Papa Francisko kwa vijana:msiache kusonga mbele daima kwa furaha na ujasiri!
Vatican News
“Wapendwa vijana, moja ya mambo muhimu zaidi ni kutembea...” Haya ni maneno yanayofungua ujumbe mfupi kwa njia ya video, ambao Baba Mtakatifu Francisko alirekodiwa kwa ajili ya vijana wote ulimwenguni, ikiwa ni sehemu ya kazi ya kikao cha II cha Sinodi ya kisinodi iliyoanza tangu tarehe 2 hadi 27 Oktoba 2024.
Ili kuwatia moyo vijana hao katika kusonga mbele na kama alivyosemwa mara nyingi, bila kukoma, Papa Francisko alitumia mfano wa maji kwamba:“Kijana anapotembea kila kitu kiko sawa, lakini kijana anaposimama... ni kama maji. Maji yanaposogea ni mazuri, lakini maji yakituama... yanaishia vibaya, ni mabaya huku ndani kukiwa na ‘wanyama’ (akimaanisha wadudu wadogo) wengi ndani”, alisema Baba Mtakatifu katika video hiyo fupi iliyorekodiwa na Kijana mmoja wa washiriki wa Sinodi inayoendelea wakati wa mapumziko kidogo ndani ya mkutano mkuu kwa ujumla.
Kwa njia hiyo, Video hiyo ilioneshwa mchana Jumatano tarehe 23 Oktoba 2024 wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican na kusambazwa kupitia tovuti na mitandao ya kijamii ya Sekretarieti Kuu ya Sinodi. Papa Francisko aliendelea kusema: "Maji yaliyochoka ndiyo uharibika kwanza. Kijana aliyechoka, ndiye wa kwanza kuharibika.” Kwa hiyo aliongeza Papa: ”Endeleeni mbele, tembea kila wakati. Tazameni mbele kwa ujasiri na furaha." Kutoka hapo ndipo lilijitokeza ombi lake la kawaida kwamba: "Ninawasalimu. Mniombee."