Papa baada ya Sala ya Malaika wa Bwana:Wito wa kuombea amani kwa nchi zinazoteswa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko , Sominika tarehe 20 Oktoba 2024 akiwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mara baada ya maadhimisho ya Ibada Takatifu ya kuwatangaza watakatifu wa Kanisa 14 wakiwa ni Ndugu, Mapadre, na waliowekwa wakfu ambao walijipanua katika wito wa kumfuasa Kristo hadi mwisho alisema "Kabla ya kumalizika kwa adhimisho hili la Ekaristi, ninawashukuru ninyi nyote, ambao mmekuja kuwaheshimu Watakatifu wapya.
Papa aliongeza: "Nawasalimu Makardinali, Maaskofu, mapadre, watu waliowekwa wakfu, hasa Ndugu Wadogo na Waamini wa Maronite, Wamisionari wa Consolata, Masista Wadogo wa Familia Takatifu na Waoblate wa Roho Mtakatifu, pamoja na makundi mengine ya mahujaji waliotoka sehemu mbalimbali."
Katika sherehe hii kulikuwa na uwakilishi mbali mbali hata wa mkuu wa chi ya Italia Bwana Sergio Mattarella , kwa njia hiyo Papa katika salamu zake aliendelea "Ninatoa salamu za kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, wajumbe wengine rasmi na mamlaka za kiraia."
Miaka 60 ya kutangazwa mashahidi wa Uganda
"Ninasalimia kundi kubwa la mahujaji wa Uganda, pamoja na Makamu Rais wa nchi hiyo, ambao wamekuja kwa ajili ya kuadhimisha miaka sitini baada ya kutangazwa kuwa watakatifu Mashahidi wa Uganda."
Ushuhuda wa Padre Giuseppe
Papa Francisko alisema "Ushuhuda wa Mtakatifu Giuseppe Allamano unatukumbusha umakini unaohitajika kwa watu dhaifu na walio hatarini zaidi. Ninafikiria hasa watu wa Yanomami, katika msitu wa Amazonia wa Brazili, miongoni mwa wajumbe ambao muujiza unaohusishwa na kutangazwa kuwa mtakatifu leo ulitokea." Baba Mtakatifu ameongeza: “Ninatoa wito kwa mamlaka za kisiasa na za kiraia kuhakikisha ulinzi wa watu hawa na haki zao za kimsingi na dhidi ya aina yoyote ya unyonyaji wa hadhi yao na maeneo yao."
Siku ya kimisionari ulimwenguni
Papa Francisko mtazamo wake pia katika siku muhimu ya utume ambapo amesema: "Leo tunaadhimisha Siku ya Wamisionari Ulimwenguni, ambayo mada yake - "Enendendi kawaalike watu wote kwenye karamu"(taz Mt 22:9) - inatukumbusha kwamba tangazo la kimisionari ni kupeleka kwa kila mtu mwaliko wa kukutana na Bwana, ambaye anatupenda na anataka tushiriki furaha ya mchumba wake. Kama Watakatifu wapya wanavyotufundisha: "Kila Mkristo ameitwa kushiriki katika utume huu wa ulimwengu wote kwa ushuhuda wake wa kiinjili katika kila mazingira" (Ujumbe wa Siku ya XCVIII, ya Kimisionari Ulimwenguni 25 Januari 2024).Na tuwaunge mkono, kwa maombi na msaada wetu, wamisionari wote ambao, mara nyingi kwa kujitolea sana, wanapeleka tangazo zuri la Injili katika kila sehemu ya dunia."
Kuombea amani nchi zenye migogoro ya kivita
Hatimaye Baba Mtakatifu kama kawaida yake ametoa wito katika maeneo ya kivita. Papa amesema: "Na tunaendelea kuombea watu wanaoteseka kutokana na vita-Palestina inayoteswa, Israeli, Lebanon, Ukraine inayoteswa, Sudan, Myanmar na zingine zote - na tunaomba zawadi ya amani kwa wote. Bikira Maria atusaidie kuwa, kama yeye na kama Watakatifu, mashahidi jasiri na furaha wa Injili."