotuba yake ambayo Mkuu wa Nchi hiyo alisifia utetezi wa Kanisa Katoliki wa amani, haki za binadamu na hatua muhimu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Baadaye Baba Mtakatifu alikukutana na mamlaka za kiraia na katika hotuba yake alisifu watu wa taifa hilo na kukumbusha mamlaka jukumu linalotokana na utajiri wa ajabu wa kiutamaduni na mazingira hivyo, watumie fursa hiyo kukuza ustawi wa wote bila ubaguzi. Na zaidi taifa hilo lijaribu kushinda changamoto ya tofauti ambapo inawezekana kabisa kuupatia ulimwengu ishara ya udugu na kuishi kwa maelewano, amani na zaidi amesisitizia sala ambayo imo katika kauli mbiu ya ziara ya kitume.
Baba Mtakatifu Francisko badaye katika siku hiyo alikutana na watoto wa mitaani na watoto walemavu nchini Papua New Guinea na kuwakumbusha kwamba kila mtu ni tofauti kwa sababu Mungu ndiye aliyewaumba hivyo, na hii imeokana na maswali ya watoto waliyomuuliza. Katika Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Caritas huko Port Moresby alisalimiana na watoto wapatao 800 wanaohudumiwa na Huduma za Mitaani na Huduma za Callan.
Hatimaye Baba Mtakatifu alihitimisha Siku yake kwa kukutana na Maaskofu wa Papua New Guinea na visiwa vya Solomoni, mapadre, mashemasi, waliowekwa wakfu, waseminari na makatekista katika Madhabahu ya Maria Msaada wa Wakristo , inayohudumiwa na Wasalesinai ambapo katika hotuba yake amefafanua juu ya ujasiri wa kuanza, uzuri wa kuwepo na matumaini ya kukua kama ilivyotolewa ushuhuda.
Hayo na mengine yalisikika katika kisiwa hiki kizuri kilichajaa utajiri wa mali ya asili na watu wake wa mila na desturi na mavazi yeye rangi zote zinowaka na zisizo waka.