Maktaba ya Kitume ya Vatican. Maktaba ya Kitume ya Vatican. 

Papa anahamisha sehemu ya Nyaraka na Maktaba ya Vatican kwenye Seminari Kuu ya Kirumi

Katika maandishi ya Papa Francisko yanabainisha juu ya kupanua nafasi zilizopo kwa taasisi hizo mbili kwa kutumia sehemu ya jengo na maeneo jirani katika eneo la Seminari ya Kipapa,ili kufanya urithi huo kutumika zaidi.Tume ya wawakilishi kutoka Sekretarieti ya Vatican,Nyaraka za Vatican na Maktaba ya Kitume itaundwa ili kubainisha aina za nyaraka zitakazohamishiwa katika mazingira mapya.

Vatican News

Tunachapisha  barua ya Papa Francisko kuhusiana na kuhamisha baadhi ya nyaraka za kitume na maktaba za Vatican katika Seminari Kuu ya Kipapa ya Roma ambapo anaandika kuwa:  “Utunzaji wa zamani wa kulinda  salama kwa matendo na nyaraka zinazohusu Utawala wa Kanisa la Ulimwengu, pamoja na kujitolea kwa maendeleo na usambazaji wa utamaduni, ni sifa bainifu za shughuli za Pango hifadhi za Nyaraka za Kitume na Maktaba ya Vatican.

Kuendeleza kazi ambayo tayari imeanzishwa na Watangulizi wangu, tangu Scrinium ya Kanisa la Roma, Taasisi hizi mbili leo hii zinaitwa kufanya upatikane  urithi huu wa thamani. Kwa hivyo, kufuata lengo la kuchangia katika usimamizi bora zaidi wa shughuli na uhifadhi wa mali, baada ya kupata habari inayofaa na maoni yanayofaa, NINATOA AMRI kwamba nafasi zilizopo kwa ajili ya Nyaraka za Kitume na Maktaba ya Kitume zipanuliwe, kwa kutumia sehemu ya jengo na mazingira yake ambayo katika eneo la nje la  Mtakatifu Yohane  huko Laterano inakaribisha Seminari Kuu ya Kipapa ya Kirumi, kulingana na waraka uliombatanishwa hapa.”

Kwa ajili hiyo, taasisi zinazohusika zitashirikiana kwa pamoja kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo, kulingana na uwezo wao, kuzingatia vifungu vinavyotumika, taratibu na maagizo ambayo yatakuwa muhimu kwa utekelezaji wa utaratibu wa kazi hii muhimu ambayo Makao ya Petro yanafanya kazi, maeneo katika huduma ya Kanisa na ulimwengu wa utamaduni. Wakati huo huo, ninaamuru kwamba Tume iundwe itakayoundwa na wawakilishi wa Sekretarieti Vatican, wa Pango Hifadhi Nyaraka za kitume na Maktaba ya Kitume ya Vatican, ili kuamua aina  gani za nyaraka zinazopaswa kuhamishiwa katika mazingira mapya. Tume itaweza kufanya kazi mara moja, sambamba na kazi ya ujenzi kwenye mpango huo. Masharti hayo yanapaswa kuzingatiwa kuwa thabiti na halali tangu kuchapishwa kwa Osservatore Romano.

Papa anahamisha baadhi ya Nyaraka za kitume na maktaba
12 November 2024, 12:26