Tafuta

Mchezo wa mpira. Mchezo wa mpira. 

Papa na Gazeti la Corriere dello Sport liwe uzoefu wa michezo kama wimbo wa maisha!

Katika ujumbe wake kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya gazeti la Corriere dello Sport-Stadio,Papa Francisko amehimiza kuungana kama maadili ya michezo yanavyofundisha.Makala ya gazeti,hata ya michezo,inaweza kufanya mengi mazuri,lakini pia inaweza kuharibu au kuchochea hali ya kutoaminiana,msiwe hivyo."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko Dominia tarehe 20 Oktoba 2024  katika fursa ya miaka 100 ya Gazeti la Corriere dello Sport-Stadio la mchezo kiwanjani anawapa hongera! Miaka mia moja ni hatua muhimu, nembo ya ushindi kubwa ya  kuweka kwenye ukuta wenu! Kubwa zaidi ya hiyo kwa usambazaji wa nakala milioni mbili zilizouzwa wakati wa ushindi wa Italia kwenye Kombe la Dunia la 2006! Wamekuwa na mbio kubwa katika miaka hii mia moja: baada ya yote, kati ya wale waliochangia kuzaliwa kwa gazeti kulikuwa na Enzo Ferrari ambaye alijua kuhusu injini na ushindi! Papa amemshukuru Mkurugenzi Ivan Zazzaroni kwa kumtumia barua nzuri inayozungumzia kumbukumbu ya miaka mia moja ya gazeti, na amefurahi kuwa karibu nao katika siku hii ya sherehe.

Uzoefu wa mchezo wa mpira wa vitambaa

“Nikifikiria kuhusu michezo, na kuhusu nchi yangu, Argentina, hata kabla ya kufikiria kuhusu vifaa bora vya kandanda, ninafikiria wakati tukiwa watoto tulicheza mpira wa miguu na mpira uliotengenezwa kwa vitambaa.” Mabingwa wengi walianza hivyo, wakicheza na marafiki kwa njia isiyojali kwenye uwanja ulioboreshwa kati ya nyumba, hata katika mazingira duni sana. Jinsi inavyopendeza kupata hisia za udugu: wanacheza, pamoja, na wanajua kwamba wao ni wapinzani tu uwanjani, lakini  kamwe si maadui. Wanajifunza furaha ya ushindi na wanajua jasho na kujitolea inavyogharimu, pia wanajifunza kutokana na kushindwa, kujaribu kuamka tena na kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa ili kujaribu kuyashinda wakati ujao, au kukubali tu utofauti ulio kati ya mtu na mtu  na bila kikomo: “sisi sote ni wa thamani na wa kipekee, lakini sisi si wakamilifu.”

Uzoefu wa mpira katika vituo vya Parokia

Wengine wanasema kuwa mimi ni shabiki wa Mtakatifu Lorenzo, timu ya Argentina: bado ni siri, lakini jambo moja linaonekana zuri kwangu katika historia ya timu hiyo. Wakati  vijana  walicheza barabarani mwanzoni mwa karne ya ishirini walikuwa wakitafuta nafasi salama ambapo wangeweza kucheza mpira wa miguu, Padre mmoja wa kiitaliano alikuwa ni Msalesiano Padre Lorenzo Massa, alifungua milango ya kituo na hapo akaanza historia nzuri. Leo hii  pia tunahitaji nafasi za kucheza michezo, hasa katika mazingira duni na yaliyotengwa zaidi, lakini zaidi ya yote tunahitaji watu wazima ambao wanawakaribisha watoto na vijana kihalisi, wanajua jinsi ya kusikiliza ndoto zao, na kutamani maisha bora ya baadaye pamoja nao.  Pia tunafikiri hapa Italia ni kiasi gani kizuri kimefanywa kupitia nyanja za parokia na vituo na ni vijana wangapi ambao sasa ni mabingwa wa michezo mara nyingi wanakumbuka kuwa wameanzia kutoka katika viwanja vya Parokia.

Mashindano ya michezo ni afya

Papa Francisko amebainisha kwamba gazeti lao gazi lina historia ndefu, na kwa nia yake linakusudia kuikumbatia Italia nzima, kwa matukio ya michezo yanayoihusu ndani ya mipaka yake na nje ya nchi: michezo ni moja ya mambo ambayo yanatufanya tujisikie kama watu wasio na vifungo,  kama vile wakati unaamka kuimba wimbo, nyumbani, uwanjani au katika viwanja vya michezo. Ni muhimu jinsi gani kutembea pamoja, kujisikia kuwa sehemu ya familia moja, na ya familia ya mataifa wakati wa Olimpiki au michuano ya dunia au ya bara: katika miaka ya hivi karibuni mara nyingi bado tumeona watu jirani, au vikundi ndani ya nchi sawa, wanaanza kupigana  wao wakiwa na silaha. Mashindano ya michezo ni ya afya, kwa sababu yanahitaji uvumilivu, kumsikiliza kocha, heshima kwa wapinzani, kwa sheria na kwa waamuzi, uratibu na wachezaji wa timu: katika ulimwengu, hata hivyo, lengo mara nyingi ni kuharibu mpinzani, kufanya sheria pekee, kukataa wale wanaotaka kudhibiti makabiliano kati ya vyama kwa mujibu wa sheria za kimataifa

Kukuza mchezo bila ubaguzi

Kueneza utamaduni mzuri wa michezo kwa maana hii inamaanisha kufanya ubinadamu kukua katika maadili yake mazuri na ya kweli na kwa hilo Papa ameshukuru. Ingawa kwa bahati mbaya katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya kutovumiliana, ambayo ni lazima kulaaniwa, “nina hakika kwamba kuna mifano mingi zaidi ambayo katika michezo tumeweza “kuunganisha,” bila rangi, tabaka, au imani za kidini kuwa vikwazo au vizuizi: “Ninawahimiza kukuza hali hii ya ubinadamu wa kweli na wa kukaribisha.” Tunapaswa kukataa mantiki yoyote ya kutengwa na vurugu, na kwa sababu hiyo tunajua vizuri kwamba neno lina thamani yake, kuelimisha kuhusu mema na uzuri, badala ya kuharibu. Makala ya gazeti, hata ya michezo, yanaweza kufanya mengi mazuri, lakini pia yanaweza kuharibu au kuchochea hali ya kutoaminiana lakini msiwe hivyo, tafadhali!” Papa ameonya.

Gazeti liwe njia ya uzoefu wa wimbo wa maisha

Kwa kuzungumzia ukarimu na uhamasishaji  fungamani wa binadamu: kwa sababu za shirika peke yake, haiwezekani kupata uzoefu wa kuishi  Olimpiki na Paralimpiki kwa wakati mmoja. Katika matoleo ya hivi karibuni huko Paris tulifurahiya mafanikio mengi ya wavulana na wasichana wa ajabu: kwa baadhi yao, maisha yalikuwa yamewapa medali ya dhahabu, kwa jinsi walivyoweza kushinda, shukrani kwa nguvu zao za ndani na msaada wa kila mtu, changamoto ya ulemavu binafsi. Michuano yao ni wimbo wa maisha! Gazeti lenu na lieleze ushindi na kushindwa, lakini liwe njia ya kufikiria na kupata uzoefu wa mchezo kama wimbo wa maisha! Asante kwenu kwa kile mlicho na kwa kile mnachofanya. Msisahau kuniombea.”

Ujumbe wa Papa kwa miaka 100 ya Corriera dello Sport-Stadio
20 October 2024, 11:12