Tafuta

2024.10.02 Wakati wa mahubiri ya Papa kwenye ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu,Papa aliomba kusindikizwa kusali kwa ajili ya amani tarehe 6 na 7 Oktoba. 2024.10.02 Wakati wa mahubiri ya Papa kwenye ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu,Papa aliomba kusindikizwa kusali kwa ajili ya amani tarehe 6 na 7 Oktoba.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ungana na wito wa Papa wa sala na kufunga Oktoba 7 ili kuomba amani duniani!

"Kuna hitaji,hasa katika saa hii ya kushangaza ya historia yetu,wakati pepo za vita na moto wa ghasia unaendelea kusumbua watu na mataifa yote.Ili kuomba zawadi ya amani kwa maombezi ya Maria Mtakatifu.Dominika nitasali Rozari Takatifu na kumwelekeza sala kwa Bikira".Papa Francisko anaomba kusali pamoja sala na kufunga Oktoba 6 na 7 ili kuomba amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 2 Oktoba 2024, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza Ibada ya Misa Takatifu  katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XVI wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu ambao utaendelea hadi tarehe 27 Oktoba 2024. Kama ilivyokuwa tayari kwa Siria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) na Sudan Kusini, Lebanon, Afghanistan, Ukraine na Nchi Takatifu kuanzia 2013 hadi 2023, Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena ametoa wito kwa siku ya Jumatatu tarehe 7 Oktoba 2024 ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kwanza ya shambulio la kigaidi la Hamas dhidi ya Israeli, kusali na kufunga kwa ajili ya zawadi ya amani. Na kwa hiyo tarehe 6 Oktoba atasali Rozari.

Haya aliyasema wakati anahitimisha mahubiri yake kwamba: “Ndugu na dada, tuanze tena safari hii ya kikanisa kwa jicho kuu kuelekea ulimwengu, kwa sababu jumuiya ya Kikristo daima iko katika huduma ya wanadamu, kutangaza furaha ya Injili kwa kila mtu. Kuna hitaji, hasa katika saa hii ya kushangaza ya historia yetu, wakati pepo za vita na moto wa ghasia unaendelea kusumbua watu na mataifa yote. Ili kuomba zawadi ya amani kutokana na maombezi ya Maria Mtakatifu, Dominika ijayo nitakwenda kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Maria Mkuu ambako nitasali Rozari Takatifu na kumwelekeza sala ya dhati kwa Bikira; ikiwezekana, pia ninawaomba ninyi washiriki wa Sinodi kuungana nami katika hafla hiyo. Na siku itakayofuata, tarehe 7 Oktoba ninaomba kila mtu aishi siku ya sala na kufunga kwa ajili ya amani ya ulimwengu. Twende pamoja. Hebu tumsikilize Bwana. Na tuongozwe na upepo wa Roho.”

Misa ya Ufunguzi wa Sinodi tarehe 2 Oktoba 2024
Misa ya Ufunguzi wa Sinodi tarehe 2 Oktoba 2024

Tarehe 6 Oktoba, ikiwa ni Dominika ya XXVII ya wakati wa kawaida, wakati wa sherehe zote za kiliturujia, Jimbo la Roma limetoa mwaliko wa kusali sala ifuatayo: Baba mwenye huruma, nguvu za Roho wako wa amani zikomeshe ukatili wa pambano la dunia linalokaribia zaidi, utikise mioyo yetu kutokana na kutojali, uwaongoze wale wanaoleta uharibifu na kifo na useme nasi tena kwa lafudhi ya matumaini. Tuombe."

Maaskofu wanaoudhuria Sinodi
Maaskofu wanaoudhuria Sinodi
03 October 2024, 09:54