Papa akutana na wajumbe wa Mtandao wa kikatoliki wa Hisani(FADICA)
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 11 Noveba 2024 amekutana na Ujumbe wa Mtandao wa Kikatoliki wa Hisani(FADICA) ambapo katika hotuba yake amewakaribisha katika fursa ya hija yao, kongamano na mafungo katika Jiji la Milele. “Ni matumaini yangu kwamba siku hizi za tafakari na sala katika makaburi ya Mitume na wafiadini zitaongeza upendo wenu kwa Kanisa na kujitolea kwenu katika kueneza Injili na ujenzi wa ufalme wa Kristo wa utakatifu, haki na amani.," alisema Papa Francisko
Papa Francisko alisisitiza kuwa “Katika siku hizi, kama mnavyojua, Kanisa limejishughulisha na mchakato wa kutafakari juu ya asili yake kama jumuiya ya "sinodi", iliyosimikwa katika hadhi yetu ya pamoja ya ubatizo na wajibu wa pamoja wa utume wa Kanisa tunapokabiliwa na wakati wa mabadiliko ya milele na matokeo yake kwa mustakabali wa familia yetu ya kibinadamu. Papa amewashukuru sana kwa msaada wanaoutoa kwa ofisi za Vatican zinazotafuta kutambua alama za nyakati na kusaidia Kanisa la ulimwengu kujibu kwa hekima, upendo na kuona mbele mahitaji na changamoto za wakati huu.
Wakati huo huo, Papa amewashukuru kwa kutiwa moyo wao kwa utulivu kwa mipango mingi ambayo inaboresha maisha na utume wa Kanisa nchini Marekani. Kama "mtandao", FADICA kwa kawaida ni sinodi kwa kuwa inategemea maono ya pamoja, kujitolea na ushirikiano wa watu wengi, familia na mifuko ya hisani. "Ninaomba kwamba roho hii ya mshikamano na kujali kwa ukarimu kwa wengine daima iweze kukuzwa na hisia ya shukrani kwa ajili ya zawadi tele ambazo Bwana ametujalia na uzoefu wa ndani zaidi wa nguvu inayobadilisha ya upendo wake."
Papa amewapongeza wote kwa upendo huo, uliofunuliwa katika Moyo Mtakatifu wa Mwokozi, na wakati anawaombea wao pamoja na washiriki wote wa Mtandao wa Kikatoliki wa Hisani, Papa ameongeza kusema kuwa “mtazidi kupata furaha iliyotokana na juhudi zetu za kushiriki upendo wa Kristo na wengine”(Rej. Waraka wa Dilexit Nos, 216).” Na mwisho aliwabariki wao na familia zao na aliwaomba, tafadhali, wasisahau kumuombea.