Papa Francisko:Kanisa lisijiuzulu bali lijichafue mikono katikati ya maovu ya ubinadamu

Katika mahubiri ya Misa ya kuhitimisha kikao cha pili cha Sinodi ya Maaskofu Papa Francisko anatoa taswira ya jumuiya ya kikanisa ambayo tumwombe Bwana atupe Roho Mtakatifu ili tusikae katika upofu wetu,upofu unaoweza kuitwa ulimwengu,urahisi ambao unaweza kuitwa moyo uliofungwa.Upofu wa kuwa watumwa wa kutumikisha watoto,sehemu nyingi za dunia kwa ajili ya kazi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika dominika ya 30 ya Mwaka B wa Kanisa, tarehe 27 Oktoba 2024, Baba Mtakatifu Francsiko ameongoza Ibada ya Misa Takaatifu, ya kufunga Sinodi ya Maaskofu iliyoanza tangu tarehe 2 Oktoba kwa kuudhuliwa na washiriki kutoka Ulimwenguni kote wakiwakilisha Kanisa la Ulimwengu. Tukio kuu la Kanisa ambalo linazidi kutufundisha namna ya kuishi kisinodi ma kimarisha ile kauli mbiu iliyoongoza vipindi vyote hivi vya sinodi tangu ianze 2021 isema: Kanisa la Kisinodi, Ushiriki, ushirika na Umisionari, tutembee Pamoja.” Mara baada ya masomo ya liturujia, Baba Mtakatifu Francisko amesema kusema kuwa:“Injili inatuonesha Bartimayo, kipofu ambaye analazimishwa kuomba omba kando ya barabara, mtu asiye na matumaini ambaye, hata hivyo, anapomsikia Yesu akipita, anaanza kumlilia. Alichobaki nacho ni hiki: kulia uchungu wake na kumpelekea Yesu hamu yake ya kupata kuona tena. Na huku kila mtu akimshutumu kwa sababu wamevurugwa na sauti yake, Yesu anasimama. Kwa sababu Mungu daima husikiliza kilio cha maskini na hakuna kilio cha maumivu kisichosikika mbele zake.”

Papa ameongoza misa ya kufunga sinodi 27 Oktoba 2024
Papa ameongoza misa ya kufunga sinodi 27 Oktoba 2024

Baba Mtakatifu francisko amesema “Leo, katika hitimisho la Mkutano Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, tukiwa tumebeba mioyoni mwetu shukrani nyingi kwa kile tulichoweza kushiriki, tuzingatie kile kinachotokea kwa mtu huyu: hapo mwanzo, “aliketi kando ya njia akiomba” (Mk. 10:46), huku mwishoni, baada ya kuitwa na Yesu na kupata kuona tena, “alimfuata njiani” (Mk 10, 52). Jambo la kwanza ambalo Injili inatuambia kuhusu Bartimayo ni hili: alikaa kuomba. Msimamo wake ni mfano wa mtu ambaye sasa amejifungia kwa maumivu yake mwenyewe, akiketi kando ya barabara kana kwamba hakuna kitu kingine cha kufanya zaidi ya kupokea kitu kutoka kwa mahujaji wengi waliopitia jiji la Yeriko wakati wa Pasaka. Lakini, kama tunavyojua, kuishi kweli huwezi kukaa tuli: kuishi ni kusonga mbele kila wakati, kujiweka katika njia, kuota ndoto, kupanga na kufungua siku zijazo. Basi, Bartimayo, kipofu, anawakilisha upofu wa ndani unaotuzuia, hutufanya tutulie tuli, hutufanya tuendekeze ukingo wa maisha, bila tumaini tena. Na hii inaweza kutufanya tufikirie sio tu juu ya maisha yetu ya kibinafsi, lakini pia juu ya kuwa kwetu Kanisa la Bwana. Mambo mengi, njiani, yanaweza kutufanya tuwe vipofu, tushindwe kutambua uwepo wa Bwana, tusiwe tayari kukabiliana na changamoto za ukweli, wakati mwingine tusijue jinsi ya kujibu maswali mengi ambayo yanatulilia kama Bartimayo anavyofanya na Yesu.

Misa ya kufunga Sinodi
Misa ya kufunga Sinodi

Hata hivyo, tukikabiliwa na maswali ya wanawake na wanaume wa siku hizi, changamoto za wakati wetu, uharaka wa uinjilishaji na madonda mengi yanayowasumbua wanadamu, Papa amekazia kusema:  “hatuwezi kukaa kimya. Hatuwezi kukaa tuli.” Kanisa lililoketi, ambalo karibu bila kutambua linajitenga na maisha na kujifungia pembezoni mwa ukweli, ni Kanisa ambalo linahatarisha kubaki kipofu na kutulia katika usumbufu wake lenyewe. Na tukikaa katika upofu wetu, tutaendelea kutoona uharaka wetu wa uchungaji na matatizo mengi ya ulimwengu tunamoishi. Tafadhali, tumwombe Bwana atujalie Roho Mtakatifu ili tusikae katika upofu wetu, upofu unaoweza kuitwa ulimwengu, ambao unaweza kuitwa urahisi, ambao unaweza kuitwa moyo uliofungwa ... upofu wetu, katika upofu wetu.” Hebu tukumbuke hili badala yake: Bwana hupita, Bwana hupita kila siku, Bwana daima hupita na kusimama ili kuponya upofu wetu. “Lakini je ninasikia anapita? Je, ninao uwezo wa kusikia hatua za Bwana? Je, ninao uwezo wa kutambua wakati Bwana anapopita?”

Misa ya kufunga Sinodi
Misa ya kufunga Sinodi

Na ni vyema kama Sinodi inatusukuma kuwa Kanisa kama Bartimayo: jumuiya ya wanafunzi ambao, wakihisi Bwana anapita, wanahisi furaha ya wokovu, wanajiruhusu kuamshwa na nguvu ya Injili na kuanza kulia kwake. Inafanya hivyo kwa kukusanya kilio cha wanawake na wanaume wote duniani: kilio cha wale wanaotaka kugundua furaha ya Injili na wale ambao badala yake wamehama; kilio cha kimya cha wale wasiojali; kilio cha wale wanaoteseka, cha maskini, cha waliotengwa, “cha watoto ambao ni watumwa wa kufanya kazi, waliotumikishwa sehemu nyingi za ulimwengu kwa kazi; sauti iliyovunjika, na kusikia sauti hiyo iliyovunjika ya mtu ambaye hana hata nguvu ya kumlilia Mungu, kwa sababu hana sauti au kwa sababu amejitoa mwenyewe.” Papa amesisitiza kuwa “Hatuhitaji Kanisa linalokaa chini na kukata tamaa, bali Kanisa linalosikia kilio cha ulimwengu” Papa ameongeza kusema: “ na Nataka kusema, labda mtu atashutumu hili - Kanisa ambalo linachafua mikono yake ili kumtumikia Bwana.”

Misa ya Kufunga Sinodi ya kisinodi
Misa ya Kufunga Sinodi ya kisinodi

Papa Francisko kwa njia hiyo alisema “kwa hivyo tunafika kwenye kipengele cha pili: ikiwa hapo mwanzo Bartimayo alikuwa ameketi, tunaona kwamba mwishoni, badala yake, anamfuata njiani. Huu ni usemi wa kawaida wa Injili unaomaanisha: akawa mfuasi wake, akaanza kumfuata. Baada ya kumlilia, kiukweli, Yesu alisimama na kumwita. Bartimayo, kutoka kuketi, akaruka juu na mara akapata kuona kwake. Sasa, anaweza kumwona Bwana, anaweza kutambua kazi ya Mungu katika maisha yake mwenyewe, na hatimaye anaweza kutembea kumfuata. Vivyo hivyo, sisi pia, Papa amesema “ tunapoketi na kuketi, wakati hata kama Kanisa hatupati nguvu, ujasiri na na uthabiti ni muhimu wa kuamka na kuendelea na safari, tafadhali tukumbuke, siku zote ni kumrudia Bwana, turudi katika Injili. Papa amekazia kusema “turudi kwa Bwana, irudieni Injili.” Daima na tena, anapopita, lazima tusikilize mwito wake, ambao huturudisha kusimama na miguu yetu na kututoa katika upofu. Na kisha kuanza kumfuata tena, kutembea pamoja naye njiani.

Misa ya kufunga Sinodi 27 Oktoba
Misa ya kufunga Sinodi 27 Oktoba

Baba Mtakatifu Francisko aliendelea kusema: "Na ningependa kurudia: Injili inasema juu ya Bartimayo kwamba “alimfuata njiani.” Hii ni picha ya Kanisa la Sinodi: Bwana anatuita, hutuinua tunapoketi au tunapoanguka, hutusaidia kupata tena kuona upya, ili katika mwanga wa Injili tuweze kuona mahangaiko na mateso ya ulimwengu; na hivyo, tukisimamishwa tena kwa miguu yetu na Bwana, tunapata furaha ya kumfuata njiani. Tunapomfuata Bwana njiani, hatumfuati tukiwa tumefungwa katika starehe zetu, hatumfuati katika mawazo yetu, bali tunamfuata njiani. Na tukumbuke hili daima: tusitembee sisi wenyewe au kulingana na vigezo vya ulimwengu, bali kutembea njiani, pamoja nyuma yake na kutembea pamoja Naye. Papa Francisko amekazia hilo kusema: lisiwe Kanisa lililoketi, na Kanisa lililosimama. Si Kanisa lililo kimya, bali liwe Kanisa linalosikia kilio cha wanadamu. Si Kanisa kipofu, bali Kanisa lililoangazwa na Kristo ambalo huleta nuru ya Injili kwa wengine.

Misa ya kufunga Sinodi
Misa ya kufunga Sinodi

Si Kanisa tulivu, Kanisa la kimisionari, ambalo hutembea na Bwana katika njia za ulimwengu.Na leo, tunapomshukuru Bwana kwa safari tuliyosafiri pamoja, tutaweza kuona na kuheshimu masalia ya  kiti cha kale cha Mtakatifu Petro, kilichoerjeshwa kwa uangalifu. Tukitafakari kwa mshangao wa imani, tukumbuke kuwa hiki ndicho kiti cha upendo, ni kiti cha umoja, ni kiti cha rehema, sawasawa na agizo hilo ambalo Yesu alimpatia mtume Petro kwamba asiwatawale wengine, bali wawatawale, watumikieni kwa sadaka. Na tukistaajabia dari kuu ya Bernini, yenye kung'aa zaidi kuliko hapo awali, tunagundua tena kwamba inaweka msingi wa kweli wa Basilica nzima, yaani, utukufu wa Roho Mtakatifu.

Mababa wa Sinodi
Mababa wa Sinodi

Hili ndilo Kanisa la Sinodi: jumuiya ambayo ukuu wake uko katika karama ya Roho, ambayo inatufanya sisi sote kuwa ndugu katika Kristo na kutuinua kuelekea kwake. Papa Francisko amebainisha kwamba “ basi tuendelee na safari yetu pamoja kwa ujasiri. Hata kwetu leo Neno la Mungu linarudia, kama lilivyomrudia Bartimayo: “Jipe moyo, inuka, anakuita”. “Ninahisi kuitwa? Hili ndilo swali la kujiuliza. Je, ninahisi kuitwa? Ninahisi dhaifu na siwezi kuamka? Je, ninaomba msaada? Tafadhali, tuweke chini vazi la kujiuzulu na kukabidhi upofu wetu kwa Bwana, tusimame na kupeleka furaha ya Injili, tuipeleke kwenye njia za ulimwengu.

Masalia ya Kiti cha Mtakatifu Petro kuwekwa katika maonesho
Masalia ya Kiti cha Mtakatifu Petro kuwekwa katika maonesho
Homelia ya Papa ya kufunga Sinodi ya Kisinodi 27 Oktoba 2024
27 October 2024, 11:45