Papa kwa FAO:ubinadamu hujeruhiwa na dhuluma,hatua za haraka zifanyike!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko aliandika ujumbe wake kwa Dk Qu Dongyukwa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la FAO, IFAD na WFP, wakati wa kuadhimisha Siku ya 44 ya Chakula Duniani, katika kilele chake tarehe 16 Oktoba. Katika ujumbe huo Papa anabainisha kuwa “kiukweli kushughulikia na kutatua shida za chakula za wanadamu wa wakati wetu ambao, wamejeruhiwa na ukosefu mwingi, inahitaji hatua za haraka na madhubuti ili kuishi maisha bora na ni muhimu kuzingatia kanuni za ushirika na mshikamano kama msingi wa programu na miradi yetu ya maendeleo na kusikiliza maombi ya wale walio chini ya mnyororo wa ukosefu wa chakula kama vile wakulima wadogo na familia zinazohusika moja kwa moja katika kulisha watu.”
Kusikiliza mahitaji ya waliochini
Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu, “kusikiliza mahitaji yanayotoka chini, kuanzia wafanyakazi na wakulima, maskini na wenye njaa na kutoka kwa wale wanaoishi katika mazingira magumu katika maeneo ya vijijini yaliyotengwa haipaswi kamwe kuahirishwa. Ikiwa tunachukua “mwongozo wa haki tu kama mwongozo wa hatua yetu, ndipo mahitaji ya watu yatakapotoshelezwa.” Ni kanuni ya ikolojia fungamani” iliyopendekezwa na Papa katika waraka wa Laudato si', unaoomba kwamba mahitaji ya kila mtu na ya mtu mzima yazingatiwe, ili utu wao ulindwe katika uhusiano na wengine na kwa uhusiano wa karibu na utunzaji wa uumbaji.”
Haki msingi wa binadamu unapuuzwa
Baba Mtakatifu anakumbuka kwamba, kaulimbiu ya Siku hii inatualika kutafakari juu ya “haki ya chakula kwa ajili ya maisha bora na ya baadaye” inayokidhi “moja ya mahitaji ya kimsingi ya mwanadamu”, yaani, kula ili kuishi kulingana na viwango vinavyostahili. ambayo "inahakikisha uwepo wa heshima wa mtu.” Lakini tunaona kwamba haki hii mara nyingi inapuuzwa, Papa Francisko analalamika, na “haitumiki kwa usawa, na matokeo mabaya. Kwa hiyo Papa amesisitiza pendekezo la FAO la “mabadiliko ya mifumo ya chakula ambayo yanazingatia wingi na aina mbalimbali za vyakula vyenye lishe, vinavyopatikana, vyenye afya na endelevu ili kufikia"usalama wa chakula na lishe bora kwa wote.”
Ubinadamu unahitima hatua madhubuti kwa haraka kuish maisha bora
Ubinadamu unahitaji hatua haraka madhubuti za kuishi maisha bora, anaendelea Papa, Francisko akitenda pamoja na roho ile ile ya udugu na kujua kwamba sayari hii ambayo Mungu ametupa lazima iwe bustani iliyo wazi ili kuishi pamoja. Hili linahitaji maamuzi yenye msingi wa mshikamano, ambapo ulinzi wa vizazi vijavyo unakwenda sambamba na ule wa vizazi vya sasa, kupitia muungano wa ndani na kati ya vizazi, msingi wa udugu, unaotoa maana mpya kwa ushirikiano wa kimataifa, ambao lazima uhuishe FAO na mfumo mzima wa pande nyingi. Katika safari hii, Papa Francisko alihitimisha kwamba, Jumuiya ya Kimataifa itaweza kutegemea kutiwa moyo na Vatican na Kanisa Katoliki, na “mchango wao wa kistaarabu ili kila mtu apate chakula cha kutosha na chenye ubora wa kutosha kwa ajili yake na familia yake, kila mtu anaweza kuishi maisha ya heshima na pigo chungu la umaskini na njaa duniani vishindwe kabisa.”