Papa:vita ni kujidanganya,msiamini kuwa wasioshindwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wito wa kusitisha kila aina ya vurugu ambao ulitolewa na Baba Mtakatifu, kwa mtazamao hata juu ya Ukraine, sala yake kwa ajili ya Jumuiya ya kimataifa, ili wasiache watu kufa kwa baridi nchini humo na baadaye kusitisha kabisa masambulizi ya Ndege za kudhibiti raia ambao daiwa wanashambuliawa. Alisisitiza hayo mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 13 Oktoba 2024.
Vita ni kushindwa na kuleta mateso makubwa yasiyo na maana
Baba Mtakatifu Francisko alisema: “Ninaendelea kufuatilia kwa wasiwasi kile kinachotokea Mashariki ya Kati, na kwa mara nyingine tena ninatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja kwa pande zote. Tufuate njia za diplomasia na mazungumzo ili kufikia amani. Niko karibu na watu wote wanaohusika katika Palestina, Israel na Lebanon, ambapo naomba vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa viheshimiwe. Ninawaombea waathiriwa wote, waliohamishwa, mateka ambao ninatumaini wataachiliwa mara moja, na ninatumaini kwamba mateso haya makubwa yasiyo na maana yanayotokana na chuki na kisasi yataisha hivi karibuni. Ndugu zangu, vita ni udanganyifu, ni kushindwa, kamwe havitaleta amani, kamwe havitaleta usalama, ni kushindwa kwa kila mtu hasa kwa wale wanaoamini kuwa hawawezi kushindwa. Acha, tafadhali.”