Papa na Imamu wa Msikiti wa Istiqlal wametia saini "Tamko la pamoja la Istiqlal 2024" Papa na Imamu wa Msikiti wa Istiqlal wametia saini "Tamko la pamoja la Istiqlal 2024"  (Vatican Media)

Tamko la Istiqlal 2024:waamini wajibidishe kuhamasisha amani na mazungumzo!

Wakati wa Mkutano wa Kidini katika Msikiti wa Istiqlal huko Jakarta imesahiniwa Tamko la pamoja,kati ya Papa na Imamu Mkuu.Hati hiyo inasisitiza juu ya jitihada za waamini wote dhidi ya vurugu na kwamba Dini zina nafasi kubwa ya kuhamasisha amani na maelewano.

Vatican News

Ulimwengu wetu unakabiliwa na migogoro miwili mikubwa: “kupunguza utu na mabadiliko ya tabianchi.” Katika Tamko la pamoja la Istiqlal 2024 linatokana na mazingatio haya, ambapo Papa Francisko na Imamu Mkuu, Profesa Nasaruddin Umar, alitia saini tarehe 5 Septemba 2024 katika muktadha wa mkutano wa kidini katika msikiti mkubwa wa Jakarta. Azimio hilo linabainisha kwa uchungu kwamba "dini mara nyingi hutumiwa na kusababisha mateso kwa wengi katika ulimwengu unaozidi kuwa na vurugu. Kwa hiyo inasisitizwa tena kwamba "jukumu la kidini linapaswa kujumuisha kukuza na kulinda utu wa kila maisha ya mwanadamu na kwa hakika si kinyume chake. Wakati huo huo, "matumizi mabaya ya kazi ya uumbaji, ya nyumba yetu ya pamoja yanashutumiwa na matokeo ya uharibifu kama vile majanga ya asili na ongezeko la joto duniani ambalo hufanya mgogoro wa mazingira kuwa kikwazo cha kuishi kwa amani kwa watu.”

Mwitikio wa dini kwa majanga ya wakati wetu

Katika Tamko hilo aidha linaonesha ni majibu gani  au hatua ambayo dini, kupitia ahadi ya pamoja, zinaweza kutoa kwa majanga haya makubwa ya wakati wetu. Na wameonesha kuwa “kanuni ya falsafa ya Indonesia ya Pancasila” inaweza kutoa mchango wake.  Papa na Imamu Mkuu, kwa njia hiyo wanahimiza kuelekeza maadili ya kidini “kwa kukuza utamaduni wa heshima, utu, huruma, upatanisho na mshikamano wa kidugu ili kuondokana na uharibifu wa utu na uharibifu wa mazingira.” Kazi muhimu kama tunavyosoma katika hati hiyo, inawaangukia viongozi wa kidini ambao lazima washirikiane kwa pamoja kwa ajili ya manufaa ya ubinadamu.

Wakati wa hotuba ya Papa
Wakati wa hotuba ya Papa

Mazungumzo ya kidini lazima yathaminiwe zaidi

Katika Tamko la Pamoja la Istiqlal linabainisha tena kwamba: “Kwa vile kuna familia moja ya kibinadamu duniani, mazungumzo ya kidini yanapaswa kutambuliwa kama chombo muafaka cha kutatua migogoro ya ndani, kikanda na kimataifa, hasa inayosababishwa na matumizi mabaya ya dini.” Kwa njia hiyo hati kwa hakika inahitimisha kwa kutoa mwaliko kwa watu wote wenye mapenzi mema “kuhifadhi uadilifu wa mfumo ikolojia” ili kupitishia rasilimali za kurithi kwa vizazi vijavyo.

Papa akipewa zawadi
Papa akipewa zawadi
Papa na Imamu wametia sahini Tamko
05 September 2024, 09:56