Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 6 Oktoba 2024 ametangaza majina ya Makardinali wapya ishirini na mmoja, watakaosimikwa rasmi tarehe 7 Desemba 2024  na kuadhimisha Misa ya Pamoja tarehe 8 Desemba 2024 Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 6 Oktoba 2024 ametangaza majina ya Makardinali wapya ishirini na mmoja, watakaosimikwa rasmi tarehe 7 Desemba 2024 na kuadhimisha Misa ya Pamoja tarehe 8 Desemba 2024  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Orodha ya Makardinali Wateule Watakaosimikwa 7 Desemba 2024

Baba Mtakatifu Francisko, ametangaza majina ya Makardinali wapya ishirini na mmoja, watakaosimikwa rasmi tarehe 8 Desemba 2024 katika Sherehe ya Bikira Maria Kukingiwa Dhambi ya Asili. Kati ya Makardinali wapya yumo Kardinali Angelo Acerbi, mwenye umri wa miaka 99. Mama Kanisa anatambua na kuthamini mchango wake katika maisha na utume wa Kanisa. Kutoka Barani Afrika tunaye Askofu mkuu Ignace Bessi Dogbo, wa Jimbo kuu la Abidjan, Pwani ya Pembe

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko anasema lengo la kuwa na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwenye Baraza la Makardinali ni kuweza kushuhudia Kanisa moja, takatifu, katoliki na la Mitume; kuendeleza umoja wa Kanisa huku wakiwa wameungana na Khalifa wa Mtakatifu Petro pamoja na Makanisa mahalia. Makardinali wapya kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake. Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanabainisha kwamba, kusudi uaskofu uwe na umoja usiogawanyika, Kristo Yesu alimweka Mtakatifu Petro, juu ya Mitume wengine, na katika yeye akatia chanzo na msingi unaodumu na unaoonekana wa umoja wa imani na ushirika wa Kanisa. Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, kwa nguvu ya Ukatoliki (Catholicitatis) huu kila sehemu huvipeleka vipaji vyake yenyewe kwa sehemu nyingine na kwa Kanisa lote, hivi kwamba sehemu zote pamoja, na kila moja pia, hukithiri kwa kushirikiana zenyewe kwa zenyewe na kufanya juhudi ili kupata ukamilifu katika umoja. Mamlaka kuu ya Kiti cha Mtakatifu Petro imepewa dhamana ya kusimamia ushirika wote wa mapendo, hulinda tofauti za haki zilizopo kwa kukazia ushirika katika mema na huduma makini kwa watu wa Mungu. Rej. Lumen gentium, 13.

Papa Francisko ametangaza majina ya Makardinali wapya 21 kwa Mwaka 2024
Papa Francisko ametangaza majina ya Makardinali wapya 21 kwa Mwaka 2024

Urika wa Maaskofu hauwezi kuwa na mamlaka usipounganika na Baba Mtakatifu, aliye Mwandamizi wa Petro, Mtakatifu na Mtume; kwa nguvu ya wadhifa wake kama Wakili wa Kristo na Mchungaji wa Kanisa lote, ana mamlaka katika Kanisa, iliyo kamili, ya juu kabisa na iwahusuyo wote (plenam, supremama et universalem potestatem) ambayo anaweza kuyatimiza kwa uhuru. Urika wa Maaskofu ni urithi wa urika wa Mitume katika kuongoza, kufundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu. Rej. Lumen gentium, 22-27. Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 6 Oktoba 2024 ametangaza majina ya Makardinali wapya ishirini na moja, watakaosimikwa rasmi tarehe 8 Desemba 2024 katika maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Kukingiwa Dhambi ya Asili. Kati ya Makardinali wapya yumo Kardinali Angelo Acerbi, mwenye umri wa miaka 99. Mama Kanisa anatambua na kuthamini mchango wake katika maisha na utume wa Kanisa. Yumo pia Askofu Mykola Bychok, C.Ss.R., wa Jimbo la “Saints Peter na Paul, huko Melbourne nchini Ukraine, Yeye ana umri wa miaka 44. Kutoka Barani Afrika tunaye Askofu mkuu Ignace Bessi Dogbo, wa Jimbo kuu la Abidjan, Pwani ya Pembe pamoja na Askofu mkuu Jean-Paul Vesco, O.P., Jimbo kuu la Alger, Algeria.

Kardinali mteule Angelo Acerbi mwenye umri wa miaka 99
Kardinali mteule Angelo Acerbi mwenye umri wa miaka 99

Na orodha rasmi ni kama ifuatayo!

1. Askofu mkuu Angelo Acerbi, Balozi Mstaafu wa Vatican.

2. Askofu mkuu Carlos Gustavo Castillo Mattasoglio, wa Jimbo kuu la Lima, Perù

3. Askofu mkuu Vicente Bokalic Kalic Iglic C.M., wa Jimbo kuu la Santiago Argentina

4. Askofu mkuu Luis Gerardo Cabrera Herrera, O.F.M., wa Jimbo kuu la Guayaquil, Ecuador.

5. Askofu mkuu Fernando Natalio Chomalí Garib, wa Jimbo kuu la Santiago de Cile Chile.

6. Askofu mkuu Tarcisio Isao Kikuchi, S.V.D., wa Jimbo kuu la Tokyo, Japan

7. Askofu mkuu Pablo Virgilio Siongco David, wa Jimbo kuu la Kalookan, Ufilippin

8. Askofu mkuu Ladislav Niemet, S.V.D., wa Jimbo kuu la Beograd-Smederevo, Serbia

9. Askofu mkuu Jaime Spengler, O.F.M., wa Jimbo kuu la Porto Alegre, Brazil

10. Askofu mkuu Ignace Bessi Dogbo, wa Jimbo kuu la Abidjan, Pwani ya Pembe

11. Askofu mkuu Jean-Paul Vesco, O.P., Jimbo kuu la Alger, Algeria.

Makardinali ni washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro
Makardinali ni washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro

12. Askofu Paskalis Bruno Syukur, O.F.M., wa Jimbo la Bogor, Indonesia.

13. Askofu mkuu Dominique Joseph Mathieu, O.F.M. Conv., wa Jimbo kuu la Teheran Ispahan, Iran.

14. Askofu mkuu Roberto Repole, wa Jimbo kuu la Torino, Italia.

15. Askofu Msaidizi Baldassare Reina, Jimbo kuu la Roma, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma.

16. Askofu mkuu Francis Leo, wa Jimbo Katoliki la Toronto, Canada.

Makardinali wapya: Changamoto ni ujenzi wa Kanisa la Kisinodi
Makardinali wapya: Changamoto ni ujenzi wa Kanisa la Kisinodi

17. Askofu mkuu Mwandamizi Rolandas Makrickas, Kiongozi mkuu, Kanisa kuu la Bikira Maria Mkuu, Jimbo kuu la Roma.

18. Askofu Mykola Bychok, C.Ss.R., wa Jimbo la “Saints Peter na Paul wa Melbourne nchini Ukraine

19. Padre Timothy Peter Joseph Radcliffe, OP, Mwanataalimungu.

20. Padre Fabio Baggio, C.S., Katibu mkuu msaidizi Idara ya Wahamiaji na Wakimbizi, Baraza la Kipapa la Maendeleo Endelevu ya Binadamu

21. Monsinyo George Jacob Koovakad, Afisa Mwandamizi Sekretarieti kuu ya Vatican na Mratibu wa Hija za Kitume za Baba Mtakatifu.

Makardinali Wateule
07 October 2024, 14:49