Papa aoneshwa masalia ya kiti cha Mtakatifu Petro Mtume!
Vatican News
Tarehe 2 Oktoba 2024, asubuhi, katika Sakrestia ya Basilika ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kabla ya Ibada ya Misa Takatifu ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XVI wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, “Baba Mtakatifu Francisko aliweza kuona Kiti cha Mtume Mtakatifu Petro(Cathedra Sancti Petri Apostoli).Hayo yaliripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican. Kama tulivyoarifiwa ni kwamba: “Kiti cha kale cha mbao ni ishara ya ukuu wa Petro, kwamba kilitolewa wakati wa kazi ya ukarabati wa kurejesha mnara wa Bernini kwenye Basilika hiyo.”
Kwa njia hiyo Karanakana (Fabbrica di San Pietro,) inayoongozwa na Kardinali Mauro Gambetti, ndiyo iliyowasilishwa kwa baba Mtakatifu masalia hayo ya kiti cha Kharifa wa Mtume Petro.