Papa,Mtakatifu Bernard Mkuu na sifa tatu:kuhubiri,kukaribisha na kukuza amani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Uwakilishi wa Jimbo la Aosta na Shirika la Wakanoni wa Mtakatifu Bernard mkuu, Jumatatu tarehe 11 Novemba 2024 mjini Vatican. Katika hotuba yake alianza na salamu kwa wote na kueleza furaha yake ya kukutana nao wakati wanahitimisha Mwaka wa Jubilei iliyojikita na miaka 100 ya Kutangazwa kwa Mtakatifu Bernard wa Aosta kuwa Msimamizi wa wapanda milima, wasafiri na wakazi wa vilimani (Papa PIO XI, na Barua Quod Sancti, 20 Agosti 1923), vile vile Miaka 900 tangu kutangazwa Mtakatifu na miaka 1000 ya kuzaliwa kwake. Kwa hivyo Papa amesema kuwa umati wa nyakati mbalimbali zilizoambatana na wakati huu wa kusherehekea ulikuwa ni mfano wa Mtakatifu huyo wa Mlimani ambaye pia Papa ametaka kujikita na tafakari yake. “Tunaweza kufupisha baadhi ya sifa za kimsingi za kazi yake kwa kurejea maeneo matatu ya utekelezaji ambayo Mungu Mpaji alimjalia, ambayo ni muhimu sana hata leo, hii kutangaza, kukaribisha na kuhamasisha amani.
Kwanza kabisa tangazo. Bernard, Shemasi Mkuu wa Jimbo la Aosta, alikuwa mhubiri mwenye uwezo wa kugusa hata mioyo migumu zaidi, akiwafungulia zawadi ya imani na uwongofu. Aliweza kufanya tangazo hilo "uzoefu mkali na wa furaha wa Roho" (Waraka wa kitume Evangelii gaudium, 135) na alijitolea kwa utume huu kwa bidii hadi kifo chake, kilichotokea mnamo 1081 huko Novara, ambapo alikuwa anahubiri. Pili: kukaribisha. Papa Francisko amesema “ikiwa la kwanza ilikuwa ni Kutangaza na la pili ni Kukaribisha. Safari ya upendo ambayo ingemfanya kuwa maarufu, hata hivyo, inahusishwa na misheni nyingine alizokabidhiwa kwa utii: ile ya kuwatunza mahujaji na wasafiri waliovuka njia za Milimani karibu na Mlima Blanc(Mweupe) - njia ambazo bado zina jina lake leo hii na alikuwa karibu kuja Italia kutoka Ufaransa na Uswizi na kinyume chake katika safari ya usafiri wa kimataifa. Safari ilikuwa ngumu na ilikuwa na hatari ya kupotea, kushambuliwa na kufa kwenye barafu. Ili kuwatunza watu hawa, Bernard alianzisha hospitali mbili zinazojulikana sana, akikusanya jumuiya yao ya Wakanoni, ambao bado leo hii wanajitolea kwa huduma hiyo , waaminifu kwa kauli mbiu isemayo: Hic Christus adoratur et pascitur, yaani "Hapa Kristo anaabudiwa na kumwilishwa.”
Mpango wa mapendo ya kimwili na kiroho
Baba Mtakatifu ameendelea kueleza kuwa “Ni mpango wa mapendo muhimu, ya kimwili na ya kiroho, ambao una Ekaristi katikati yake, na ambao kutokana na sala unaongoza kwa kumkaribisha yeyote anayebisha hodi. Mfano wa kweli kwa leo pia: kukaribisha na kutunza mtu yeyote anayeomba msaada, katika mwili na roho, bila tofauti na bila kufungwa. Tangazo, ukarimu na hoja ya tatu ni mhamasishaji amani. Bernard mtunza amani. Kipindi kizuri, katika suala hili, ilikuwa ni safari yake kwenda Pavia, tayari akiwa mgonjwa, ili kujaribu kumshawishi Mfalme Henry IV aache nia ya kufanya vita dhidi ya Papa Gregory VII. Ilikuwa ni safari iliyogharimu maisha yake. Kiukweli, atakufa muda mfupi baada ya kurudi. Kama tunavyojua, jaribio lake halikufaulu. Walakini, hii inamfanya kuwa mtakatifu zaidi machoni petu, kwa sababu inatuonesha na kujishughulisha na shughuli nyeti na isiyo na uhakika, zaidi wa dhamana yoyote ya mafanikio.
Kuhamasisha amani, bila kukata tamaa, hata katika uso wa kushindwa: na ni kiasi gani cha haja ya ujasiri huu hata sasa! Papa Francisko amebainisha. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesema, kwa kuzingatia kwamba baadhi yao ni viongozi wa Mlimani (Alpine) na wakufunzi wanaofundisha kutembea kwenye theruji, Papa amependa kuhitimisha kwa kumkumbuka Mtakatifu wao Mlinzi kupitia alama mbili za milima: shoka la barafu na karamu ya kamba. Shoka la barafu la Mtakatifu Bernard lilikuwa Neno la Mungu, ambalo kwa hilo aliweza kuziba roho zenye baridi na ngumu zaidi; muungano wake ulikuwa jumuiya, ambayo alitembea nayo na kuwasaidia wengine kutembea - hata kwenye njia za hatari, kufikia lengo. Papa anatamani kila mtu atembee njia nzuri kama zao, kati ya milima mirefu, lakini zaidi ya yote kutembea ndani ya moyo. “Je, tuna ujasiri wa kutembea ndani ya moyo ili kujua moyo unahisi nini, moyo unasema nini? Amewabariki wao na watu wa Bonde la Aosta,na kuwaomba tafadhali wamwombee.