Papa,Mkesha wa toba:Tunawezaje kuwa Kanisa la kisinodi bila upatanisho?

Tarehe Mosi Oktoba 2024,jioni,Papa ameongoza mkesha wa Toba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa washiriki wa Sinodi wakihitimisha mafungo ya kiroho tangu Septemba 30.Makardinali 7 walisoma maombi ya msamaha wa nyanyaso,mamlaka,kutojali wahamiaji,dhidi ya amani,wanawake,watu wa asili na kukosa kusikiliza.Shuhuda za kuhuzunisha za watu 3 walionusurika pia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ambalo takriban waamini 2,500 walikuwepo wakiwemo washiriki wote wa mkutano wa sinodi, uliopangwa kwenye viti ambavyo, kwa kutazama kutoka juu, vilizalisha umbo la msalaba, na ndiyo ilikuwa tukio la Mkesha wa Sala na Toba ya Kisinodi iliyoandaliwa na Sekretarieti Kuu ya Sinodi na Jimbo la  Roma kwa ushirikiano na Na Umoja wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa(Usg) na vijana.  Hii ilikuwa ni mkesha wa hatua ya mwisho wa safari ya sinodi, ambayo hata hivyo wameanza na mafungo ya kiroho.  Katika mkesha huo, kwaya mbili ziliongoza la Jimbo la Roma, na kundi la Wakongo. Mara baada ya sala, shuhuda mbali mbali  na maombi kwa makardinali saba wa Mabaraza ya Kipapa, Baba Mtakatifu Francisko alitoa tafakari yake. Akianza alisema: “Kama Wasiria walivyotukumbusha, "sala ya maskini hupitia mawingu"(35, 17). Tuko hapa waombaji wa huruma  za Baba, tukiomba msamaha. Kanisa daima ni Kanisa la maskini wa roho na la wenye dhambi katika kutafuta msamaha na si Kanisa la wenye haki na watakatifu pekee, au tuseme la wenye haki na watakatifu wanaojitambua kuwa maskini na wenye dhambi.

"Nilipendelea kuandika maombi ya msamaha ambayo yalisomwa na baadhi ya makardinali, kwa sababu ilikuwa ni lazima kutaja dhambi zetu kwa jina na ubini. Na tunazificha au kuzisema kwa maneno ya heshima sana ... Dhambi daima ni jeraha katika mahusiano: uhusiano na Mungu na uhusiano na kaka na dada. Ndugu, hakuna anayeokolewa peke yake, lakini ni kweli vile vile kwamba, dhambi ya mtu mmoja ina madhara kwa wengi: kama vile kila kitu kimeunganishwa kwa uzuri, pia kinaunganishwa na uovu. Kanisa kwa asili yake ni Kanisa la imani na tangazo ambalo daima ni la uhusiano, na kwa kuponya tu mahusiano ya wagonjwa tunaweza kuwa Kanisa la Sinodi. Tunawezaje kusadikika katika utume ikiwa hatutambui makosa yetu na hatuinami kuponya majeraha ambayo tumesababisha na dhambi zetu? Lilikuwa ni swali la Papa.

Mkesha wa Toba 1 Oktoba
Mkesha wa Toba 1 Oktoba

Baba Mtakatifu akiendelea alisema: "Na uponyaji wa jeraha huanza kwa kuungama dhambi tuliyofanya. Mfano kutoka katika Injili ya Luka ambayo tulisikia, unatuonesha watu wawili, Mfarisayo na mtoza ushuru, ambao wote wanakwenda hekaluni kusali. Mmoja alisimama na paji la uso wake juu, mwingine alikaa nyuma, na macho yake yakitazama chini. Mfarisayo anajaza tukio hilo kwa kimo chake kinachovutia uangalifu, akijifanya kuwa kielelezo. Kwa njia hiyo anajidai kuomba, lakini kiukweli anajikweza mwenyewe, akificha udhaifu wake katika usalama wake wa kudumu. Je anatarajia nini kutoka kwa Mungu? Anatarajia thawabu kwa ajili ya sifa zake, na kwa njia hiyo anajinyima mshangao wa bure wa wokovu, akiumba mungu ambaye hangeweza kufanya chochote isipokuwa kutia sahihi cheti cha ukamilifu unaodhaniwa. “ni mtu aliyefungwa kwa mshangao wote. Yote amejifungia mwenyewe, amefungwa kwa mshangao mkubwa wa huruma.” Ubinafsi wake hautoi nafasi kwa chochote kwa mtu yeyote, hata kwa Mungu. Na ni mara ngapi katika Kanisa tunafanya hivyo? Ni mara ngapi tumechukua nafasi yote pia, kwa maneno yetu, hukumu zetu, vyeo vyetu, tukiwa na imani kwamba tunastahili tu?"

Papa Francisko aliendelea kukazia: "Na kwa njia hiyo kile kilichotokea wakati Yosefu na Maria na Mwana wa Mungu akiwa tumboni mwake, walipobisha hodi kwenye milango ya ukarimu kinaendelea. Yesu atazaliwa katika hori kwa sababu, kama Injili inavyotuambia kwamba: “hapakuwa na nafasi kwa ajili yao katika nyumba ya wageni” (Luka 2:7). Na leo sisi sote ni kama mtoza ushuru, tuna au tunataka kuinamisha macho yetu na tunahisi, tunataka kujisikia aibu kwa ajili ya dhambi zetu. Kama yeye, tunabaki nyuma, tukiweka huru nafasi iliyotawaliwa na kiburi, unafiki na majivuno na pia, wacha tuseme hivyo, kwetu sisi maaskofu, mapadre, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, tukiweka huru nafasi iliyochukuliwa na kiburi, unafiki na majivuno. Hatutaweza kulitaja jina la Mwenyezi Mungu bila kuomba msamaha kutoka kwa kaka na dada zetu, kutoka katika Ardhi na kwa viumbe vyote. Hebu tuanze hatua hii ya Sinodi. Na tunawezaje kuwa Kanisa la sinodi bila upatanisho? Je, tunawezaje kusema tunataka kutembea pamoja bila kupokea na kutoa msamaha unaorejesha ushirika katika Kristo?

Papa Francisko alisemaM: "Msamaha, unaombwa na kutolewa, huzalisha maelewano mapya ambayo tofauti hazipingani, na mbwa mwitu na mwana-kondoo wanaweza kuishi pamoja, kwa ujasiri, mfano wa Isaya. (Is 11, 6). Katika uso wa uovu na mateso yasiyo na hatia tunauliza: Bwana huko wapi? Lakini ni lazima tujiulize swali, na tujiulize kuhusu majukumu tuliyonayo pale tunaposhindwa kuacha ubaya kwa wema. Hatuwezi kutarajia kusuluhisha mizozo kwa kuchochea jeuri ambalo linazidi kuwa la kikatili, tujikomboe kwa kusababisha maumivu, tujiokoe na kifo cha wengine. Tunawezaje kufuatia furaha iliyolipwa kwa gharama ya kutokuwa na furaha kwa kaka na dada zetu? Na hii ni kwa kila mtu kuanzia: watu wa kawaida, walei, watu waliowekwa wakfu, watawa wa kike na kiume, kwa kila mtu! Katika mkesha wa kuanza kwa Mkutano wa Sinodi, kukiri ni fursa ya kuanzisha tena imani kwa Kanisa na kuelekea kwake, uaminifu uliovunjwa na makosa na dhambi zetu, na kuanza kuponya majeraha ambayo hayajaacha kutokwa na damu, kuvunja minyororo ya uovu” (Is 58, 6)."

Mkesha wa Toba Oktoba 2024
Mkesha wa Toba Oktoba 2024

Baba Mtakatifu alisema "Tunasema katika sala ya Adsumu ambayo kwayo tutatambulisha maadhimisho ya Sinodi kesho: “Tunakandamizwa na ubinadamu wa dhambi zetu”. Na tusingependa mzigo huu upunguze kasi ya maendeleo ya Ufalme wa Mungu katika historia.Tumefanya sehemu yetu, hata ya makosa. Tunaendelea na utume kadiri tuwezavyo, lakini sasa tunawageukia ninyi vijana mnaosubiri kifungu cha ushuhuda kutoka kwetu, tukiomba msamaha kutoka kwenu pia ikiwa hajawa mashahidi wa kuaminika. Na leo katika kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Msimamizi wa kimisionari tunaomba maombezi yake."

Kipindi kifupi cha ukimya. Kisha, kila mtu alisimama na kuinamisha kichwa.

Baba Mtakatifu alianza tena akiomba: Ee Baba, tumekusanyika hapa tukifahamu kuhitaji mtazamo wako wa upendo. Mikono yetu ni tupu, tunaweza kupokea kile unachoweza kutupa tu. Tunakuomba msamaha kwa dhambi zetu zote, utusaidie kurejesha sura yako tuliyoiharibu kwa kukosa uaminifu wetu. Tunaomba msamaha, tukiona aibu, kutoka kwa wale ambao wameumizwa na dhambi zetu. Utupe ujasiri wa toba ya kweli kwa ajili ya uongofu. Tunaomba haya kwa kumwomba Roho Mtakatifu ili aijaze mioyo yake aliyoiumba kwa Neema yake, katika Yesu Kristo, Bwana wetu. Sisi sote tunaomba msamaha, sisi sote ni wenye dhambi, lakini sote tuna matumaini katika upendo wako Bwana. Amina.

Hairusiwi kumtazama mtu kutoka juu hadi chini labda kuinama na kumsaidia

Hata hivyo Baada ya Injili, Papa Francisko alisema: “Kwenu ninasema: Injili Takatifu ni njia yetu, ukweli wetu, maisha yetu. Ninawakabidhi ninyi ambao ni walinzi wa siku mpya katika Kanisa, linalotaka kuwa sinodi kwa ajili ya utume. Kwa kuwa neno lilifanyika mwili, neno la Yesu linatafuta miili yetu, hata iwe dhaifu na isiyo ya uaminifu. Sisi sote ni wenye dhambi, sote ni waombaji wa huruma za Baba, ndiyo maana tumeungama dhambi zetu. Sasa tutapokea baraka ya Mungu ambayo ni pumzi ya uhai, mahangaiko ya tumaini ambayo yanawaruhusu wale walioanguka kuinuka daima. Na tukumbuke sote, kaka na dada, kwamba mara moja tu, mara moja, inaruhusiwa kumtazana mtu kutoka juu kwenda chini kwa ajili ya kumsaidia, mara nyingine haiwezekani. Inaruhusiwa kutamzama mtu kuanzia juu hadi chini ili kumsaidia ainuke. Kumbukeni kwamba Injili lazima ilindwe na kutangazwa kwa mikono isiyo na hatia na moyo safi, na ikiwa yeyote kati yetu hana mikono isiyo na hatia, hana moyo safi, angalau kuwa na moyo wa toba.

Tafakari ya Papa katika Mkesha wa toba tarehe 1 Oktoba 2024
01 October 2024, 20:35