Papa:Apokeaye neema nyingi ndiye atoaye sadaka

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro,Papa ametoa onyo la kutochanganya maana ya kutoa sadaka na hisani na kutoa mwaliko wa kutazama mwombaji usoni wakati wa kutoa sadaka kama Yesu aliyesikia kilio cha Bartimayo,kipofu aliyeponywa.Unapotoa sadaka yako mtazame mwombaji usoni na kugusa mwili wake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Misa Takatifu ya kufunga Sinodi ya kisinodi iliyoanza tangu tarehe 2 Oktoba, Dominika ya 30 ya mwaka B wa Kanisa, tarehe 27 Oktoba 2024, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari nyingine kabla ya sala ya Malaika wa Bwana akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu akianza tafakari amesema: “Injili ya liturujia ya leo (Mk 10,46-56) inatunzumza juu ya Yesu ambaye anaponesha mtu kipofu. Jina lake ni Bartimayo, lakini umati wa watu njia wanamdharau: ni maskini ombaomba. Watu wale hawana macho kwa ajili ya kipofu huyo, wanamwacha, wanamdharau. Hakuna mtazamo wa utunzaji, hakuna hisia ya huruma. Hata Bartimayo haoni, lakini anasikia na kufanya asikike. Anapaza sauti kwa nguvu: Mwana wa Daudi, unirehemu (Mk 10,48). Yesu lakini anamsikia na kumuona. Anajiweka katika nafasi yake na kumuuliza:“ Je wataka nikufanyie nini?(Mk 10,51).

Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Dominika Oktoba 27
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Dominika Oktoba 27

Unataka nikufanyie nini?: Swali hili, mbele  ya mtu  kipofu, utafikiri ni uchochezi, kinyume chake ni jaribio.  Yesu yupo amamuuliza Batrimayo kweli anatafuta nini na kwa sababu gani. Ni nani kwako “Mwana wa Daudi”? Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amezidi kusisitiza kwamba: “Ndiyo hivyo Yesu anaanzia kumfungua macho ya kipofu. Kwa kufikiria mantiki tatu za mkutano huo ambazo zinakuwa mazungumzo yaani: kupaza sauti, imani na safari. Hiki ndiyo kilio cha Bartimayo, Imani ya Bartimayo na safari ya Bartimayo.Papa akianza  kudadavua mantiki hizo tatu amesema,  awali ya yote, ni kupaza sauti kwa Bartimayo ambapo si tu kuomba msaada. Ni uthibitisho wake. Ni kipofu anayesema: ‘Mimi nipo, nitazameni.’ ‘Mimi sioni Yesu.’ ‘Wewe unaniona”? Ndiyo Yesu anaona mtu anayeomba na anamsikiliza, kwa macho ya mwili na ya yale ya moyo.

Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana
Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana

“Lakini hebu tujifikirie tunapompita ombaomba fulani barabarani: ni mara ngapi tunatazama upande mwingine; ni mara ngapi tunampuuza, kana kwamba hakuwepo ... Kwanza: kilio. Na je tunasikia kilio cha ombaomba? Na Yesu anasemaje “Enenda zako, imani yako imekuponya” alisema Yesu (Mk 10,52). Bartimayo aliona kwa sababu anamini; Kristo ni nuru ya macho yake. Bwana anatazama kama Bartimayo anavyotazama Yeye. Je, ninamtazamaje mwombaji? Je, mimi humpuuza? Je, ninamtazama kama Yesu? Je, nina uwezo wa kuelewa maswali yake, kilio chake cha kuomba msaada? Je, unapotoa sadaka, ninamwangalia mwombaji machoni? Je, ninagusa mkono wake ili kuhisi mwili wake? katika giza la maisha yake, maskini na kipofu. Injili inatueleza kuwa aliacha vazi lake, yaani mali yake ya mwisho aliyo kuwa nayo ili kwenda kwa Yesu. Imani hii inaokoa kipofu kwa sababu ni uhusiano kamili wa tumaini na Kristo, nuru ya Ulimwengu.

Mahujaji wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Mahujaji wakati wa sala ya Malaika wa Bwana

Papa ameongeza kusema, hatimaye tunakuja neno ‘kutembea’; Bartimayo aliye takasika, “alimfuata Yesu njiani(Mk 10,52).  Lakini kila mmoja wetu ni Bartimayo, kipofu kwa ndani, anayemfuata Yesu mara tunapomkaribia. Tafadhali tusichanganyikiwe: kutoa sadaka si kufadhili. Anayepokea neema nyingi kutoka katika sadaka ndiye anayetoa, kwa sababu anaruhusu kutazamwa na macho ya Mungu. Bwana alimfungulia njia na kuifanya kuwa na hakika ya hatua zake. Mtu ambaye aliomba huruma alipokea neema nyingi sana: kipofu hakupata kuona tu, lakini hata mwelekeo wa maisha na katika kumfuasa Yesu. Kwa niaba ya Bartimayo, tunaweza kuwa kuwa mbadala mzuri: sisi waombaji wa wokovu. Wokovu wa uchungu, wa dhambi wa vita na wa kifo. Kwa kuangazwa na kukutana na Yesu, tunaweza kijiuliza: je ninaona ndugu mwombaji njiani? Ninajitambua kuwa mimi mwenyewe pia ni omba omba mbele ya Bwana? Je ninatafuta kwa imani huruma ya Mungu ambaye daima ananirehemu? Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amesema “  tuomba pamoja Maria pambazuko la wokovu, ili alilinde safari yetu katika nuru ya Kristo.

Tafakari ya Papa Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana Oktoba 27
27 October 2024, 12:34