Papa Francisko:tuungane na watoto milioni moja ya kusali Rozari
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Dominika tarehe 13 Oktoba 2024, Baba Mtakatifu mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, alielezea juu ya Mpango wa kampeni ya Shirika la Misaada kwa Kanisa lenye mahitaji iliyopangwa kufanyika tarehe 18 Oktoba 2024 ili kuunga mkono Kanisa na wale wote wasiojua upendo na amani ya Kristo. Baba Mtakatifu alisema: "Ijumaa ijayo, Oktoba 18, Shirika la "Msaada kwa Kanisa hitaji litendeleza mpango wa "Watoto milioni moja kusali Rozari kwa ajili ya amani duniani". Asante kwa wavulana na wasichana wote wanaoshiriki! "Tunaungana nao na kujikabidhi kwa maombezi ya Mama - ambaye leo hii ni kumbukumbu ya tukio la mwisho la Fatima na kwa maombezi ya Mama tunawakabidhi Ukraine wanaoteswa, Myanmar, Sudan na watu wengine wanaoteseka kwa vita na kila namna ya jeuri na taabu.”
Maana ya kampeni
Kupitia kampeni ya “Watoto milioni moja ya kusali Rozari”, kwa mujibu taarifa za Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (AACS)tunasoma kwamba: “tunajifunza kuweka imani yetu kwa Mama Yetu, ili aweze kuingilia kati kuunga mkono Kanisa na wale wote wasiojua upendo na upendo wa amani ya Kristo." Kuwaelimisha watoto wadogo “katika imani na sala ni jambo la msingi”, kwa kuwa “wanaweza kuwa vyanzo vya uinjilishaji kwa wengine, huku maombi yao, yaliyozaliwa na mioyo yenye imani, yanamvutia Roho wa Mungu ulimwenguni”.
Mipango katika nchi zenye matatizo
Sambamba na maombi hayo shirika hili, (ACS)linasaidia mipango inayolenga kuboresha maisha ya watoto wanaopitia hali ngumu duniani, kama vile watoto wa Lebanon, ambapo wanajaribu kudhamini vifaa vya shule kwa wale ambao hawana, au wale wa Sudan Kusini, Cuba na Uruguay, ambapo Biblia hutolewa kwa watoto ili kuwaongoza kwenye "safari yao ya imani".