2024.10.16 Papa Francisko amekutana na Chama cha Madkatari wapasuaji Italia. 2024.10.16 Papa Francisko amekutana na Chama cha Madkatari wapasuaji Italia.  (Vatican Media)

Papa,madaktari wa upasuaji:kila wakati mtu anaweza kuponywa!

Papa Francisko,Oktoba 16 akikutana na washiriki katika Kongamano la Kitaifa la Jumuiya ya Upasuaji ya Italia ya mada:"Mustakabali wa daktari wa upasuaji-daktari wa upasuaji wa siku zijazo"ambao lilifanyika,Roma amewasihi wawe"mafundi wa afya,walinzi wa maisha ya wale wanaoteseka.Kuna hatari,hata kwa madaktari,kupoteza wito wao wa kuweka wagonjwa au majeruhi katikati."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana Wanachama wa Jumuiya ya Upasuaji ya Italia mjini Vatican, Jumatano tarehe 16 Oktoba 2024. Akianza hotuba yake amewakaribisha kwa furaha katika fursa ya miaka 126 ya Kongamano la Kitaifafa la Chama chao iliyoongozwa na mada Mustakabhali wa daktari wa upasuaji - daktari wa upasuaji wa siku zijazo,” lililofanyika jijini Roma. Papa amewasalimia kwa moyo mkunjufu Rais wa Jumuiya, wajumbe wote. “Yeyote anayezungumza juu ya siku zijazo, anazungumza juu ya tumaini, mpago na kujitolea. Papa amwasifu kuwa wametengeneza mada nzuri! Na kwa maana hiyo  kazi yao ni ya thamani kwa mwanadamu, ambaye ni kiumbe mzuri na dhaifu, kiumbe mwenye hamu ya maisha na wakati ujao na wakati huo huo hatari sana.  Kwa sababu hiyo ni muhimu kwamba mtindo wao daima uwe wa kibinadamu na wa kitaaluma, kwa wale wanaotunza mateso, ili kwanza kabisa wauchukue  kwa moyo, kuchanganya uwezo na maadili katika hatua zao zote, kulingana na utamaduni wa afya  ambao ni huduma kwa mtu katika uadilifu wake.

Sayansi ni ya mwanadamu na si mwanadamu kwa ajili ya sayansi

Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kwamba katika kufikiria juu ya mustakabali wa daktari wa upasuaji kuanzia utamaduni wa kujitolea kwa ndugu, hasa ikiwa ni masikini na aliyetengwa daima ni mwanadamu anayeishi na kufa, ambaye anateseka na kuponya, sio tu viungo vyake au tishu. Kinyume chake, kuna hatari, hata kwa madaktari,katka kupoteza wito wao, kujiweka nje ya muungano huo wa matibabu, ambao huwaweka wagonjwa au majeruhi katikati.” Dawa ya kisasa, kiukweli, wakati mwingine huelekea kuzingatia sana mwelekeo wa kimwili wa mwanadamu, badala ya kumzingatia kwa jumla na upekee. Kwa hiyo, hata hivyo, mwili unakuwa kitu cha utupu cha uchunguzi wa kisayansi na uendeshaji wa kiufundi, kwa madhara ya mgonjwa, ambaye huchukua nafasi ya pili. Badala yake, sayansi ni ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sayansi! Papa amerudia kusema Sayansi ni ya kibinadamu.

Madaktari wawe mafundi wa afya,kutendea wengine upendo

Papa amesema "Leo, katika wakati ambapo upasuaji hutumia teknolojia nyingi mpya, ikiwa ni pamoja na akili mnemba, ni bora  kutosahau kamwe kwamba hakuna kitu kinachoweza kupuuza mkono wa upasuaji.  Upasuaji unamaanisha kazi iliyofanywa kwa mkono, uendeshaji wa mkono. Na ni kama hiyo: madaktari wa upasuaji lazima wajeruhi, wakate, na waponye. Kwa hivyo, wanapokuwa na mwili wa mwanadamu mikononi mwao, ulioumbwa kwa mfano wa Mungu, wanafanya kama “mafundi wa afya,” wakiwatendea wengine kwa uangalifu sawa na ambao wangependa kutendewa. Tafakari juu ya ishara ambazo, kama wataalamu, wanaweza kuzitumia pamoja, kama timu na washiriki wao, na wasiogope kukuza mafunzo ya kibinadamu, kisayansi, kiteknolojia na kisaikolojia, hasa kati ya vijana wenye sifa bora za siku zijazo ambao watatoka hapo madaktari wa upasuaji. Kazi yao na utume wao daima utakuwa muhimu sana.Kwa hiyo Papa amewaalika “kuwa walinzi wa maisha ya wale wanaoteseka.” Hata wakati mtu hawezi kuponya, wanaweza kutibiwa daima, ili kwamba  pasiwepo mtu anayefikiriwa au kujisikia kama kapotea.

Madaktari wawe wasamaria:Huruma,kukaribia na kufunga majeraha

Na katika suala hili, kwa madaktari wa upasuaji Papa amependa kuhitimisha kwa kuwapatia sura halisi ambayo inaweza kuhamasisha mustakabali wa taaluma yao: Picha ya Yesu, daktari wa roho na miili  ambaye ni ya mtu mzima,  iliyosimuliwa katika mfano huo wa  Msamaria Mwema (Luka 10:30-37 ). Ndani yake, mwenye kuchunga anaona na kuacha bila haraka: anayo huruma kwa wale anaokutana nao, anawakaribia na kuwafunga majeraha yao.” Papa amerudia kusema maneno hayo kuwa “anaona huruma, anakaribia na kufunga majeraha yake.” Kwa hiyo hizi ndizo tabia ambazo Papa amependeleza kwao  kwamba kuona kwa upendo, kuhisi huruma, kuwa karibu na kujali. Hivi ndivyo kila daktari mzuri anaweza kuwa jirani ya mgonjwa. Papa amewashukuru kwa kila kitu wanachofanya, hata kwa kujitolea sana. Aliwahimiza kujitolea kwa shauku kwa wanadamu wanaoteseka ambao sisi sote ni sehemu yao. Bikira Maria, afya ya wagonjwa, asindikize huduma yao, awafariji katika magumu ya kazi na utafiti. Amewabariki kila mmoja wao, familia zao,  wafanyakazi wote wa afya wanaoshirikiana na Chama chao na tafadhali wasisahau kumuombea.

Papa kwa madaktari wa upasuaji
16 October 2024, 17:09