Papa atoa wito wa kuombea Haiti:Tusisahau kamwe kaka na dada zetu wa Haiti
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tafadhali tuwaombee wale walio Haiti ambao wanapata vurugu na kulazimika kukimbia. Ndiyo maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 13 Oktoba 2023 akizungumzia nchi ya Caribbean, yenye mawindo ya ukatili na wa makundi yenye silaha ambayo yaharibu maisha ya watu wasio na hatia. Papa Francisko alisema: “Ninafuatilia hali ya kushangaza nchini Haiti, ambapo vurugu zinaendelea dhidi ya watu wanaolazimika kukimbia makazi yao kutafuta usalama mahali pengine, ndani na nje ya nchi. Tusisahau kamwe kaka na dada zetu wa Haiti. Ninaomba kila mtu aombe kwamba aina zote za vurugu zikome na kwa dhamira ya Jumuiya ya Kimataifa tuendelee kufanya kazi ya kujenga amani na maridhiano nchini, daima tukitetea utu na haki za wote.”
Siku chache tu zilizopita, Shirika la 'Human Rights Watch' liliripoti kuwasili kwa "mamia ikiwa sio maelfu"ya watoto waliosukumwa katika umaskini na njaa katika magenge ya watoto, wanaonyonywa kwa biashara haramu na waathiriwa wa unyanyasaji wa kila aina na vikundi vya wahalifu wasio waaminifu. Kwa hivyoShirika hilo HRWl iliitaka serikali ya mpito kuwapa ulinzi na upatikanaji wa bidhaa na huduma muhimu. Watoto hao wanaandikishwa na makundi ya wahalifu, ambayo sasa yanadhibiti karibu asilimia 80 ya mji mkuu wa Port-au-Prince, kufuatia kuimarika kwa operesheni za polisi na vikosi vya kimataifa na vya ndani. Kulingana na Shirika la kimataifa la Watoto (Unicef), kuna takriban watu milioni 2.7, wakiwemo watoto nusu milioni, wanaolazimika kuishi chini ya udhibiti wa magenge ambayo yanaendelea kusababisha mamia ya vifo.