2024.10.17 Bwana Ehud Olmert, Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli;Nasser Al-Kidwa, Waziri wa zamani wa mambo ya Nje wa Palestina;Gershon Baskin, na Samer Sinijlawi 2024.10.17 Bwana Ehud Olmert, Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli;Nasser Al-Kidwa, Waziri wa zamani wa mambo ya Nje wa Palestina;Gershon Baskin, na Samer Sinijlawi  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Olmert na Al-Kidva wakiwa na Papa,kwa mazungumzo ya mpango wa amani

Osservatore Romano,imefanya mahojiano na waziri mkuu wa zamani wa Israel na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Palestina waliokutana na Papa Francisko:Yerusalem inapaswa kusimamiwa na utawala wa wadhamini wa nchi tano zikiwemo Israel na Palestina.

Na Roberto Cetera na Angella Rwezaula – Vatican.

Bwana Ehud Olmert, mwenye umri wa miaka 78, Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel alikutana na Papa Francisko asubuhi tarehe 17 Oktoba 2024 akiwa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Bwana Nasser Al-Kidva, na ujumbe wa wanaharakati wa amani. Bwana Olmert alisema: "Ulikuwa mkutano muhimu na wa hisia. Baba Mtakatifu ameonesha nia ya ajabu katika juhudi za kuleta amani katika Mashariki ya Kati. Bwana Olmert, ambaye alikuwa waziri mkuu hadi 2009, ana historia muhimu katika mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati: serikali ya nchi  yake ilitia saini ya usitishaji wa mapigano katika vita vya Lebanon mwaka 2006, na alihusika na jaribio la mwisho la kweli la makubaliano ya kuundwa kwa mataifa hayo mawili na rais wa Palestina Mohamud Abbas, kama maendeleo ya makubaliano ya Oslo ya 1993, ambayo  hayakufikiwa.

"Papa Francisko alijitolea sana kwetu kwa zaidi ya nusu saa, akitufafanulia kwamba anafuata kila mabadiliko ya mzozo kila siku na kwamba kila siku anaungana na Wakristo wa Gaza. Tumewasilisha kwa Baba Mtakatifu pendekezo letu la amani kwa Gaza ambalo linatoa usitishaji wa mapigano mara moja, kuachiliwa kwa mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa na Hamas pamoja na kuachiliwa kwa wakati mmoja kwa idadi iliyokubaliwa ya wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Israeli, kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya kuanzishwa kwa mataifa mawili tofauti kwa amani baina yao." Hayo pia yalielezwa na  Waziri wa zamani wa Palestina Al-Kidva, ambaye anajulikana Palestina, sio tu kwa misimamo yake ya kuunga mkono amani, bali pia kwa kuwa mpwa wa kihistoria ya  kiongozi wa OPL Yasser Arafat.

Bwana Olmert, ni vipi mataifa mawili yanaweza kuundwa leo kwa uwepo wa makazi haramu yanayozidi kuongezeka ya walowezi wa Israel?

Tunakisia kunyakua kwa Israeli sehemu ya eneo ili kukubaliwa sawa na 4% ya Ukanda wa Magharibi wa Palestina, kwa kubadilishana na eneo la ukubwa sawa leo ndani ya mipaka ya Israeli. Eneo litakalotolewa kwa Wapalestina linaloruhusu ukanda unaounganisha Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Gaza.

Bwana Al-Kidva, ni suluhisho gani kwa Gaza?

Israel lazima iondoe kabisa jeshi lake kutoka Gaza na kuruhusu kuundwa kwa chombo cha Palestina kuisimamia. Tunafikiria, kama isho la muda, la Baraza la Makamishna linaloundwa na wanateknolojia na wataalamu wenye thamani inayotambulika na si wawakilishi wa kisiasa.Baraza hili linapaswa kuunganishwa na Baraza la Mawaziri wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, ambalo hatimaye linapaswa kuandaa uchaguzi mkuu katika ardhi za Palestina ndani ya miezi 24 hadi 36.

Bwana Olmert, je, zoezi hili la nia njema kwa pande zote mbili, kwa maoni yako, lingetosha kuhakikisha amani ya haraka?

Hapana. Pia tunafikiria haja ya "Uwepo wa Usalama wa Muda wa Waarabu" (TASP) kutumwa Gaza, ambayo pamoja na kujiondoa kwa Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) kunaweza kuleta hali ya utulivu. hiki cha Waarabu kinapaswa kuwa katika uhusiano na vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina (PNA), na kupokea mwongozo kutoka kwa Bodi ya Makamishna. Kazi yake kuu inapaswa kuwa kuzuia mashambulio zaidi yanayoweza kutokea dhidi ya Israeli kutoka Gaza.

Bwana Al-Kidva, ni kwa jinsi gani muungano wa serikali mbili ungehakikisha mustakabali wa amani?

Kupitia hitaji la Taifa la Palestina kuwa taifa lisilo la kijeshi, isipokuwa kwa mahitaji yake ya ndani ya polisi.

Bwana Olmert ungebaki wazi kwa tatizo kuu: hadhi ya Yerusalemu

Hili ndilo jambo ambalo Papa Francisko alipendezwa zaidi na mkutano wetu wa leo. Tunafikiria juu ya sheria maalum ya Yerusalemu, ambayo inapaswa kusimamiwa na udhamini wa mataifa matano (pamoja na Israeli na Palestina) ambayo ina mamlaka kamili juu ya kila sehemu ya jiji, kwa mujibu wa sheria zilizooneshwa mara kadhaa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwa jukumu maalum linalohusishwa na Ufalme wa Yordani, kama ilivyo tayari leo kwa Mlima wa Hekalu. Kwa vyovyote vile tunafikiri kwamba Mji kongwe unapaswa kuwa nje ya udhibiti wowote wa kisiasa na kujitolea kwa dini tatu za kuamini Mungu mmoja zinazouona kuwa mahali patakatifu pa sala.

Na vipi kuhusu madai ya pande zote mbili kuwa na Yerusalemu kama mji mkuu nchi?

BwanaOlmert: Yerusalemu inaweza kuwa mji mkuu wa Israeli katika sehemu ambazo tayari zilikuwa Israeli kabla ya tarehe 5 Juni 1967, pamoja na vile vitongoji vya Wayahudi vilivyojengwa baada ya '67, ambavyo vingeangukia katika hiyo 4.4% niliyotaja hapo juu.

Al-Kidva: na Al Quds, mji mkuu wa Palestina, itajumuisha vitongoji vyote vya Waarabu ambavyo havikuwa sehemu ya Israeli kabla ya vita vya '67.

Swali la mwisho Bwa Olmert, Mpango huu ulioelezwa vizuri unahatarisha kubaki kuwa na matamanio. Ni kinyume kabisa na nia ya serikali ya sasa ya Israeli ...

Yeyote anayenifahamu anajua ninachofikiria kuhusu serikali inayoongozwa na Netanyahu, na iliyo chini ya ushupavu wa itikadi kali wa Ben Gvir na Smotrich. Lakini ninafarijiwa na ukweli kwamba 70% ya Waisraeli wamechoshwa na muungano huu, na uharibifu mkubwa ambao umesababisha Israeli, na unaendelea kusababisha. Israel ni demokrasia yenye nguvu, na itaweza kuishinda serikali hii kidemokrasia.

Kwa njia gani mbadala?

Jumuiya ya kiraia ambayo imekuwa ikifanya maandamano makubwa dhidi ya Netanyahu kwa miaka miwili itaweza kuelezea uongozi mpya ambao hatuwezi hata kufikiria leo. Kwa sababu, narudia, Israeli ni nchi hai kidemokrasia na imara.

 

18 October 2024, 10:34