Tafuta

Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo na kwamba, kauli mbiu hii inachota amana na utajiri wake kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni vyombo na mashuhuda wa matumaini. Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo na kwamba, kauli mbiu hii inachota amana na utajiri wake kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni vyombo na mashuhuda wa matumaini.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko Kwa Vijana wa Jimbo Kuu la Madrid, Hispania, 2024

Jimbo kuu la Madrid, nchini Hispania, Jumamosi jioni, tarehe 5 Oktoba 2024 liliandaa “Mkutano Mubashara wa Madrid 2024” imekuwa ni fursa ya pekee kwa vijana wa kizazi kipya kufurahia jioni iliyopambwa kwa muziki, sala, na shuhuda mbalimbali. Hili ni tukio ambalo limeacha chapa ya kudumu katika nyoyo za vijana wa kizazi kipya. Mkutano huu umenogeshwa na kauli mbiu "Watu wenye furaha katika matumaini," Maandalizi ya Jubilei kuu ya miaka 2025 ya Ukristo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Tamko la Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo linanogeshwa na kauli mbiu “Spes non confundit" yaani “Tumaini halitahayarishi” Rum 5:5 na kwamba, kiini cha maadhimisho haya ni matumaini yatakayowawezesha watu waaminifu wa Mungu kutoka sehemu mbalimbali za dunia kufanya hija ya maisha ya kiroho mjini Roma sanjari na maadhimisho haya kufanyika kwenye Makanisa mahalia, ili kukutana na Kristo Yesu aliye hai na ambaye pia ni Mlango wa uzima. Rej, Yn 10:7.9. Mama Kanisa anaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini dhidi ya hofu na mashaka; ukosefu wa imani na furaha ya kweli. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo itakuwa ni fursa ya kupyaisha tena matumaini kwa kuongozwa na Neno la Mungu. Katika Tamko hili, Baba Mtakatifu anakazia kuhusu Matumaini katika Neno la Mungu ili kuamini, kutumaini, kupenda na kuvumilia kwa kutambua kwamba, wao ni mahujaji wa matumaini. Alama za matumaini zinazomwilishwa katika amani, kwa kujikita katika Injili ya uhai, maboresho ya magereza; huduma kwa wagonjwa, vijana, wahamiaji na wakimbizi, wazee na maskini.

Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo
Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa madhimisho ya Siku ya 39 ya Vijana Ulimwenguni kwa ngazi ya kijimbo itakayoadhimishwa tarehe 24 Novemba 2024 unanogeshwa na kauli mbiu: “Wale wanaomtumainia Bwana, watapiga mbio, wala hawatachoka” (Is 40,31). Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo, Jimbo kuu la Madrid, nchini Hispania, Jumamosi jioni, tarehe 5 Oktoba 2024 liliandaa “Mkutano Mubashara wa Madrid  2024” ambayo imekuwa ni fursa ya pekee kwa vijana wa kizazi kipya kufurahia jioni iliyopambwa kwa muziki, sala, na shuhuda mbalimbali. Hili ni tukio ambalo limeacha chapa ya kudumu katika akili na nyoyo za vijana wa kizazi kipya. Mkutano huu umenogeshwa na kauli mbiu “Watu wenye furaha katika matumaini.” Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo na kwamba, kauli mbiu hii inachota amana na utajiri wake kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko anayewataka vijana kuwa ni mahujaji na vyombo vya matumaini na upendo wa Mungu ambao kamwe haudanganyi. Vijana wengi walijiunga na mkutano huu, hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video amependa kuwaonesha uwepo wake wa karibu, ili kuwaongoza na kuwatia shime ili waweze “kucharika” usiku na mchana, ili wasije kuzeeka na hatimaye, kufa mapema.

Mkutano Mubashara wa Madrid 2024: Vijana Tumaini la Kanisa
Mkutano Mubashara wa Madrid 2024: Vijana Tumaini la Kanisa

Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu na kwamba, anawahamasisha kuhakikisha kwamba, wanashiriki kikamilifu, kwa kujenga umoja na udugu wa kibinadamu unaoshiriki katika kanuni maadili na utu wema; sanjari na utamaduni wa kusikilizana. Vijana wajenge utamaduni wa kuwasikiliza wazee ambao ni chimbuko la hekima ya watu; wazee nao wanapaswa kuwasikiliza vijana, ili kuendeleza mizizi ya maisha. Mti unaokata mizizi yake hauna utomvu tena. Huu ni mwaliko wa kushikilia mizizi yao kwa kuendelea kujikita katika ubunifu na kwamba, ujana usiokuwa na ubunifu huo “ni sawa na choka mbaya.” Vijana waoneshe ujasiri na kamwe wasikubali kupoteza furaha ya maisha yao ya ujana; waendelee kuwa wacheshi na Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na neema awajaze: ucheshi, neema na baraka.

Vijana Madrid 2024
06 October 2024, 11:28