2024.10.27 Angelus 2024.10.27 Angelus  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Watoto wengi ni waathirika wa vita duniani!

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa anakumbusha kumbukumbu ya miaka 75 ya Mikataba ya Geneva na kupyaisha sala ya amani,huku akitarajia mwamko wa dhamiri:wakati wa migogoro,maisha na heshima ya watu binafsi na watu lazima yaheshimiwe pamoja na miundo ya raia na maeneo ya ibada.Wazo pia kwa Padre Marcelo Pérez,aliyeuawa huko Mexico.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 27 Oktoba 2024, Baba Mtakatifu Francisko mara tu alipomaliza Ibada ya Misa Takatifu  ya kufunga Sinodi  katika Basilika ya Mtakatifu Petro, akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume kwa waamini na mahujaji alisema: "Ndugu na dada wapendwa! Leo tumehitimisha Sinodi ya Maaskofu. Tuombe kwamba yote tuliyofanya mwezi huu yaendelee kwa manufaa ya Kanisa. Tarehe 22 Oktoba 2024 ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka 50 tangu Mtakatifu Paulo VI, Tume ya mahusiano ya kidini na dini ya Kiyahudi ilipoundwa, na tarehe 28 Oktoba itakuwa ni kumbukumbu ya miaka 60 ya Tamko la Nostra aetate la Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican."

Malaika wa Bwana
Malaika wa Bwana

Mkutano wa kimataifa:Msalaba Mwekundu na Nusumwezi,Geneva

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea alisema:“Kesho Mkutano muhimu wa Kimataifa wa Msalaba Mwekundu na Nusu mwezi  utafunguliwa huko Geneva, miaka 75 baada ya Makubaliano ya Geneva.  Tukio hili na liamshe dhamiri ili, wakati wa migogoro ya silaha, maisha na utu wa watu binafsi na watu viheshimiwe, pamoja na uadilifu wa miundo ya kiraia na mahali pa ibada, kwa kufuata sheria za kimataifa za kibinadamu."

Kuuawa kwa Padre Marcelo Perez nchini Mexico

Inasikitisha kuona jinsi katika vita, mahali fulani, hospitali na shule zinaharibiwa. Ninajiunga na Kanisa pendwa la Mtakatifu Cristóbal de las Casas, katika jimbo la  Chiapas huko  Mexico ambalo linaomboleza kifo cha Padre Marcelo Pérez, aliyeuawa Dominika  iliyopita. Mtumishi mwenye bidii wa Injili na watu waaminifu wa Mungu. Sadaka yake, kama ile ya mapadre wengine waliouawa kwa ajili ya uaminifu kwa huduma, iwe mbegu ya amani na maisha ya Kikristo."

Kimbunga nchini Ufilippino

Baba Mtakatifu akitazama bara la Asia amesema "Niko karibu na watu wa Ufilipino waliokumbwa na kimbunga kikali sana. Bwana na awaimarishe watu hao waliojawa na imani."

Umati katika sala ya Malaika wa Bwana
Umati katika sala ya Malaika wa Bwana

Salamu kwa mahujaji

Nawasalimu, Waroma na mahujaji. Kwa namna ya pekee, ninawasalimu Washirika wa Señor de los Milagros, wa Peruvia huko Roma, ambao ninawashukuru kwa ushuhuda wao na kuwatia moyo kuendelea katika njia ya imani. Niwasalimia kikundi cha wazee cha Loiri Porto San Paolo, watoto wa Kipaimara cha Assemini (Cagliari), "Mahujaji wa Afya" kutoka Piacenza, Cistercian Oblates ya Kidunia ya Sanctuary ya Cotrino na Shirikisho la Mashujaa Maskini wa Saint Bernard. ya Clairvaux

Kuombea Amani

Papa ametoa wito wa kuombea amani na kusitisha vita kwa mara nyingine tena: "Na tafadhali endeleeni kuombea amani, hasa katika Ukraine, Palestina, Israel, Lebanon, ili ongezeko hilo la vita liishe na heshima kwa maisha ya binadamu ambayo ni matakatifu iwekwe kwanza! Wahathiriwa wa kwanza ni miongoni mwa raia: tunaona kila siku. Waathirika wengi sana wasio na hatia! Tunaona picha za watoto waliouawa kila siku. Watoto wengi sana! Tunaomba amani." Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko amesema: " Nawatakia wote Dominika njema. Na tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema , mchana mwema na kwaheri ya kuonana." 

Wito wa Papa baada ya sala ya Malaika wa Bwana 27 Oktoba 2024
27 October 2024, 13:00