Papa akutana na Sinodi Takatifu ya Kanisa la Malakara:tutembee,tusali pamoja na kufanya kazi pamoja!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akihutubia Jumatatu tarehe 11 Novemba 2024 na Sinodi Takatifu ya Kanisa, la Syro-Malankara, la mrithi wa mapokeo ya Kisiria ya Wakristo wa Mtakatifu Thomas alianza kusema kuwa “ Hakika hii ni siku ya furaha katika historia ndefu ya Makanisa yetu, kwani ni mara ya kwanza kwa Sinodi Takatifu ya Kanisa la Syro-Malankara Mar Thoma kulitembelea Kanisa la Roma kubadilishana kukumbatia amani na Askofu wake. Papa Francisko ameshukuru kwa uwepo wao na kwa maneno yake ya urafiki.” Amewakaribisha kila mmoja wao na aliomba wamfikishie salamu zake za heri na afya kwa Mji Mkuu wao, Heri zake pia Theodosius Mar Thoma. Salamu zake vile vile ziwaendee waamini wote: “Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo” (Rm 1:7). Kanisa lao, mrithi wa mapokeo ya Kisiria ya Wakristo wa Mtakatifu Thomasi na mapokeo ya Mageuzi, linajieleza kwa usahihi kuwa ni “Kanisa la kidaraja” kati ya Mashariki na Magharibi. Kama Neema ilivyoonesha, Kanisa la Mar Thoma lina wito wa kiekumene na si kwa bahati kwamba lilijihusisha na harakati za kiekumene mapema, na kuanzisha idadi ya mawasiliano baina ya nchi mbili na Wakristo wa mapokeo tofauti.
Mikutano ya kwanza na Kanisa la Roma ilifanyika wakati wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ambapo Philipose Mar Chrysostom, ambaye angekuwa Mkuu wa Kanisa hilo, alishiriki kama Mtazamaji. Hizi ni hatua ndogo zinazotuleta karibu. “Katika miaka ya hivi karibuni, Neema imeruhusu mahusiano mapya kustawi kati ya Makanisa yetu. Nakumbuka hasa wakati, mnamo Novemba 2022, nilipata furaha ya kumpokea, mpendwa Metropolitan Barnabas. Mawasiliano yetu haya yalisababisha kuanza kwa mazungumzo rasmi: mkutano wa kwanza ulifanyika Desemba iliyopita huko Kerala na unaofuata utafanyika baada ya juma chache. Papa Francisko kwa hiyo amefurahia mwanzo wa mazungumzo haya, ambayo “ninamkabidhi Roho Mtakatifu na ambayo natumaini yataharakisha siku ambayo tutaweza kushiriki Ekaristi hiyo hiyo, katika utimilifu wa unabii wa Bwana: “Watakuja kutoka mashariki na magharibi na kuketi mezani” (taz. Mt 8:11).” Katika safari hii ya mazungumzo, ningependa kuakisi mitazamo miwili: sinodi na utume. Kuhusu sinodi, ni muhimu kwamba mlitaka kufanya ziara hii kama Sinodi Takatifu, kwa kuwa Kanisa lako kimsingi ni la sinodi.
Kama mnavyojua, siku chache zilizopita Kanisa Katoliki lilihitimisha Sinodi ya kisinodi, ambayo pia ilihudhuriwa na Wajumbe ndugu kutoka katika mapokeo mengine ya Kikristo ambao waliboresha tafakari zetu. Mojawapo ya imani zinazooneshwa ni kwamba sinodi haiwezi kutenganishwa na uekumene, kwa kuwa yote mawili yanatokana na Ubatizo mmoja tuliopokea na juu ya sensus fidei yaani maana ya imani ambayo Wakristo wote wanashiriki kwa njia ya Ubatizo wenyewe. Hati ya Mwisho ya Sinodi hiyo inasema kwamba hatupaswi tu "kuzingatia zaidi mazoea ya sinodi ya washirika wetu wa kiekumene, katika Mashariki na Magharibi", lakini pia "kufikiria mazoea ya sinodi za kiekumene, hadi na kujumuisha aina za mashauriano" na utambuzi juu ya mambo ya pamoja na ya dharura ( 138). Kwa hiyo Papa amesema “, nina hakika kanisa lako, linaweza kutusaidia katika safari hii ya sinodi ya kiekumene. Ninakumbushwa yale maneno ambayo Zizioulas alisema kuhusu umoja wa Wakristo. Alikuwa mtu mkuu, mtu wa Mungu. Alisema: "Ninajua tarehe ambayo kutakuwa na umoja kamili kati ya Makanisa". Tarehe ni nini? "Siku baada ya Hukumu ya Mwisho". Aliongeza: "Lakini, wakati huo huo lazima tutembee pamoja, tusali pamoja na kufanya kazi pamoja". Wote pamoja.
Mtazamo mwingine ni ule wa utume. Kwa hakika, sinodi na uekumene pia havitenganishwi kwa sababu zote mbili zina kama lengo lao ushuhuda wenye matokeo zaidi kwa upande wa Wakristo. Hata hivyo, utume sio tu lengo la safari ya kiekumene; bali ni njia yake. Papa anaamini kwamba “kufanya kazi pamoja ili kutoa ushahidi kwa Kristo Mfufuka ndiyo njia bora zaidi ya sisi kukaribiana zaidi. Kwa sababu hii, kama Sinodi yetu ya hivi majuzi ilivyopendekeza, ni matumaini yangu kwamba siku moja tunaweza kusherehekea Sinodi ya kiekumene kuhusu uinjilishaji kwa kila mtu pamoja. Sinodi hii itasaidia kuhakikisha, kwa njia ya sala, tafakari na ahadi yetu ya pamoja, ushuhuda bora wa Kikristo, “ili ulimwengu upate kuamini” (Yh 17:21). Hapa pia, nina hakika kwamba Kanisa la Mar Thoma, ambalo lina mwelekeo huu wa kimisionari, lina mengi ya kutoa. Lakini lazima sote tufanye pamoja.” Papa amesema: Ninawashukuru tena katika Kristo wa ziara yenu.” Amewakakabidhi kwa maombi yao na kukuhakikishia yake pia. Na kumalizia walisali sala ya Bwana wetu.