Papa,Misa ya kutangaza watakatifu:Ukaribu,huduma na upole!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Dominika tarehe 20 Oktoba 2024 amawatangaza Watakatifu wapya 14, mashuhuda wa imani katoliki wakati wa Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ambao, ulijaa mababa wa Sonodi, Makardinali, maaskofu wakuu, maaskofu, Mapadre, watawa kike na kiume na waamini Watu wa Mungu kutoka ulimwenguni kote kushuhudia tukio hili. Waliotangazwa ni Padre Giuseppe Allamano, Mmisionari wa Consolata, Sista Elena Guerra, Sista Marie-Léonie Paradis na Mashahidi kumi na mmoja wa Damasco. Baba Mtakatifu Francisko akianza mahubiri yake baada ya Injili alisema: “Kwa yakobo na Yohane, Yesu anawauliza “mnataka niwafanyie nini?”(Mk 10,36). Na kwa haraka baada anawauliza“Mnaweza kunywa kikombe ninachonywea, au kubatizwa katika ubatizo niliobatizwa?(Mk 10,38).
Yesu anaulizwa swali, kwa namna hiyo, anatusaidia kufanya mang’amuzi, kwa sababu maswali yanatufanya tugunduea kile ambacho kimo ndani mwetu, tunamulika kile tunachobeba ndani mwetu na mara nyingi hatujuhi. Baba Mtakatifu ameongeza kusema “tuache nasi tuhojiwe na Neno la Bwana. Tufikirie kwamba anatuuliza sisi, kila mmoja: Unataka nini nikufanyie wewe? Na la pili “jemnaweza kunywa katika kikombe sawa na changu?” Kwa njia ya maswali haya Yesu anatufanya kuibua uhusiano na matarajio ambayo mitume wanayo kuelekea Yeye na mwanga na vivuri vya kawaida ya kila uhusiano. Kiukweli Yakobo na Yohane, wana uhusiano na Yesu lakini wanajidai.
Wao walielezea shuku ya kukaa karibu na Yeye, lakini kwa kuchukua nafasi tu ya sifa, ya kujivika nafasi muhimu, ili “kukaa katika utukufu wake, kuume na kushoto kwake”(Mk 10,37). Kwa vyovyote vile wanafikiri Yesu kama Masiha wa ushindi, na utukufu na kutoka kwake wanasubiri aweze kushirikisha utukufu wake nao. Wanaona katika Yesu Masiha, lakini wanamfikiria kwa mantiki ya nguvu. Yesu hasimami juu ya maneno ya mitume, lakini anatelemka kwa kina, anasikiliza na kusoma mioyoni. Na katika mazungumzo, kwa njia ya maswali, anatafuta kufanya iibuke shauku ambayo nyuma yake kuna maombi yake.
Kwanza kabisa anawauliza “ Ninyi mnataka nifawanyie nini?”; na swali hili anaibua mawazo ya mioyo yao, anayaweka katika nuru ya matarajio yaliyojificha, na ndoto za utukufu ambazo wafuasi wanakuza kwa siri. Ni kama vile Yesu anataka kusema: “Mnataka niwafanyie nini?” na hivyo anawambia kwa kile wanachotamani kweli: Masiha wa nguvu na mshindi ambaye awapatie nafasi ya heshima. “Na mara nyingi katika Kanisa wazo hili linajitokeza: heshima na madaraka…” Baadaye, kwa swali la pili, Yesu anakataa picha hiyo ya Masiha, mtindo huu unawasaidia kubadili mtazamo, yaani kuongoka: “ Mnaweza kunywa katika kikombe ninyweapo, au kupokea ubatizo nibatizwao?”
Kwa namna hiyo Yeye anawaonesha wao kuwa siyo Maswali ambayo wanafikiri; ni Mungu wa upendo ambaye anainama ili kumfikia aliye chini; anayekuwa dhaifu ili kumuinua aliye mdhaifu, anayetenda kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya vita, na ambaye alikuja kwa ajili ya kuhudumia na siyo kwa ajili ya kuhudumiwa. Kikombe ambacho Bwana atakunywa ni sadaka ya maisha yake, yaliyotolewa kwetu kwa ajili ya upendo, hadi kifo, na kifo cha Msalaba. Kwa hiyo kuume kwake na kushoto kwake kutakuwepo majambazi wawili kama Yeye katika msalaba na sio waliotulia katika nafasi ya madaraka; majambazi wawili waliombwa na misumari na Kristo katika uchungu na sio kukaa katika utukufu. Baba Mtakatifu amesema “Mfalme aliyesulibiwa, mwenye haki aliyehukumiwa anajifanya mtumwa wa wote: Yeye kweli ni Mwana wa Mungu1 (Mk 15,39).
Anashinda na siyo anayetawala, lakini anayetumikia kwa ajili ya upendo. Papa ameomba kurudia “anashinda na si mtawala, lakini anayehudumia kwa upendo.” Papa ameogeza “Tumekumbushwa hata katika Barua kwa Wahebrania “Hatuna kuhani mkuu asiyeweza kushiriki katika udhaifu wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa katika mambo yote kama sisi.”(Heb 4,5).” Kwa njia hiyo Yesu anaweza kusaidia wafuasi kuongoka, kubadili mtazamo, “Ninyi mnajua kwamba wale wanaohesabiwa kuwa watawala wa mataifa wanawatawala na viongozi wao wanawaonea (Mk 10,42). Lakini sivyo hivyo miongoni mwenu anayemfuata Mungu ambaye anakijifanya mtumishi ili kuwafikia wote kwa upendo wake. Anayemfuata Kristo ikiwa anataka kuwa mkubwa lazima ahudumie, kwa kujifunza kutoka kwake.
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema, Yesu anaibua mawazo, shauku na mielekeo ya mioyo yetu kwa mara nyinyine tena matarajio ya utukufu, mamlaka na nguvu. Yeye anatusaidia kufikiria si kwa mantiki za ulimwengu huu, bali kwa mtindo wa Mungu ambaye anajifanya kuwa wa mwisho ili wa mwisho wainuliwe na kuwa wa kwanza. Katika maswali haya ya Yesu, kwa fundisho lake juu ya huduma, mara nyingi hayaeleweki kwetu sisi kama ilivyokuwa kwa mitume wake. Kwa kufuata Yeye, kutembea katika nyayo zake na kukaribisha zawadi ya Upendo wake ambao ubadili namna yetu ya kufikiria , tunaweza hata sisi kujifunza mtindo wa Mungu, ule wa huduma. Papa ameongeza: “Tusisahau maneno matatu yanayoonesha mtindo wa Mungu wa kutumikia: ukaribu, huruma na upole. Mungu huja karibu kutumikia; anakuwa na huruma ili kutumikia; anakuwa mpole ili kutumikia. Ukaribu, huruma na upole…”
Katika hili tunapaswa kutamani, si katika mamlaka, bali huduma. Huduma ni mtindo wa maisha ya kikristo. Hautazami orodha ya mambo ya kufanya, kana kwamba mara baada ya kufanae tunaweza kufikiri tumemaliza hatua yetu: anayehudumia kwa upendo hasemi: “sasa anapaswa afanye mwingine.” Hili ni wazo la mwajiriwa, na siyo la shuhuda. Huduma inazaliwa na upendo na upendo hauna kikomo, haufanyi mahesabu, unajituma na kujitoa. Haiishii tu katika kuzalisha ili kuleta matokeo, si utendaji wa hapa na pale, bali ni jambo linalotoka moyoni, moyo unaofanywa upya kwa upendo na upendo. Tunapojifunza kuhudumia, kila ishara ya umakini ni utunzaji, kila kilelezo cha upole, kila tendo la huruma linakuwa kioo cha upendo wa Mungu. Na hivyo tuendelea katika kazi ya Yesu ulimwenguni.
Baba Mtakatifu akigeukia watakatifu wapya amesema: “katika nuru hiyo tunaweza kuwakumbuka wafuasi wa Injili ambao leo hi wamekuwa watakatifu. Katika safari ya historia inayohumiza ubinadamu, wao walikuwa watumishi aminifu, wanaume na wanawake ambao walihudumia katika ushahidi na katika furaha kama Ndugu Ruiz Lopez na wenzake. Ni mapadre na waliowekwa wakfu hai wa shauku ya kimisionari, kama vile Padre Giuseppe Allamano, Sr Paradis, Marie Leonie na Sr Elena Guerra. Watakatifu hawa wapya waliishi mtindo wa Yesu: yaani wa huduma. Imani na utume ambao waliupeleka mbele hawakuzuiwa na tamaa za kidunia na upendeleo wa madaraka, bali kinyume chake walijifanya watumishi wa ndugu, wabunifu katika kufanya mema, kuwa na msimamo katika mataitizo, na wakarimu hadi mwisho. Tuombe kwa imani kwa maombezi yao, ili hata sisi tunaweza kufuata Kristo, kumfuata katika huduma na kuwa mashuhuda wa tumaini katika ulimwengu.