Papa akutana na Waziri Mkuu wa Armenia,Nikol Pashinyan
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Armea Bwana Nikol Pashinyan, na ujumbe wake mjini Vatican Jumatatu tarehe 18 Novemba 2024 katika Jumba la kitume mjini Vatican.
Aliingia saa 2.55 na kuhitimisha mazungumza saa 3.25. Baada ya mazungumzo yao, walibadilisha zawadi ambapo Papa amempa kazi ya kisaa na picha ya udongo wa mfinyanzi yenye kichwa: “ upole na upendo” na Hati za kipapa ikiwemo ujumbe wa Amani kwa mwaka 2024. Wakati Waziri Mkuu huyo amempatia Papa Francisko Kitabu cha Maombolezo ya Mtakatifu Gregory wa Narek, kikiwa na kifuniko chenye mchoro kwa rangi ya dhahabu ambayo ni kazi ya fundi wa mkono huko Armeinia.
Zawadi ya Papa ina maana yake
Kuhusaiana na Picha ya Papa aliyomzawadia kiongozi wa Armenia inayoonesha sura ya Mtakatifu Francis wa Assisi kwa upande mmoja, ishara ya amani na heshima kwa ubinadamu na asili, na kwa upande mwingine sura ya ulimwengu unaotishiwa na uchafuzi wa mazingira. Kwa hiyo hii imetengenzwa kwa mbinu ya udongo wa mfinyanzi ambao ni laini na iliyoimarishwa na patina ya wax. Kazi ya sanaa inaeleza ujumbe wa upendo na ulinzi wa kazi ya uumbaji, ukichochewa na maneno ya Papa mwenyewe katika mahubiri yake ya tarehe 19 Machi 2013, kwa ajili ya Misa Takatifu mwanzoni mwa Upapa wak, wakati hu0o alisema: “Kulinda viumbe, kila mwanamume na kila mwanamke, kwa huruma na upendo, inafungua upeo wa matumaini, inafungua mwangaza wa nuru katikati ya mawingu mengi, inaleta joto la matumaini!”