Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko:akutana na watoto na kuwashukuru wahudumu wao

Baba Mtakatifu akitembelea shule ya watoto wenye ulemavu,aliwashukuru wafanyakazi kwa malezi yao na kwamba wanatufundisha jinsi ya kutunza na watoto hao pia kujiruhusu kuhudumiwa.Kuatika kuadhimisha miaka 60 ya shule hiyo,Papa alitia saini katika bango kabla ya kuwapungia mkono watoto na kuwaaga.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika Ziara yake ya 45 ya Kitume katika nchi za Asia na Oceania, Jumanne asubuhi, tarehe 10 Septemba 2024 akiwa huko Timor ya Mashariki, amekuwa na mkutano wa kugusa sana, hasa kwa kuwatembelea watoto wenye ulemavu na kuadhimisha tukio la kwanza la siku yake ya pili katika taifa hilo changa la Kikatoliki. Baba Mtakatifu mara tu alipowasili katika shule ya Irmas Alma, mitaa ilikuwa tayari imejaa watu waliokuwa na shauku ya kumsalimia. Kundi la watoto waliovalia mavazi ya kiutamaduni walimkaribisha, wakisindikizwa na kwaya ya waimbaji.

Papa Francisko alitembea shule ya walemavu
Papa Francisko alitembea shule ya walemavu

Katika jumba la Mtakatifu Vincenti wa Pauli, watoto 50 na watawa 28 walisubiri kwa shauku. Watoto watatu, wakitiwa moyo na mmoja wa masisita hao, walimwendea Baba Mtakatifu na kumkabidhi skafu ya kiutamaduni. Sr Getrudis Bidi, Mkuu wa Shirika, kisha akamkaribisha Papa Francisko na kushirikisha juu ya utume wa shule hiyo, ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka sitini. Alizungumza kuhusu kazi yao ya kutunza watoto wenye ulemavu na hasara mbalimbali, akiwataja kuwa  wao ni “hazina zilizokabidhiwa na Mungu.

Papa akutana na watoto walemavu
Papa akutana na watoto walemavu

Wakati wote huo wa kukutana kwa karibu, watoto watatu walikaa kimya chini ya  miguu ya  Baba Mtakatifu. Katika hotuba fupi, Papa Francisko alizungumza kuhusu Hukumu ya Mwisho, akieleza kwamba: “Yesu anapozungumza kuhusu Hukumu ya Mwisho, aliwaambia wengine: ‘Njoo pamoja nami’. Lakini hakusema: 'Njoo pamoja nami kwa sababu mlibatizwa, kwa sababu mmepokea kipaimara, kwa sababu mlifunga ndoa Kanisani, kwa sababu hamkusema uongo, kwa sababu hamkuiba..., Hapana!  Yeye alisema: ‘Njoo pamoja nami kwa sababu mmenitunza. Mlijishughulisha kwa ajili yangu na kwa hiyo kwa sababu hiyo  walimtunza yeye. Yesu aliwaita watu wamfuate kwa sababu walionesha kujali na huruma kwa wengine.

Papa ametembelea Shule ya walemavu
Papa ametembelea Shule ya walemavu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea aliitaja hii kama sakramenti ya maskini, akielezea kama upendo unaosongesha mbele, unaojenga,na kuimarisha. Alisisitiza  kwamba upendo huu upo wazi katika Shule ya Irmas Alma, na bila hayo, kazi ya shule isingewezekana. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu alitoa shukrani zake, akisema na kuelekeza mawazo yake kwa mvulana katika utunzaji wa shule hiyo aitwaye Silvano. Aliomba Silvano aletwe kwake na alipoushika mkono wa mvulana huyo, alimshukuru kwa kuwaruhusu dada hao wamtunze.

Wakati wa kukutana na watoto na wanao watunza
Wakati wa kukutana na watoto na wanao watunza

"Kama vile Silvano anavyojiruhusu kutunzwa, sisi pia lazima tujifunze kujiruhusu kutunzwa,”Papa alisema. Msisahau: lazima tujifunze kujiruhusu kutunzwa, kila mtu, kama vile wanavyojiruhusu kutunzwa. “Nataka kuwashukuru kwa yote mnayofanya, na pia ningependa kuwashukuru watoto—hawa wavulana na wasichana wanaotoa ushuhuda na kujiruhusu kutunzwa. Wanatufundisha jinsi ya kuwaacha. Mungu atujalie. Bila upendo, hii haiwezi kueleweka. Hatuwezi kuelewa upendo wa Yesu ikiwa hatutaanza kufanya mazoezi ya upendo. Kushiriki maisha na watu wenye uhitaji zaidi ni programu, programu yenu, ni programu ya kila Mkristo."

Papa akutana na watoto walemavu
Papa akutana na watoto walemavu

Asante” Ili kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 ya shule hiyo, Papa Francisko aidha alitia saini katika bango kabla ya kuwapungia mkono watoto wanaoimba kwaheri.

Wanawake waliomwinamia Papa
Wanawake waliomwinamia Papa

Hata hivyo Wanawake wengi walipiga magoti mbele ya Papa; mmoja, akiwa amekumbatia mikono, akazika kichwa chake katika vazi lake; alizimia na kusaidiwa haraka na usalama; mama, mwenye umri mdogo kuliko wengine, aliyeinama mbele kwa uzito wa mtoto mwenye ugonjwa wa hydrocephalus aliokuwa amembeba kwenye mfuko, alilia kwenye mkono wa Papa Francisko. Alitazama kila kitu kwa ukimya, alifunga macho yake nusu, akatoa baraka zake, akaweka mkono wake kwenye vipaji vya nyuso vilivyoonekana mbele yake. Hakuna maneno kwenye hafla hii: machozi tu. Wale wa moyoni.

Watoto walemavu
Watoto walemavu
10 September 2024, 15:54