Tafuta

2024.10.02 Wawakilishi wa Kiekumene wa Jimbo la Dresden-Meissen. 2024.10.02 Wawakilishi wa Kiekumene wa Jimbo la Dresden-Meissen.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa wanahija wa Dresden-Meissen:Maisha ya watu wengi hayana tumaini!

Papa Jumatano tarehe 2 Oktoba amekutana na wanahija wa Jimbo la Dresden-Meissen na Kanisa la Kilutheri la Kiinjili la Sassonia,mjini Vatican,akizungumzia kwaya alisema:"sanaa inahusu fumbo la Mungu,ambalo huenda mbali na mawazo na miktadha yetu.Kwa sababu katika makanisa,kuna utajiri mkubwa wa alama:mishumaa,uvumba,sanaa na muziki."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 2 Oktoba 2024 amekutana na wawakilishi wa kiekeumene, wanahija wa Jimbo la Dresden-Messen, Nchini Ujerumani na Kanisa la Kilutheri la Kiinjili la Sassonia, mjini Vatican ambapo katika hotuba yake amewakaribisha na kushukuru Askofu Landesbischof, Waziri, Meya,na ndugu wote lakini pia hata kwaya  nzuri sana ya nyimbo. Kufanya hija ina maana ya kujiweka katika safari, ambayo kwa kawaida ni kwenda madhabahu. Safari hiyo inageuka kuwa ishara ya kweli ya mchakato wa maisha na hatima kubwa ya kufikia ambayo ni Mungu mwenyewe, kama inavyojieleza vizuri katika lugha ya kijerumani ambayo walichagua kama kauli mbiu ya safari : Auf dich hoffen wir allein!” “Ni kwako tu, tunatumaini.”

Katika hija yao wanatarajia kama walivyoandika kugundua pamoja na kwa ajili ya watu wa nyakati zetu, hazina za kiroho za hija.” Papa amesema kuwa “Huu ni utajiri wote wa imani yetu ambayo ni zawadi ya Mungu tunayopokea na siyo tu kwa ajili yetu, lakini pia daima hata kwa wengine, kwa ajili ya watu wanaotuzunguka, wakiwemo wale ambao tunafikiri wako mbali na imani, ambao hawajawahi kusikia wanazungumzia Kristo au wanafikiri kuwa hawana lolote muhimu la kusema juu yao. Papa ameongeza: “ Hii ninafikiri kwamba maisha ya watu wengi leo hii wanakosa maana, matumaini na furaha ambayo ulimwengu hauwezi kutoa. "Kwa sababu hiyo Papa amewaomba "washirikishane maana, tumaini na furaha ya imani kwa wote, kwa uaminifu na unyenyekevu."

Wawakilishi wa Kiekuemene wa Jimbo la Dresden Meissen
Wawakilishi wa Kiekuemene wa Jimbo la Dresden Meissen

Ushuhuda wa watu na kuaminika ni kile ambacho kinahesabiwa wakati kinaonesha imani wazi. Na kama muktadha  wa uaminifu, Bwana mwenyewe anataja umoja wa wafuasi wake na kuomba Bwana: “Ili wote wawe na umoja na ulimwengu upate kuamini (Yh 17,21). Kwa niaba ya Kanisa, Papa Francisko amewashukuru kwa kuwa makini na utume huo wa kiekumene wa Yesu na  kujaribu kutafuta kuukamilisha kwa hija hiyo ya pamoja na zaidi ni muhimu katika maisha ya kila siku. Baba Mtakatifu amebainisha kwamba amejua kuwa miongoni mwao wengi ni watu wa kujitolea. Shukrani maalum imewaendea wao  kwa sababu huduma yao ya bure ni ushuhuda maalumu unaoaminika.

Papa  Francisko amependa pia kuwashukuru hao wa “Dresdner Kapellknaben”,(Kikundi cha Kwaya) kwa ajili ya ushuhuda maalum. Sanaa kwa ujumla, lakini muziki kwa namna ya pekee ni lugha ambayo inatambuliwa na wote na ina uwezo wa kutafsiriwa, kuhuisha, kufariji watu. Baadhi ya mambo ni magumu kueleza kwa maneno. Na hiyo inahusu hasa fumbo la Mungu, ambalo huenda mbali na mawazo na miktadha yetu. Na tazama kwa sababu katika makanisa, tuna utajiri mkubwa wa alama ambazo ni mhimu na za  dhati zinazoaminika kama vile: mishumaa, uvumba, sanaa, na muziki. Amewashukuru kwa maajabu ya pamoja, maelewano ambayo kwa sauti nyingi yanapatikana na yanatufanya kukumbuka kazi ya Roho Mtakatifu ambaye anaungnisha wengi. Amewashukuru kwa ushuhuda tena.

Wawakilishi wa kiekuemene wa Dresden-Meissen
Wawakilishi wa kiekuemene wa Dresden-Meissen

Papa amewaomba waendelee  kufanya kazi pamoja na kushudia tumaini ambalo limo ndani mwao (rej. 1Pt 3,15. Ameomba wakumbuke ishara ya kuwa chumvi wa dunia na nuru ya ulimwemngu, na mbegu ndogo; katika Biblia, kumejaa ishara hizi nyingi ambazo jambo dogo tu na kisichohesabiwa kinakua na kuwa kikubwa kwa neema ya Mungu, kitu kikubwa zaidi, kizuri zaidi ambacho kama wanadamu tusingeweza kutimiza peke yetu na nguvu zetu. Mnamo Oktoba 1989 , Papa Francisko amebainisha kwamba walianza kuwa na wazo, wakati baadhi ya wakristo waprotestanti na wakatoliki wa Dresda walipokusanyika kukabiliana na polisi. Ilikuwa ni muujiza ambao hawakuweza kuwapiga risasi hata moja, na hata katika miji mingine ilifunguliwa njia ya amani ambayo hakuna hata mmoja angefikiria uwezekano na hatimaye ilipelekea muujiza wa umoja wa Ujerumani. Tarehe 3 Oktoba kwa hiyo wao  watasherehekea tukio hili hapa Roma. Baba Mtakatifu hatimaye amewaomba wasali pamoja sala ya Baba Yetu wa Mbinguni kwa sala ambayo inaunganisha wakristo wote. Kasali Baba yetu ni kuomba kile ambacho kinahitajika kuishi, kwa ajili ya hija yao na ambapo mwisho wa tumaini kubwa la matumaini yetu yatatimizwa:  maelewano kamili ya umoja na Mungu na kati yetu.

02 October 2024, 15:59