Papa Fransisko:Utajiri wa kweli si mali ya dunia,bali kupendwa na Mungu!

Katika tafakari yake wakati wa Malaika wa Bwana kuhusu kifungu cha Injili ya Marko cha tajiri anayemkimbilia Yesu ili kumuuliza jinsi ya kuwa na uzima wa milele,Papa alikumbusha kwamba sisi sote tunahitaji furaha,lakini hii haipatikani katika utajiri,japokuwa katika kuhatarisha maisha kwa upendo wa Mungu,kutoa kila kitu kwa maskini na kumfuata.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 13 Oktoba 2024 akiwa katika Dirisha la kitume mjini Vatican, amewageukiwa waamini na mahujaji waliokuwapo katika Uwanja wa Mtakatifu na kuanza tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana. Baba Mtakatifu alianza kwa kusema “Injili ya liturujia ya leo (Mk 10,17-30) inatuambia kuhusu tajiri anayekimbia kumlaki Yesu na kumuuliza: “Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? (Mk 10,17). Yesu anamwalika aache kila kitu na kumfuata, lakini kwa huzuni, anaondoka kwa sababu –andiko  linasema hilo – “kweli alikuwa na mali nyingi” (Mk 10, 23). Na inagharimu kuacha kila kitu. Tunaweza kuona mienendo miwili ya mtu huyu: hapo mwanzo alikimbia, kwenda kwa Yesu; mwishowe, hata hivyo, anarudi nyumbani kwa huzuni. Kwanza ali kimbia kuelekea kwake, na kisha aliondoka akiwa na huzuni. Hebu tuzingatie hili.

Waseminari Chuo cha Kipapa Cha Urbano
Waseminari Chuo cha Kipapa Cha Urbano

Baba Mtakatifu amesema kuwa “Kwanza kabisa, mtu huyu anamkimbilia Yesu. Ni kama kwamba kuna kitu kilimsukuma moyoni mwake: kwa kweli, licha ya kuwa na mali nyingi, haridhiki, amebeba hali ya kutotulia ndani yake, anatafuta maisha kamili zaidi. Kama vile wagonjwa na wenye kupagawa walivyofanya mara nyingi ( Mk 3:10; 5:6), tunaona katika Injili, anajitupa miguuni pa Bwana; yeye ni tajiri, lakini anahitaji kuponywa.” Yesu anamtazama kwa upendo (Mk 10, 21); kisha, anampatia "tiba" ya kwenda kuuza kila kitu alicho nacho, kuwapatia maskini na kumfuata. Lakini, kwa wakati huo, hitimisho lisilotarajiwa linakuja: mtu huyu ana huzuni juu ya uso wake na anakwenda! Shauku ya kukutana na Yesu ilikuwa kubwa na ya haraka kama vile kuaga kutoka Kwake kulivyokuwa baridi na haraka.

Sisi pia tunabeba mioyoni mwetu uhitaji usiozuilika wa furaha na maisha yaliyojaa maana; hata hivyo, tunaweza kuanguka katika udanganyifu wa kufikiri kwamba jibu liko katika milki ya vitu vya kimwili na dhamana za kidunia. Yesu badala yake anataka kuturudisha kwenye ukweli wa shauku zetu na kutufanya tugundue kwamba, kiukweli, wema tunaotamani ni Mungu mwenyewe, upendo wake kwetu na uzima wa milele ambao yeye pekee anaweza kutupa. Utajiri wa kweli unatazamwa kwa upendo na Bwana - huu ni utajiri mkubwa, kama Yesu anavyofanya na mtu huyo, na kupendana kwa kufanya maisha yetu kuwa zawadi kwa wengine.

Mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro

Kwa hiyo, Baba Mtakatifu amebainisha kuwa, Yesu anatualika "kuhatarisha upendo": kuuza kila kitu ili kuwapa maskini, ambayo ina maana ya kujivua wenyewe na dhamana zetu za uongo, kuzingatia wale walio na shida na kugawana mali zetu, si vitu tu bali pia sisi wenyenywe na ni nini yaani  talanta zetu, urafiki wetu, wakati wetu, na kadhalika. Ndugu, tajiri huyo hakutaka kujihatarisha, upendo wake na  aliondoka na akiwa na  uso ulijaa huzuni.

Uwanja waulivyofurika kwa waamini na mahujaji
Uwanja waulivyofurika kwa waamini na mahujaji

Na sisi je? Hebu tujiulize: moyo wetu umeshikamana na nini? Je, tunawezaje kushibisha njaa yetu ya maisha na furaha? Je, tunajua jinsi ya kushiriki na wale walio maskini, walio katika magumu au wanaohitaji kusikilizwa kidogo, wanaohitaji tabasamu, neno linalowasaidia kupata tumaini tena? Au hilo linahitaji kusikilizwa. Tukumbuke hilo Papa amekazia kuonya kwamba : Utajiri wa kweli si mali ya dunia hii, mali ya kweli ni kupendwa na Mungu na kujifunza kupenda kama Yeye. Kwa kuhitimisha ameomba kuomba maombezi ya Bikira Maria, atusaidie kugundua hazina ya uzima ndani ya Yesu.

Tafakari ya Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana 13 Oktoba 2024
13 October 2024, 15:13