2024.10.16 Papa atuma ujumbe wake kwa njia ya video katika Tasisi ya Kipapa ya Kitivo cha Taalimungu huko Sicilia. 2024.10.16 Papa atuma ujumbe wake kwa njia ya video katika Tasisi ya Kipapa ya Kitivo cha Taalimungu huko Sicilia.  

Papa kwa Kitivo cha Taalimungu:Taalimungu itumike katika ukombozi wa utamaduni

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa njia ya video Oktoba 16,katika ufunguzi wa mwaka mpya wa kitaalumawa Kitivo cha Kitaalimungu"Yohane Mtabatizaji,"Sicilia.Ameomba wafanye"michakato ya tafiti za kitaalimungu na kijamii kuhusu msamaha.Padre Puglisi,hakimu Livatino,mahakimu Borsellino na Falcone ni mfano wa haki,wakito mwaliko wa Taalimungu ya ukombozi wa utamaduni."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekabidhi changamoto mbali mbali kwa Taasisi ya Kipapa ya Kitivo cha Taalimungu huko  cha Sicilia kiitwacho: “Yohane Mbatizaji” kilichoko mjini Palermo, wakati wa ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo, tarehe 16 Oktoba 2024, ambapo katika maelezo yake kameeleza changamoto nadhaa kuanzia na: “mazungumzo ya kiekumene na Mashariki; mazungumzo ya kidini na Uislamu na Uyahudi; ulinzi wa utu wa binadamu wa nostrum Mare,  yaani bahari yetu ambayo mara nyingi ni mahali pa mantiki ya kifo,  nguvu ya kiutamaduni na kijamii za ibada maaru  za watu, rasilimali ya fasihi kwa ajili ya ukombozi wa heshima ya kiutamaduni ya watu; na kilio cha wahaathiriwa wa uhalifu wa kupangwa(mafia.) Kwa sababu hiyo Papa Francisko amekazia kusema kwamba “tunahitaji taalimungu inayoendelea katika maisha madhubuti ya mwanadamu." Ifuatayo ni ujumbe kamili kwa njia ya video wa Baba Mtakatifu Francisko.

“Ninayo furaha kuongea wakati wa ufunguzi wa Mwaka wenu mpya wa Masomo 2024/2025. Uwasilishaji kamili utawasilishwa kwenu. Ninajiweka katika nyayo za Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alitembelea Kitivo cha Sicilia tarehe 21 Novemba 1982, wakati wa ziara yake ya kichungaji huko Belice na Palermo. Kitivo chenu, kilichozaliwa na wito madhubuti wa kikanisa, kinaitwa kutoka ndani ya historia na kusikiliza silika ya imani waliyonayo watu wa Mungu, kuwa wahusika wakuu wa kukabiliana na changamoto hizo ambazo Mediterania inaleta ndani ya taalimungu kama vile: mazungumzo ya kiekumene na 'Mashariki; mazungumzo ya kidini na Uislamu na Uyahudi; ulinzi wa utu wa binadamu wa nostrum Mare, yaani Bahari Yetu, mara nyingi imekuwa mantiki ya kifo; nguvu ya kiutamaduni na kijamii ya Ibada maarufu ya “Uchamungu, kama Mtakatifu Paulo VI alivyosema; rasilimali ya fasihi kwa ajili ya ukombozi wa heshima ya kiutamaduni ya watu; na zaidi ya yote, changamoto za ukombozi zinazotokana na kilio cha wahanga wa mafia.

Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video katika fursa ya Ufunguzi wa kitivo cha Taalimungu huko Sicilia

Hii inahusu kujifunza ufundi wa taalimungu kama mfumaji wa mitandao ya kiinjili ya wokovu, kandokando ya mwambao wa Sicilia katika bahari ya  Mediterania; ni kazi ya subira inayojaribu kusimulia upendo wa Mwalimu, wenye uwezo wa kuamsha mshangao wa kukutana na urafiki. Mshangao, ambao ndio mshipa unaochochea imani. Hebu fikirieni  wakati huo ambapo Bwana alisimama, kando ya Bahari ya Galilaya, kuwatafakari wale wavuvi waliokuwa wakitengeneza nyavu zao (Mt 4:18-22): Ni nini kilimsukuma kuwaita karibu naye, kujizungusha na ubinadamu wao, kuwatuma kama wavuvi wa watu? Na kwa nini mitandao, katika akili ya Yesu, katika njia yake ya kufikiri, inakuwa ishara na chombo cha wokovu? Hii ndiyo kazi ya taalimungu kutoka Mediterania: kusuka mitandao ya wokovu, mitandao ya kiinjili aminifu kwa njia ya kufikiri na kumpenda Yesu; iliyojengwa kwa nyuzi za neema na kuunganishwa na huruma ya Mungu, ambayo Kanisa linaweza kuendelea kuwa, hata katika Mediterania, ishara na chombo cha wokovu kwa wanadamu (rej. Lumen gentium, 2). Na hii ndiyo njia ambayo taalimungu inaweza kupenda, na inaweza kuwa upendo.

Huu ni mfano halisi wa Msalaba: “Kutoka juu ya msalaba mtaalimungu anachochewa kuutazama uhalisia wa mwanadamu kwa macho ya mtu ambaye amejishusha chini kiasi cha kuwa mdogo kabisa wa wanadamu, akikataa haki zake za kimungu na kuchukulia hali ya mtumishi wake. Kwa hiyo napenda kufikiria mruko wa ukaribu, ambao unakamilisha mruko wa imani, ili nisiwe kizingiti cha historia, bali mfumaji wa mitandao ambaye anajua jinsi ya kufunga ubinadamu wa Kristo na Injili yake karibu naye. Papa Francisko alisema nyavu zinanafumwa na kupangwa upya zikiwa zimelala chini, na mara nyingi huku wanazifuma wakiwa wamepiga magoti.

Tusisahau kwamba hii ndiyo nafasi nzuri ya kumpenda Bwana: kwa magoti yetu. Inamaanisha kupitisha mtindo wa kuosha miguu na ule wa Msamaria Mwema ambaye anainama mbele ya majeraha ya mwathirika wa bahati mbaya mikononi mwa majambazi. Tunaweza kufikiria mikono ya wataalimungu kama hii: mikono inayosimulia kumbatio la Mungu, mikono inayotoa huruma,  msisahau neno hili, la huruma, ambayo ni mtindo wa Mungu na mikono inayoinua wale walioanguka na kuwaongoza kuelekea matumaini. Na tusisahau kwamba kuna kanuni moja inayoruhusiwa mara moja tu, ya  kumtazama mtu kutoka chini kwenda juu,  hasa wakati wa  kuinama na kuwasaidia wadhaifu kuinuka.

Kwa hiyo basi, taalimungu inahitaji na inajumuisha ushuhuda hadi kufikia hatua ya mtu kutoa maisha yake, kwa zawadi ya nafsi yake kwa njia ya kifo cha kishahidi. Nchi hii inajua mashahidi wakuu na wafiadini9, kutoka kwa Padre Pino Puglisi hadi hakimu Rosario Livatino, bila kusahau mahakimu Paolo Borsellino na Giovanni Falcone, na watumishi wengine wengi wa Serikali. Wao ni “viti vya kweli” vya haki, ambavyo vinakaribisha taalimungu kuchangia, kwa maneno ya Injili, kwa ukombozi wa kiutamaduni wa eneo ambalo bado lina alama kubwa ya janga la mafia. Tusisahau hili. Kwa hiyo, kufanya taalimungu katika bahari ya Mediterania ina maana ya kukumbuka kwamba, utangazaji wa Injili unapitia katika kujitolea kwa ajili ya kukuza haki, kuondokana na ukosefu wa usawa na utetezi wa waathirika wasio na hatia, ili Injili ya uzima iangaze daima na uovu na aina zake ukataliwe. Kuna hitaji la taalimungu yenye ahadi, ambayo inazama katika historia na kufanya mapendo ya Kristo kung'aa ndani yake.

Kwa maana hiyo, ningependa Kitivo kianzishe michakato ya utafiti wa kitaalimungu na kijamii juu ya msamaha, katika njia panda za uhalali, upinzani na utakatifu. Anzeni na ubunifu wa maabara halisi ya kitaalimungu na kijamii ya msamaha, kwa mapinduzi ya kweli ya haki! Na hii, ninapenda kusema, ni wito wa Kisiwa chenu. Hata hivyo, ni mahali pia ambapo tamaduni, historia na nyuso mbalimbali hukutana kwa maelewano, ambayo yanaweka taalimungu katika kukuza mazungumzo na Makanisa dada ya Mashariki ambayo pia yanaipuuza Mediterania. Njia ya mazungumzo ya kiekumene na ya kidini, hata kama ni magumu, ndiyo itakayopendekezwa na kuungwa mkono kupitia uzoefu wa kukutana, pia uzoefu wa majadiliano na ushirikiano katika kumsikiliza Roho Mtakatifu kwa pamoja. Ni urithi wa mashahuhuda wengi wa mazungumzo katika Mediterania. Kwa hiyo mmekabidhiwa utume wa kujiimarisha kama maabara ya taalimungu ya mazungumzo ya kiekumene na ya taalimungu ya dini inayoongoza na taalimungu ya mazungumzo ya kidini. Daima neno, mazungumzo, majadiliano na uwazi.

Katika muktadha huu, hatimaye, ulinganisho kati ya taalimungu  na fasihi inaonekana kuzaa matunda, dokezo ambalo pia limebainisha utafiti wa Kitivo chenu cha Kitaalimungu katika miaka ya hivi karibuni, zaidi ya yote kwa ajili ya uchaguzi wa kutambua kipaji hicho cha imani ambacho ni cha uzoefu wa watu. Fasihi mara nyingi husimulia hili na kuruhusu usomaji wa hali halisi ya Sicilia na Mediterania, ikiwasaidia ninyi nyote kugundua utambulisho wenu katika ishara ya mazungumzo na kuwafanya muwe na uwezo wa kuvua viatu vyenu “mbele ya nchi takatifu(taz. Kut 3.5), (Evangelii gaudium, 169). Kwa upande mwingine, fikira nyingi za Sicilia zingewezaje kueleweka bila fasihi, ya Pirandello, Verga, Sciascia, na bila mada zilizopo ambazo waliandika kurasa za kukumbukwa?

Wapendwa kaka na dada, Mediterania inahitaji taalimungu hai, ambayo inakuza mwelekeo wake wa kimazingira kwa ukamilifu, na kuwa kivutio kwa wote. Sitawisheni taalimungu hii kwa ahadi ya historia, kama vile Mungu katika mwili wa Mwanadamu alivyojisalimisha kwa machozi yetu na matumaini yetu. Kuzeni taalimungu ambayo, kutoka juu ya msalaba na magoti yenu  mbele ya wengine, hutumia maneno ya unyenyekevu, kiasi na kubwa, kusaidia kila mtu kukaribia huruma; na maneno ambayo yanatufundisha kutengeneza mitandao ya wokovu na upendo, ili kuzalisha historia mpya, iliyokita mizizi katika historia ya watu. Ninawakumbatia na kuwaomba, tafadhali, mniombee. Asante.

Papa kwa wasomi wa Taalimungu- Sicilia
16 October 2024, 17:55